Wasomi kulaumu Kambi ya Upinzani kuwa bubu sio sahihi

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Nimeshangazwa Na hao wanaojiita Wasomi Kwa kuilaumu Kambi ya Upinzani Bungeni kuwa Bubu katika mijadala ya bunge. Nilitegemea wasomi hao wangekuwa wa kwanza kukosoa mwenendo mzima wa bunge unavyoendeshwa.

Tumeshuhudia Spika anakiuka taratibu Na Sheria za bunge toka upangaji wa kamati za bunge Kwa kuzipanga Kwa upendeleo Na matokeo yake tumeyaona wabunge wamekuwa wala rushwa.Kuna kamati mbili ambazo ni lazima ziongozwe Na Upinzani lakini Spika amekuwa ana kiuka taratibu .

Tumeshuhudia bunge Kwa kushirikiana Na Serikali zinakandamiza Uhuru wa watanzania kupata habari Kwa kuzuia kutushwa Kwa matangazo ya bunge moja Kwa moja ili wananchi wawaone wawakilishi wao wakichangia kile walichowatuma.Tumeshuhudia serikali ikibadili matumizi ya fedha bila kupata idhini ya bunge kama Sheria inavyotaka hata kama ni Kwa manufaa ya wananchi lakini Sheria in lazima Na bunge limekaa kimya.

Na mwisho bunge lenyewe limehamisha fedha bila wabunge kujulishwa Na kupitisha.Nilitegemea hao wasomi Dr.Bana hayo yote angeyasemea kuliko kuulaumu upinzani Kwa kukaa kimya .Upinzani umeamua kukaa kimya kwani Sheria Na taratibu zinakiukwa wasomi wetu mko kimya wao upinzani kukaa kimya ndio kina Dr.Bana mnajitokeza kulaumu mbona hamjitokezi kuhoja uvunjwajiwa katiba Na Sheria unaofanywa Na Serikali Na Bunge hamhusemei?

Mbona wananchi kukosa matangazo ya bunge Live mmenyamaza? Wasomi wetu acheni unafiki kwenye mambo ya manufaa Kwa Taifa letu.
 
Jamani bana, hajapewa cheo chochote na bROO magu mpaka leo hata ukuu wa wilaya jamani?
 
Nimeshangazwa Na hao wanaojiita Wasomi Kwa kuilaumu Kambi ya Upinzani Bungeni kuwa Bubu katika mijadala ya bunge.Nilitegemea wasomi hao wangekuwa wa kwanza kukosoa mwenendo mzima wa bunge unavyoendeshwa.Tumeshuhudia Spika anakiuka taratibu Na Sheria za bunge toka upangaji wa kamati za bunge Kwa kuzipanga Kwa upendeleo Na matokeo yake tumeyaona wabunge wamekuwa wala rushwa.Kuna kamati mbili ambazo ni lazima ziongozwe Na Upinzani lakini Spika amekuwa ana kiuka taratibu .Tumeshuhudia bunge Kwa kushirikiana Na Serikali zinakandamiza Uhuru wa watanzania kupata habari Kwa kuzuia kutushwa Kwa matangazo ya bunge moja Kwa moja ili wananchi wawaone wawakilishi wao wakichangia kile walichowatuma.Tumeshuhudia serikali ikibadili matumizi ya fedha bila kupata idhini ya bunge kama Sheria inavyotaka hata kama ni Kwa manufaa ya wananchi lakini Sheria in lazima Na bunge limekaa kimya.Na mwisho bunge lenyewe limehamisha fedha bila wabunge kujulishwa Na kupitisha.Nilitegemea hao wasomi Dr.Bana hayo yote angeyasemea kuliko kuulaumu upinzani Kwa kukaa kimya .Upinzani umeamua kukaa kimya kwani Sheria Na taratibu zinakiukwa wasomi wetu mko kimya wao upinzani kukaa kimya ndio kina Dr.Bana mnajitokeza kulaumu mbona hamjitokezi kuhoja uvunjwajiwa katiba Na Sheria unaofanywa Na Serikali Na Bunge hamhusemei?Mbona wananchi kukosa matangazo ya bunge Live mmenyamaza? Wasomi wetu acheni unafiki kwenye mambo ya manufaa Kwa Taifa letu.
Tanzania kuna upinzani, au kuna wapiga dili tu!
 
Kwani kazi ya upinzani bungeni ni nini? Dr. Bana hana jukwaa bungeni, ambapo kimsingi ndipo mustakabali wa taifa hujadiliwa kwa kuwa bunge ni mhimili unaojitegemea. Hiyo ni kazi ya upinzani mkuu. Dr. Hana atabaki kuwa mchambuzi na mshauri tu. Tutofautishe kazi za wasomi wetu na wawakilishi wetu bungeni
 
Kama Dr.Bana ni mchambuzi mbona hajayachambua hayo yaliyoelezwa hapo Juu? Kama hakuna upinzani basi hata hao wanaojiita wasomi hakuna kitu in kuganga njaa
 
HAO KINA DK. BANA NI MA KADA HEWA WA CCM! WASIKUANGAISHE! LAKINI BORA UMEAWAMAIA ILI WAJUE TUNAWAONA WAPUUZI.! WENZIE KAMA KINA BAREGU WANAFANYA SIASA PRACTICAL YEYE ZA MANENO TU! KADA HEWA HUYO!
 
Mkuu wasomi wapo na wanapingana katika itikadi na falsafa mbalimbali. Kazi ya yao ni kuchambua tu. Hoji wasomi kadhaa uone walivyo na hoja tofauti. Kimsingi unapotaka akemee serikali ya ccm sio sawa. Hiyo ni kazi ya upinzani bungeni. Kwani ulimuuliza Dr Bana akakuambia hakuna makosa? Tatizo unataka apande jukwaani. Yeye ni mchambuzi tu na sio lazima kila kitu aseme hata kama hajaulizwa. Kamhoji, huenda anapinga. Na kama hapingi msikilize hoja zake ndio umhukumu. Usilewe na mapenzi yako kwa upande fulani ukataka wasomi wetu wapande majukwaani.
 
Dr bana hajawahi kuikosoa serikali ya ccm yy tu ktk wasomi wa nchi hii ndo huisifia ccm hata kwa mambo ya kipuuzi...huwa anauchambuzi wa kishabiki mno...magu muonee huruma huyu mzee ni kati ya wale 43 waliosalia wakikusubiri uwateuwe...alafu kibaya wilaya zenyewe chache kuliko mahitaji ya vijana wa lumumba
 
Back
Top Bottom