BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,849
Wasomi mna wajibu mkubwa kuondoa umasikini-Pinda
Waandishi Wetu
Daily News; Thursday,August 07, 2008 @00:03
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka wasomi, watafiti na wanataaluma kuwa wazi kukosoa sera ya uchumi kama wanaona haiko sahihi katika kuondoa umasikini wa wananchi. Pinda alisema wasomi hao wana jukumu la kuhakikisha sera zinazotungwa na serikali zinakuwa za manufaa kwa jamii na pale wanapoona mambo hayaendi pia wanatakiwa kuwa huru kuzikosoa pale inapowezekana.
Ndio maana nasema wataalamu lazima sasa watoe maoni yao na pale wanapoona sera tulizonazo hazisaidii kupunguza umasikini waseme na wakosoe kwa uwazi, alisema Pinda. Waziri Mkuu aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kimataifa unaojadili juu ya sera za maendeleo ambao umeandaliwa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mkutano huo unashirikisha wanataaluma, watafiti na watunga sera wa Tanzania na baadhi ya washiriki wanatoka katika bara la Ulaya, Afrika na India. Alisema tafiti za wasomi zina umuhimu mkubwa kwa jamii hasa katika utatuzi wa matatizo kadhaa yanayoikabili jamii katika maisha yao ya kila siku. Alisema wasomi na watafiti wanatakiwa kuhakikisha kazi zao zinatoka nje ya kuta za vyuo vikuu na kwenye maktaba.
Alisema tafiti hizo zisiishie kwenye makabati ya vitabu na kuwanufaisha watu kwani wananchi pia wana haki ya kujua tafiti wanazofanya wasomi hao. Naye Profesa Thadeus Sata wa IFM alisema wameitisha mkutano huo kwa lengo la kuangalia sera ya uchumi na mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa uchumi.
Katika tukio lingine Pinda amekemea tabia ya baadhi ya madaktari na maofisa wa Afya nchini ya kuuza dawa na vifaa vya hospitali ambavyo vinapelekwa na Serikali mikoani kwa ajili ya kuhudumia wananchi. Akipokea msaada wa dawa juzi Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Heshima wa Jiji la Hamburg la Ujerumani kwa Tanzania, Juergen Gotthardt kupitia taasisi ya Action Medeor, Pinda aliwataka wanaofanya vitendo hivyo kuacha mara moja.
Aliwataka madaktari wa mikoa na wilaya kusimamia kwa makini dawa zinazopelekwa katika maeneo yao ili zitumike kwa matumizi yaliyokusudiwa. Taasisi hiyo ya Ujerumani ilitoa jumla ya dawa zenye thamani ya Sh milioni 5.5 kwa ajili ya zahanati 20 na vituo vya afya vitano vya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Rukwa.