Wasomi na Siasa Za Tanzania

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Kwa nyakati fofauti, wengi wetu tumejifunza katika historia ya nchi yetu kwamba moja ya sababu za msingi ambazo Mwalimu Nyerere alizitaja miaka 50 iliyopita kwamba ni kikwazo kwa Maendeleo ya taifa letu ni uhaba wa wataalam wa kusaidia kujenga taifa. Hivyo, katika miaka ya mwanzo ya uhuru, ilimlazimu Mwalimu na serikali yake kuagiza wataalam kutoka nje na hawa walikuwa wanalipwa na fedha za walipa kodi wa nchi yetu. Miaka 50 baadae, hali sio tofauti sana kwa maana ya kwamba bado kama taifa, hatuoni bado mchango wa kutosha kutoka kwa wataalam wetu katika kuendeleza nchi yetu. Tunabaki kujiuliza, tatizo ni nini hasa:

· Je, bado kama taifa tuna uhaba wa wasomi/wataalum?
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini wengi ni wababaishaji (wachakachuaji)?
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao kuchangia ujenzi wa taifa?
· Je, tunao wasomi/watalaam lakini hawathaminiwi?
· Je, tunao wataalam lakini wengi wamegeuka kuwa wanasiasa?

Nia yangu sio kutoa majibu kwa maswali haya bali kuchokoza mada huku nikijaribu kutoa maoni yangu kadhaa juu ya jambo hili. Kwa sasa nitajikita zaidi kwenye kujenga hoja kwamba moja ya tatizo lililopo ni kwamba wasomi/watalaamu wetu wengi wamegeuka kuwa wanasiasa.

Katika mazingira yetu, tunapozungumzia Siasa, ni vigumu kutenganisha neno hili na dhana ya Siasa ya Vyama. Kwa maana nyingine, in Tanzania, politics is partisan politics. By tradition, vyama vya siasa uhakisi na kukimu zaidi matakwa na mahitaji ya watawala kuliko matakwa na mahitaji ya jamii. Ni jambo la kawaida kwa vyama vya siasa kutumia muda mchache sana kujishughulisha na matatizo/changamoto zinazokabili jamii na badala yake kujikita katika masuala yanayohusiana na uongozi na kutwaa madaraka. Suala hili linapotokea kwenye jamii maskini kama Tanzania, jamii ambayo hakuna mjadala kwamba haina Dira ya Maendeleo inayoeleweka kitaifa, hili ni tatizo. Kwa mfano, ukimuuliza mtanzania wa kawaida kwamba, je dira ya taifa lako ni nini? Wengi watakujibu kwamba dira yetu ni MKUKUTA au MKURABITA. Ni watanzania wachache ambao watatamka “DIRA 2020” – na hata hivyo, huu ni upuuzi kwani Dira hii haikutengenezwa na watanzania bali wahisani kupitia IMF na World Bank. Kwahiyo sio Dira inayotokana na watanzania. Lakini mbaya zaidi ni kwamba, katika kujibu swali juu ya dira yetu ya taifa, watanzania wengi watakujibu kisiasa zaidi kwani huo ndio ufahamu wa wengi – yani katika mazingira ya ilani za vyama vyao vya siasa. Huu ni ujenzi wa janga kubwa sana la kitaifa kwa siku za usoni.

Kwa mtazamo wangu, ni muhimu katika mijadala juu ya Maendeleo ya Taifa, tukaanza kupunguza siasa za vyama kwani inazidi kutugharimu kimaendeleo. Ni muhimu tukaanza kujadili na kupangiaa Maendeleo ya Taifa letu katika mazingira ambayo ni over and above partisan politics. Mimi nadhani wenye uwezo wa kutufikisha huko ni wasomi (ambao ntawaita - intellectuals). Kabla sijaenda mbali, ni vizuri nikafafanua an intellectual ni mtu wa namna gani: An intellectual ni mtu anaetumia akili yake kwa ubunifu, lakini muhimu zaidi mtu anaetumia intelligence zaidi kuliko emotions or instincts. Hapa, maana ya intelligence ni – uwezo wa kuchanganua, kutambua, na kuelewa jambo. Na na ndio maana intellectuals katika jamii yoyote ile wana uwezo mkubwa wa kuona masuala mbali mbali over and above partisan politics, hawa yale yenye maslahi kitaifa.

Tofauti na miaka ya nyuma, Tanzania ya leo imejaliwa kuwa na wasomi wengi sana waliotokana na vyuo vyetu vikuu (ukiachilia wale waliosomeshwa na walipa kodi nje ya nchi). Vyuo vikuu ni taasisi zenye umuhimu wa kipekee wa kupangilia na kuendeleza a body of intellectual thought, kitu amhacho jamii inaweza kuakisi. This body of intellectual thought is supposed to be over and above mambo ambayo ni dhahiri/yanayoonekana/eleweka kwa urahisi. Jamii kama jamii hutingwa na many complex issues; na tatizo ukua zaidi wanasiasa wanapoingiza siasa katika complexity iliyopo tayari ndani ya jamii; kitendo hiki huzidi kuwagharimu na kuwaumiza watanzania kimaendeleo. Lakini kwa vile wasomi wana nafasi na uwezo wa kushughulika na masuala mbalimbali ya kijamii in a manner ambayo ni over and above partisan politics, hawa ndio wenye jukumu kubwa la kuisaidia jamii yetu iondokane na miaka 50 ya umaskini ambao kwa mshangao mkubwa na bila aibu, CCM imeutungia kauli mbiu ya Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele.
An intellectual body ni kama kioo cha jamii – kwa maana ya kwamba inaipa jamii taswira yake. Wasomi wa nyanja mbali mbali (politics, law, geology, engineers, journalism, medicine etc) wana uwezo na wajibu wa kutuelezea watanzania tunaonekana vipi kama jamii. Wasomi wana uwezo na wajibu pia to ‘articulate’ our hopes and fears; kutupa tahadhari juu ya hatari iliyopo mbele yetu; na vile vile kutusaidia kutupatia maana ya vitu ambavyo wanasiasa wetu aidha wanavipotosha, hawavielewi au wanafanyia mzaa kwa faida zao binafsi.

Ninapoizungumzia zaidi CCM ni kwa sababu hadi sasa, ni chama pekee ambacho miaka nenda miaka rudi (kwa miaka 50), ndicho kilichopewa dhamana ya kutuongozi kama taifa. Hivyo ni muhimu nikajadili aina ya viongozi wa CCM ya leo kwa mujibu wa maoni yangu. CCM in aina kuu tatu ya viongozi wa kisiasa:

1. Wanaitikadi Feki: Wanaitikadi wa dhati CCM hawapo tena kwani waliondoka na Mwalimu Nyerere. Wanaitikadi wa leo ni wale wajipambanua kama wana itikadi wa kijamaa, lakini wanadanganya wananchi huku wakitambua wazi kwamba CCM hakikuwaandaa watanzania kuhamia kwenye mfumo wa soko huria kutoka kwenye ule wa awali wa Ujamaa. Ndio maana watanzania wengi leo hii wamebakia kuduwaa na wasijue jinsi gani ya kukabiliana na maumivu ya sera za soko huria huku viongozi wanaohimiza CCM ni chama cha kijamaa wakiishi maisha ya ubepari uliopitiliza. Ni wajibu wa wasomi kurekebisha hili, sio wanasiasa.

2. Wapambe: Hili ni kundi la pili la viongozi wa kisiasa ndani ya CCM ya leo. Enzi za uchifu, hii ilikuwa ni ajira rasmi. Lakini leo hii, watu huteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali lakini unofficially, kazi yao ni upambe ambapo shughuli yao kubwa huwa ni to ‘amuse’, ‘cheer’ and ‘charm’ their masters (waliowapa madaraka). Hivyo ndivyo wanavyofanikiwa kuhudumia matumbo yao na familia zao. Mbali na kufanya shughuli zao kupitia vyombo vya habari, wapambe wapo hata ndani ya bunge, CCM – NEC na kamati kuu ambapo kazi yao kubwa ni kuwafagilia wakubwa waliowapa madaraka au fadhili kampeni zao, lakini muhimu zaidi, kusaidia CCM to divert attention ya umma from major issues of the day. Wapambe ni nuksi na kama msomi, ukikwaruzana nao, ni rahisi sana kukumaliza kibiashara, career-wise na hata kimaisha.

3. Wachochezi (Political trouble makers) – kundi la tatu ni lile la wachochezi. Kazi kubwa ya watu hawa ni kuushawishi na ku-bamboozle umma, na ni mabingwa wa kutumia vyema prejudices na stereotypes zilizopo kwenye jamii yetu kwa maslahi ya CCM. Viongozi hawa huwa hawaheshimu mantiki (logic), human decency, consistency na hawana muda kusoma alama za nyakati. Misamiati na kauli mbiu nyingi za CCM hutokana na viongozi wa namna hii wakisaidiwa na wenzao (wapambe na wanaitikadi feki). Lakini muhimu zaidi ni kwamba, hawa ni mabingwa wa kupika uongo mbalimbali kisha kuujengea hoja na propaganda kwamba huo ndio ukweli uliosadidika, usiopingika na unaotakiwa kuabudiwa. Na iwapo anatokea mtu mwingine kupingana nao, basi ubatizwa kila aina ya majina – muhasi, haramia, adui, mhuni, mkabila, n.k, na mara nyingine maisha yako yanaweza kuwa hatarini. Wachochezi hawana muda wa kuheshimu dhana ya uhuru wa mawazo; huwa hawaoni any merit on a political opponent (mfano tazama tabia na kauli zao dhidi ya upinzani bungeni) na badala yake wanajaribu kuwatuhumu wale wote wanaowa ‘challenge’ kwa mbinu za udini, ukabila, ukanda, n.k. Viongozi wa namna hii ni mabingwa wa ku-appeal on stereotypes, prejudices, emotions, fears, na expectations za umma kwa kujenga propaganda based on themes za kidini, kikabila, ukanda n.k. Wachochezi ndio hutumika zaidi katika kuzima hoja za wasomi zinazolenga maslahi ya taifa.

Nini nafasi ya wasomi?

Tofauti na viongozi niliowajadili, kwa kawaida wasomi huwa ni ‘great thinkers’. Tofauti kubwa iliyopo kati ya wasomi na viongozi niliowajadili ni kwamba, wakati wanaitikadi feki, wachochezi na wapambe ni kawaida kujichukulia madaraka mikononi kuifanyia jamii maamuzi, wasomi wajibu wao ni kusaidia wananchi kujenga uwezo “to think for themselves”. Ni tofauti hii kubwa baina ya viongozi hawa na wasomi ndio inayofanya viongozi wengi wa kisiasa kuwapiga vita wasomi kila wanapojitokeza kutoa maoni yao kuhusu muhstakabali wa taifa letu. Na mbaya zaidi ni kwamba, sehemu kubwa ya jamii bado inaamini wanasiasa na kuliko wasomi.

Kwa viongozi wa kisiasa, wasomi ni watu wabaya na wa hatari sana. Hii ni tofauti na enzi za Mwalimu Nyerere kwani miaka ya 1960s – 1970s, kila wakati taifa lilipokuwa linakabiliwa na changamoto mbalimbali, Mwalimu alikuwa na utamaduni wa kwenda Chuo Kikuu (Mlimani) kukutana na kujadiliana na wanafunzi. Ndio maana tofauti na leo, ilikuwa ni mara chache sana kwa serikali ya Mwalimu kukwaruzana na wasomi. Moja ya matukio machache ni lile la kuwalazimisha wasomi kujiunga na JKT ambapo Samuel Sitta na wengine walijikuta katika matatizo pale walipopinga na Mwalimu juu ya hilo. Kwa ufupi, enzi za Mwalimu, Mlimani became “a symbol of expression of critical intellectual thought”. Tofauti na enzi za Mwalimu, leo hii hatusikii wasomi wakishirikishwa na serikali katika mijadala na maamuzi ya kujenga taifa letu. Na ni nadra sana kusikia viongozi wa CCM wametembelea vyuo vikuu kwenda kubadilishana mawazo na wasomi. Ni kama vile wanawaogopa na hakuna jamii hata moja duniani iliyopiga hatua kimaendeleo kwa kuwaogopa au kutofautiana na wasomi. Katika Tanzania ya leo ni vigumu sana kuyasikia mawazo ya wasomi. Ikitokea bahati basi ni kupitia vipindi vya televisheni ambavyo sio watanzania wengi wanapata nafasi ya kuvitazama, let alone kujua in advance vipindi vitarushwa lini. Lakini mbaya zaidi ni kwamba hata mawazo na michango ya wasomi hawa huishia kuwa soga tu kwani ushauri wao haufanyiwi kazi yoyote na serikali.

Ni desturi pia kwa viongozi wengi wa kisiasa (CCM) kujenga hoja (chini kwa chini) kwamba wasomi ni watu ambao wapo too academic, too theoretical; wasomi hawaelewi reality; wasomi ni arm chair critics na wamejaa destructive criticisms. Hoja hizi ni za kawaida hasa nyakati za chaguzi mbalimbali za CCM. Kwa mfano, mwaka 2005 kulikuwa na fitina nyingi sana kwamba mgombea – Professor Mwandosya hafai kuwa Rais kwani Tanzania haina mahitaji na Rais ambae ni professor. Hata katika nafasi za ubunge na udiwani, wasomi hujengewa chuki na fitina kubwa. Lakini viongozi hawa hawa wa kisiasa baadae hushangaza pale wanapopigana vikumbo kutafuta degree za kuchakachua, huku wengine wakitafuta degree za PhD kwa kila njia ili na wao waonekana wa maana mbele ya jamii.

Tukirudi kwenye hoja kwamba wasomi hawafai kwani ni watu waliojaa theory pekee, as a matter of fact, kwa msomi wa kweli na alie makini, kuitwa too theoretical sio matusi kwani kazi kubwa ya msomi is to theorize reality na hivyo ndivyo msomii uzidi kuelewa ukweli wa suala husika. Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba - Wanasiasa wa CCM wanaposema wasomi kazi yao kubwa ni ‘destructive criticisms’, na sio ‘constructive criticisms’, wanacho maanisha hapa ni kwamba: Yale yote ambayo wanasiasa hawa au CCM hawataki kuyasikia au hawataki wananchi wayaelewe, basi hayo yote ni desctructive; Lakini yale yote ambayo wao au CCM inayaunga mkono, yale ambayo hayakiweki CCM katika hatari ya kuanguka kisiasa, na hayasaidii kuamsha watanzania kutoka kwenye usingizi mzito wa miaka 50 ya umaskini, basi hayo yote ni constructive. Isitoshe, ni dhahiri kwamba katika Tanzania ya leo, hakuna msomi makini ambae anaweza kujenga hoja na asionekana hafai machoni mwa CCM. Kwa mfano, zipo taarifa zisizo rasmi kwamba hata ndani ya vikao vya baraza la mawaziri, wapo mawaziri kadhaa ambao uonekana na mawaziri wenzao kwamba wanachafua hali ya hewa kutokana na hoja zao kulenga zaidi maslahi ya taifa - over and above partisan politics.

In actual fact, constructive criticism ni ile inayolenga kuondokana na existing dominant, unfair, unjust and unequitable relationship ndani ya jamii yetu ya Tanzania chini ya utawala wa miaka 50 wa CCM. Ndio maana it turns out kwamba any serious criticism ya wasomi ni Destructive kwani - such criticism uhimiza the need to Construct a new Tanzania. Kwa mfano, watanzania wamepitia tabu kubwa sana kutafuta katiba mpya ambapo kwa miaka mingi wasomi wamepigana kufa na kupona na utawala wa CCM (kihoja) na hatimaye kupata ushindi dhidi ya CCM. Ni muhimu kwa wasomi kuendeleza juhudi za aina hii kwani mbali ya suala la katiba Mpya ambalo dhahiri ni non-partisan, yapo mengine mengi ambayo wasomi wanaweza kusaidia ili watanzania wapigie hatua kimaendeleo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom