Wasomi kubwagwa kwenye chaguzi ni hasira za wananchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi kubwagwa kwenye chaguzi ni hasira za wananchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Netanyahu, Feb 26, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika chaguzi nyingi kuanzia za ujumbe wa nyumba kumi,serikali za mitaa ubunge na Uraisi wasomi waliobobea sana wamekuwa wakibwagwa na wasiosoma sana.

  Nakumbuka Raisi Nyerere aliwahi kuulizwa miaka ya nyuma sababu ya yeye kuwa na mawaziri wengi ambao sio wasomi na waelewa sana akajibu kuwa “tatizo sielewi kawaulize wananchi ni kwa nini msomi sana akigombea na mtu asiyesoma sana na asiye mwelewa sana wananchi wanampa kura yule mwenye elimu ya chini na uelewa mdogo”..Nyerere akasema wale anaoletewa na wananchi kupitia kura ndio hao anaowateua kuwapa uwaziri yaliyobaki watajaza wananchi waliowachagua.

  Hivi nauliza wananchi kukataa kuwachagua wasomi sana wengi kwenye chaguzi mbalimbali kwa wingi ni hasira ya wananchi kwa kuwa wasomi wakubwa hawatimizi matakwa yao au ni kwa sababu wanaona wasomi sana hawaitumii elimu yao kwa faida ya wote bali kwa faida zao binafsi zaidi? Nini tatizo hasa hadi wananchi wasiwaone wasomi sana kama ni wenzao na wawape ushindi wa kishindo dhidi ya wasomi kidogo au wasiosoma?
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni msomi,lakini nawaunga wananchi kutowachagua wasomi.Wasomi walio wengi ni wasomi uchwara na mamluki.Katika usomi wao wameshindwa kabisa kuwasaidia wananchi wa kawaida katika shida zao.Badala yake wanachumia matumbo na kutekeleza maslahi ya mabwana zao wa nchi za magharibi.Niwe muwazi,msomi halisi hawezi kujiunga na siasa,kwa vile msomi believes in hard facts and provable by scientific theories.Sasa siasa is nothing but carefully ochestrated assortment of ideas, which cannot be proved and worked upon,infact lies.Lakini tunacho ona sasa ni wasomi wengi kujiingiza kwenye siasa kuganga njaa.Wamekosa msimamo kabisa,ni watu walioharibikiwa akili zao kabisa!Wanasiasa wanapiga wanachi chenga ,wasomi nao wanapiga wananchi chenga,sasa ni nani atawasaidia?Namshangaa sana msomi mwenye zaidi ya degree moja anayeingia kwenye siasa,hawa ndio walio na vyeti 'fake.'

   
 3. N

  NTIRU Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wananchi kukataa kuwachagua wasomi sana kunasababishwa na pande zote mbili, wananchi wenyewe na wasomi. Enzi za Mwalimu, wananchi wengi hawakuwa na elimu na/au uelewa wa uwakilishi Bungeni. Na wasomi wachache waliokuwapo walikuwa na tabia ya kujiona kuwa watu wa daraja la juu katika jamii na hivyo kutokuwa karibu sana na wananchi. Hivyo wananchi walimwona yule asiye msomi sana kuwa ndiye mwenzao anayepaswa kuwawakilisha. Kwa miaka ya hivi karibuni Wasomi wengi walikimbilia CCM ili wapate nafasi ya kujikusanyia utajiri wa haraka haraka. Walipochaguliwa kwenda Bungeni wakawa "rubber stamp" ya Sheria za ukandamizaji na Sheria za Rushwa kama TAKRIMA. Hali hii ikawakatisha tamaa wananchi na wakaamua kumchagua yeyote bila kujali elimu yake. Fikiria Maprofesa na Madaktari waliojaa Bungeni na wanaoshikiria nyadhifa mbalimbali (Mawaziri, Wakuu wa Mikoa/Wilaya n.k.) lakini ni hao hao wamesababisha wananchi wa vijijini kuwa maskini wa kutupwa. Sasa ni wakati mwafaka kwa Wasomi kuanza kutumia usomi wao kwa manufaa wananchi bila kutanguliza manufaa yao.
  Sijui huko CCM kuna nini? Msomi akiingia huko anapoteza ueledi wake na kuwa kama vile hakwenda shule!! Yeye ni kuunga mkono hata kile asichokiamini eti kulinda maslahi ya Chama. Kwake yeye Rushwa ....sawa; Ufisadi ....sawa; Dhuluma ....sawa. Wasomi jisahihisheni na mtumie usomi wenu kwa ujasiri wa kutoburuzwa na Chama (CCM). Chama hicho kimeoza.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wananchi ambao tunaonekana ni wajinga kwa kuwachagua viongozi ambao si wasomi sana, tunauelewa zaidi kuliko tunavyoonekana. Kwa sababu tuna mifano, tunafahamu nini cha kufanya. Kama chaguzi zingekuwa zinafanyika kwa haki na kungekuwa hakuna kuhonga "wasomi" wasingekuwa madarakani.
  Angalia mfano mzuri kati ya waziri wa mambo wa ndani msomi Masha, na waziri wa ndani asiye msomi Mrema, nani better. Are we safe under Masha than we were during Mrema?
  Kingine ni kuwa wasio wasomi kama ni wezi si wezi sana, na walio wasomi kama ni wezi ni wezi kwelikweli. Kuna mifano mingi tu...
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kuongezea tu Mkuu Bongolander, ni kwamba wanasiasa wasio wasomi wanakuwa na nia inayokaribia ya kweli (kama sio ya kweli) katika kutatua matatizo ya wananchi kuliko wale ambao wanajisikia kuwa wasomi wakubwa. Walio wasomi mara nyingi wanakuwa wameingia kwenye siasa kwa nia ya kupata nafuu fulani fulani, ama kwa kuwa wameona opportunity fulani za kujilimbikizia mali, au hata wameombwa kufanya hivyo na wakuu wa nchi n.k. Hivyo sababu zao si za kutatua matatizo ya wananchi hasa, ila kutimiza mahitaji yao na ya wale waliowaomba waingie kwenye ulingo wa siasa. Hivyo huwa hawana njia za utatuzi wa matatizo ya wananchi kama wanavyotegemewa kuwa.

  Wakuu wa JF, Mwanasiasa asie msomi, anakuwa muoga sana kutotimiza wajibu kutokana na kuwa na nafasi chache sana ambazo zinaweza kumfanya kupata heshima, nafuu ya maisha n.k. Hivyo huwa watiifu kwa waajiri wao (wananchi) na viapo vyao kuliko wasomi. Vile vile wanasiasa wasio wasomi huwa hawana mbinu nyingi za kuibia taifa kama wale walio wasomi wa kubobea.

  Wanasiasa wasomi wakubwa hujua jinsi ya kuiba, na kuficha, kitu ambacho si rahisi kufanywa na wale wasio wasomi sana. Wanasiasa hawa huwa hawana uoga wa kuthubutu kwa kuwa wanaweza kupata maslahi yao sehemu nyingine yoyote endapo akichafua mazingira yake ya kisiasa. Wengi wao siasa sio kitu walichodhani wangekitegemea sana. Ila wakishaingia huko, ni wagumu sana kutoka. Hutumia njia zozote kubakia kwenye siasa (hata njia haramu).
   
 6. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Wana JF mliokuwa Tanzanet mtakumbuka vinara wa mtandao ule ambao wengi sana sasa wako serikalini, kisha mlinganishe perfomance na maneno yao kabla ya kuingia huko. Nawakumbuka wengi wakiwamo Dr. Chami, Bamwenda, Sterga, mwikalo, Masha, na wengine ongezea.

  Usaliti umeamzia kwa wasomi siyo kwa wananchi.
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wasomi wamekuwa wakijidhalilisha katika siasa na wanaingia huko kutafuta maslahi binafsi,hutamani keki ya Taifa afaidi yeye,familia yake na marafiki zake.Wasomi wana mbinu nyingi na dhalimu za uhujumu wa rasilimali za Taifa.Mifano ni mingi sana,wana JF tuwahamasishe wananchi wasiwachague wasomi kwenye nafasi za kisiasa ili wabakie kwenye vyuo na shule kufundisha.
   
 8. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Mmaroroi, sio rahisi kuwaambia wananchi wasimchague msomi kwenye cheo chochote. Tatizo linaanzia pale msomi anapoamua kuondoka na kuingia kwenye siasa. Ni wazi kuwa siasa imekuwa biashara nzuri kwa wengi, si wasomi tu, bali hata wasio wasomi. Sababu zinaweza kuwa nyingi kiasi cha kuanzisha thread ndefu tu.

  Kuwaomba wananchi wasichague wasomi, unatakiwa kuwa kama mwendawazimu hivi. Maana watakushangaa sana, na wengine wakidhani huwatakii maendeleo. Maana watu wengi wanadhani kuwa wasomi wanaweza kuwaletea maendeleo kwa kuwa wanajua zaidi. Inaweza kuwa kweli kwenye mambo mengine yote isipokuwa siasa.
   
Loading...