Wasomi msikate tamaa, elimu haina mbadala

diranqhe

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
1,268
2,000
WASOMI MSIKATE TAMAA, ELIMU HAINA MBADALA

WanaJF natumaini mko wazima.

Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi, chama kiendelee. Leo nimeona nitumie haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kuhusu wasomi wa nchi hii. Siku za hivi karibuni kumezidi kutokea hali ya wengi kubeza wasomi kwamba elimu haijawasaidia wao wenyewe wala jamii zao kuinuka kiuchumi. Yaani kuanzia mtaani hadi bungeni wasomi wanabezwa. Inasikitisha sana. Utasikia jamaa ana masters lakini anagongea hela ya vocha.

Kwanza kabla ya kuendelea zaidi ningetoa ufafanuzi kuhusu wasomi ninaomaanisha hapa. Ninamaanisha wale wote waliofika chuo kikuu. Lakini katika hao wasomi pia tuwatoe wale wanaoshindwa kutofautisha R na L kwenye maandishi yao. Wale wanaoandika "awo" badala ya "hao", wale wanaotuma msg wanaandika xaxa, ki2, tante, tenkyu, nk. Pia kama huwezi kuongea kiingereza kilichonyooka kwa dakika tatu ninakutoa kwenye kundi la wasomi. Wasomi ninaomaanisha hapa ni walioelimika na walipokuwa chuo walifanya bidii. Yaani watu wanaojiamini kupitia usomi wao na wasio na mambo ya ovyo.

Wanaobeza wasomi ni kutoka lile kundi kubwa la watu ambao hawakubahatika kupata elimu nzuri kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo zilizo ndani na nje ya uwezo wa kibinadamu. Kuna ambao huenda walikosa elimu kutokana na kukosa namna baada ya kuondokewa na wazazi/walezi na sababu zingine kama hizo. Na kuna wale ambao hawana elimu ya kutosha kwa maana ya kufeli mitihani yao kwenye ngazi mbalimbali yaani WANAKESHA LAKINI HAWAPANDISHI. Haya makundi mawili kwa pamoja wanaunda kundi kubwa la watu wajulikanao kama VILAZA.

Lawama kuu kwa wasomi ni kuwa na vyeti vingi ila kipato duni. Na watoa lawama huenda mbali kwa kutoa mifano ya watu ambao hawakusoma lakini ni matajiri wakubwa. Niseme kwamba hao matajiri ni wachache mno... kundi la vilaza hutoa matajiri wachache mno. Na hata hao matajiri ukiwafuatilia wengi wao wamefika walipofika kupitia njia nyingi zisizo za kihalali. Pia biashara nyingi za matajiri kutoka kundi la vilaza hazina ubunifu wowote ndo maana wakipatwa na janga kidogo hufilisika kirahisi na kuishia kusema wamerogwa. Kundi la vilaza hutoa mafukara wengi sana ambao wanasiasa huwatumia kama mitaji. Na watoa lawama wengi ni wale maisha yamewashinda au hawajiamini. Kiasili hakuna kilaza anayeweza kujiamini mbele ya msomi. Matokeo hutumia ujanja wa kumvuruga msomi ili aingie mtego wa kujibizana nae. Wasomi wengi wako na maisha ya middle class.. sio matajiri wala maskini. Na bado wasomi sio wengi kwenye jamii. Bado nchi yetu inahitaji kutengeneza wasomi wengi zaidi. Hawa vilaza waliotapakaa kila kona ya nchi ndo wanafanya jitihada za kujikomboa zinakuwa ngumu.

Niwasihi wasomi wenzangu kwamba hata kama kwa sasa ana kipato duni asikate tamaa asonge mbele. Na wasomi tusiwe waoga kujitosa kufanya mambo makubwa. Wasomi ndo huleta mabadiliko. Kwa mfano msomi mwenzetu Fred Vunjabei anakimbiza vilaza kwenye nguo waliozoea kufanya biashara kimazoea. Hata CHADEMA enzi za uhai wake ilikuzwa zaidi na wasomi wa vyuo vikuu. Bila hivyo kile Chama kisingekuwa kikubwa kabla ya kifo chake. Nimalize kusema nchi haiwezi kwenda mbele bila wasomi ila inaweza songa mbele bila vilaza.
 
joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,333
2,000
1.Vilaza wa standard 7 tuko poa kuliko nyie wasomi. Mmesoma ila mna uwezo wa kukalili vitu ambavyo haviwasaidii.

2.Ndiyo maana mkija kwenye ground hamna akili za maisha. Hata hela za kwenda kuhangaika kutembea na mibahasha yenu huwa mnatuomba huku viatu vimeenda upande. Umasikini umewakaba kila kona.

3. Aidha, wasomi wanapoteza miaka mingi na pesa nyingi kusoma halafu mwisho wa siku anaenda kupokea laki 400k kwa mwezi wakati sisi VILAZA huwa tunatengeneza hiyo laki 400k kwa siku huku Kkoo.
 
Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,267
2,000
1.Vilaza wa standard 7 tuko poa kuliko nyie wasomi. Mmesoma ila mna uwezo wa kukalili vitu ambavyo haviwasaidii.
Kama vipi havisaidii
Wewe kipi kinakusaidia ??
2.Ndiyo maana mkija kwenye ground hamna akili za maisha. Hata hela za kwenda kuhangaika kutembea na mibahasha yenu huwa mnatuomba huku viatu vimeenda upande. Umasikini umewakaba kila kona.
Reserch please...ikiwa hiki umeendika kwenye platform walioianzisha wasomi
3. Aidha, wasomi wanapoteza miaka mingi na pesa nyingi kusoma halafu mwisho wa siku anaenda kupokea laki 400k kwa mwezi wakati sisi VILAZA huwa tunatengeneza hiyo laki 400k kwa siku huku Kkoo.
Form Four Failure ambae si msomi anapoteza miaka 11 shuleni

Graduate miaka 16

Tofauti ni miaka mitano tu.
 
Hii comment yako ni ya kupuuzwa na umma wa wasomi kwasababu imejaa hisia badala ya uhalisia.
 
Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,703
2,000
Kama vipi havisaidii
Wewe kipi kinakusaidia ??

Reserch please...ikiwa hiki umeendika kwenye platform walioianzisha wasomi

Form Four Failure ambae si msomi anapoteza miaka 11 shuleni

Graduate miaka 16

Tofauti ni miaka mitano tu.

Hahaha Mkuu huyu KILAZA amelishwa tango pori huko kijiweni, ajui yeye ametumia na kupoteza miaka 11 kutafuta Ziro, leo anavimba eti msomi kapoteza muda shule VILAZA bhana wana tabu sana .
 
palsa

JF-Expert Member
Apr 24, 2011
1,217
2,000
1.Vilaza wa standard 7 tuko poa kuliko nyie wasomi. Mmesoma ila mna uwezo wa kukalili vitu ambavyo haviwasaidii.

2.Ndiyo maana mkija kwenye ground hamna akili za maisha. Hata hela za kwenda kuhangaika kutembea na mibahasha yenu huwa mnatuomba huku viatu vimeenda upande. Umasikini umewakaba kila kona.

3. Aidha, wasomi wanapoteza miaka mingi na pesa nyingi kusoma halafu mwisho wa siku anaenda kupokea laki 400k kwa mwezi wakati sisi VILAZA huwa tunatengeneza hiyo laki 400k kwa siku huku Kkoo.
Hakuna mbadala wa elimu..Acha propaganda. Usisomeshe watoto wako basi.
 
cool d

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,069
2,000
Elimu haina mbadala na ina muda wake wa kujitafuta, watoto wanatakiwa kutafuta elimu hata kwa kulazimishwa na wakubwa yaani watu wazima watafute pesa ya kuhudumia watoto wasome sasa mtu mzima akisema elimu haina maana maana yake muda wake wa kusoma akiwa mtoto hakuitafuta elimu kitu kinachofanyima maarifa hata Kama ana pesa.
 
sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,038
2,000
Msomi wa Tanzania anamaliza chuo hajawahi kujisomea hata kitabu kimoja cha elimu binafsi,

Mtu hajawahi kusoma hata vitabu muhimi kama vya rich dad poor child, how to influence people, art of war, 40 rules of power, n.k.....huyo ni mzigo tu wala hakuna jina lengine.
.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,801
2,000
Hili tatizo la kuchanganya L na R linakuwa kubwa kadri muda unavyozidi kwenda mbele.

Hadi matangazo mitaani watu wanachanganya hizi herufi siku hizi!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom