Elections 2010 Wasomi na chaguzi zao

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Hivi sasa kuna harakati za uchaguzi katika chuo cha mzumbe lakini cha kujiuliza ya kuwa kwanini wasomi wetu tuliotarajia watoe mfano bora kwa kuchagua watu kwa sera na si nini wamewapa , inasikitisha kuona wasomi wetu wanapewa pombe kama sehemu ya kampeni na kuwa ndicho kitu cha kuwashawishi kumchagua mtu.

je kama wasomi wetu hawajaelimika katika kufanya chaguzi zetu ni nani atayeonyesha mfano bora kwenye mabadiliko ya kweli?
 
shida itakuja kama watakunywa pombe na hatimaye kumchagua liyetoa pombe!
Kama wanakunywa lakini akachaguliwa mwingine ni ujasiri wa kuigwa!
 
shida itakuja kama watakunywa pombe na hatimaye kumchagua liyetoa pombe!
Kama wanakunywa lakini akachaguliwa mwingine ni ujasiri wa kuigwa!
kwa ujumla wasomi wetu wameshindwa kutumia nafasi yao kuelimisha jamii , kwani mara zote wanatoa pesa za pombe ndio wanaoshinda chaguzi,

nini kifanyike kugeuza jamii yetu
 
Back
Top Bottom