Wasomi hapa tuwekane sawa.

hakisoni

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
476
98
wana -jf. Sote tunajua elimu ndio ufunguo wa uelewa wa mambo mengi katika ulimwengu huu. Na alieyehitimu huitwa msomi au learned person. sasa wasomi wa kada ya uanasheria wao hujiita "my learned brother/sister" sasa hii imekaaje? wasomi wa kada nyingine ka wahandisi, madaktari, wahasibu n.k wanajiitaje? au usomi wao ni wa mashaka? kama ndivyo au sivyo je huu msemo umekaaje? " LEARNING IS WHAT REMAINED AFTER EDUCATION". Tafadhali tusaidiane tuondoe ubaguzi.
 
Haya majina ni kama mtindo (fashion) na sifa binafsi tu, mbona wengine wanajiita "Interllectuals".
 
Hivi Bongo kuna wasomi? Ebu Tajeni hata wa5 tuwajue na mambo waliyofanyia hapa tz hasa kitechnology achana na wanasiasa coz hata std 7 anaweza kuwa mwanasiasa ili mradi aweze jua piga domo.
 
Usomi una ugrade kwa majina mkuu?! Wako wasomi wakubwa waliofunzwa na maisha na ni watu mashuhuri kuliko hao wanaojiita kwa kujipa majina.Mkuu elimu ya mtu huwa na thamani kutokana na matokeo ya ayafanyayo muhusika na wala si majina.Sioni kama hili la majina linahitaji PhD kulielewa.
 
mh! hata kama ni mbwembwe kama zile za high school za HGE,HGL,PCB,PCM, KLF na expected general managers (EGM); hii yao kweli si nzuri kwani hata kama wanawasimamia wasomi wengine ktk kesi zao, nao pia wanahudumiwa na wasomi kama wengine madaktari, wahandisi n.k; tunawatambua kama lawyers na hata kama watajiita learned it is only with regard to legal issues; hata ktk hizo sheria si kwamba wame-learn zote.
 
mi naona hainahaja ya kuumiza vichwa kujadili majina wanaojipa watu, nikuwaacha tu na chamsingi mleta mada ningeona ni vizuri zaidi kama ungeuliza ni namna gani huo usomi wao umechangia katika maendeleo ya jamii ya kitz kuliko kujadili jina. Waswahili wanasema "kuku ni kuku tu jogoo jina" kwahiyo msomi ni msomi tu hatakama unajina fulani ama hauna cha msingi taifa limenufaika vipi na usomi wako? Nimtazamo wangu tu!
 
mi naona hainahaja ya kuumiza vichwa kujadili majina wanaojipa watu, nikuwaacha tu na chamsingi mleta mada ningeona ni vizuri zaidi kama ungeuliza ni namna gani huo usomi wao umechangia katika maendeleo ya jamii ya kitz kuliko kujadili jina. Waswahili wanasema "kuku ni kuku tu jogoo jina" kwahiyo msomi ni msomi tu hatakama unajina fulani ama hauna cha msingi taifa limenufaika vipi na usomi wako? Nimtazamo wangu tu!

Well said
 
Hivi Bongo kuna wasomi? Ebu Tajeni hata wa5 tuwajue na mambo waliyofanyia hapa tz hasa kitechnology achana na wanasiasa coz hata std 7 anaweza kuwa mwanasiasa ili mradi aweze jua piga domo.

Mkuu Tanzania tunawasomi sana tena waliobobea katika fani mbalimbali. Kutoonekana kwa matokeo kunaletwa na mfumo wa serikali usiokuwa na utaratibu wa kupima viwango vya ufanisi na uwajibikaji kazini. Sana sana ni maslahi binafsi na kulindana. Hali hii imekuwa ndio utamaduni wa serikali nzima na taasisi zake. Watu wamekuwa wanafiki kwa hofu ya mfumo huo. "Pull him down' imewaumiza watendaji wengi wazuri. Wengine tangu wameanza kazi hadi wanazeeka hawajaona mfumo sahihi wa utendaji hivyo wanadhani jinsi serikali inavyofanya kazi ndicho kiwango kikubwa duniani!. Watu hawa ni wabishi, jeuri, hawajali umma tena ndio wanaowekeza katika majungu na rushwa maadam ndio mfumo walioukuta basi lazima wautukuze. Kwa kuwa serikali haiwezi kusimamia idara zake, basi hata taasisi inazozi -regulate zinaingia katika mfumo huo huo. Zikifanya kwa kiwango ni kwa sababu ya malengo, juhudi na dhamira binafsi lakini si kwa jitihada zozote za serikali. Serikali haina mpango. Mfano utaona madawa na bidhaa fake zinaingia sokoni serikali inakoroma usingizini tu!.

Swali la kujiuliza, kila siku jk na wapambe wake (ni wapambe tu kwa ajili ya mfumo wake wa uteuzi na kukosa uwajibikaji) kila siku analala na kuamkia nchi zilizoendelea. Lakini ni kipi ambacho ame import kwamba sasa alienda nchi za wenzetu, labda akaona mfumo wao wa road reserve ulivyo sasa anahamishia hapa ili kuondoa bomoa bomoa ya kila siku ambayo haina tija kwa wabomolewaji wala serikali yenyewe zaidi ya kufrusrate watu na uchumi tu!. Technolojia na viwanda ili kuongeza ajira, masoko na uzalishaji nchini! Hollaaaa!, Ukusanyaji wa kodi na vipaumbele katika matumizi ya kodi za wananchi ili kupunguza utegemezi wa budget na kuspeed up maendeleo....HOLLAAAA!; Ni ziara za anasa tuuuu! Hana namna yoyote ya kusema kuna kitu alijifunza kizuri na kusimamia utekelezaji wake hapa nyumbani.

Lakini kuna idara na wasomi ambao kama wangekuwa chini ya mfumo sahihi, hii nchi ingekuwa mbali sana. Naisifu sana ndidara ya Umwagiliaji kwa sababu ni wasomi wengi na wanajua wanachokifanya japo utaona kabisa mara kadhaa wanawekewa vigingi njiani na mfumo dhaifu. Mfumo ambao mihimili yote inatawaliwa na siasa zenye unafiki na ufisadi; Siasa zisizokuwa na nia ya kuleta maendeleo zaidi ya kuwahadaa watu!. Hata ungekuwa ni wewe mkuu, ungeona taabu wanayoipata wasomi wenye nia safi katika nchi hii.

Badilisheni serikali badala ya ccm iwekwe CDM, halafu mtaona ni nmna gani mlichelewesha maendeleo yenu wenyewe. CDM hakuna ubabaishaji. Asiyewajibika lazima awajibishwe. Asiyefanya kazi yake kwa kiwango kinachotakiwa na muda muafaka hafai. Mwizi wa mali za umma arudishe tuzitumie kwa manufaa ya umma. Hakuna uzembe kama wa ccm. Mtu analipwa kwa kazi aifanyayo na ufanisi wa kila mtu unapimwa.
 
ndugu, hiyo ni jinsi ambayo wanasheria wanaadress each other,either lerned brother/sister, counsel au advocate...ni kama vile ukikutana na mwalimu ukamuadress hvyo au dkt au eng. na sio kwamba wanajiona wao ndio wao,....hata huko nnje, ndivyo wanasheria wanavyoitwa.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom