Wasomi Mbona Mnalia Sana Ajira Za Majeshi?

Mtumaini Mungu

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
879
1,061
Ee Bwana, Mtakatifu Mungu wetu sifa na utukufu ni Mali Yako nami kwa unyenyekevu mkubwa navirejesha kwako Sasa na hata Milele.

Ndugu watanzania wenzangu, hapa karibuni zimetolewa nafasi nyingi za ajira katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, kuanzia Jeshi la Polisi Tanzania chini ya Afande IGP Simon Sirro, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Hata idara ya uhamiaji.

Cha kushangaza ni kuwa wale ambao miaka ya nyuma walikuwa wanaukimbia huu "mgari" wa majeshi kutokana na shuruba na ugumu wa kazi leo hii wanaulilia na kuponda kuwa kwanini ajira hizi zinatolewa kwa waliofeli?

Wapo watu ambao wamefika mbali na kuanza kuyaponda majeshi yetu kuwa yanapoteza muelekeo kwa kuchukua vijana waliofeli kidato cha nne, Mimi naomba niwaulizeni Kwani hapo zamani majeshi yalikuwa hayachukui watu waliofeli? Watu wa darasa la saba?

Kazi za Majeshi ni kazi ambazo msingi wake mkuu ni "AMRI".. Hao waliofeli wanaenda huko kufanya kazi kwa kufuata amri, Na hata Ukichukuliwa wewe msomi bado utahitajika kufuata AMRI za wakuu wako bila kujali PHD yako ya kwenye vyeti.

Msomi ukiingia huko kwenye Majeshi bado huna nafasi ya KUHOJI au KUFANYA MAMBO kinyume na Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa, ni Lazima ufate Amri Kama ilivyo kwa Wale waliofeli.. Bila shaka kwa sasa vijana wanaohitajika ni wale ambao kazi na majukumu yao yanalandana na elimu zilizo ainishwa, watakapo hitaji wenye elimu za juu au za fani/taaluma tofauti na hizo zilizo ainishwa watawaita.

Ushauri wangu kwa waziri anayehusika na masuala ya kazi na ajira, Huku mtaani kuna wahitimu wengi na hawana ajira, tengenezeni mifumo ya kuwatumia hawa vijana ili kuipa thamani elimu yao na kurudisha kile walichokitumia kuitafuta hiyo elimu.

Nyie vijana wenzangu, wenye four zile za mwisho mtakaopata nafasi huko majeshini.. Ushauri huu mmepewa na YESU KRISTO WA NAZARETH...

Luka 3:14
"Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu."

Ee Mungu Uturehemu sawasawa na wingi wa Fadhili Zako.
 
Tena bora sahivi wanachukua form zamani ilikua la saba tu na ndo asilimia kubwa wasoja wengi wa zamani ni la saba, sahiv kutokana na uchache wa ajira wasomi wameona wakimbilie huko tu mkuu
 
Chuo kikuu mdebwefo akafamye nini jeshini, kwanza umri umemtupa.
Jeshi huajiri vijana shuoavu wenye miaja 18 -25 .
Wenye proffessional mwisho miaka 45/35 japo sina uhakika.
Wewe na dugrii yako haufai tena kuwa mshika bunduki, digrii holder ukaue watu kweli upo tayari kuua kama wale jamaa walivyomuua hamza?
Fikiri mara mbili
 
Chuo kikuu mdebwefo akafamye nini jeshini, kwanza umri umemtupa.
Jeshi huajiri vijana shuoavu wenye miaja 18 -25 .
Wenye proffessional mwisho miaka 45/35 japo sina uhakika.
Wewe na dugrii yako haufai tena kuwa mshika bunduki, digrii holder ukaue watu kweli upo tayari kuua kama wale jamaa walivyomuua hamza?
Fikiri mara mbili
Chukua hatua
 
Back
Top Bottom