Wasomali 82 wakamatwa Morogoro wakielekea Dar kutafuta Maisha.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomali 82 wakamatwa Morogoro wakielekea Dar kutafuta Maisha..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwenda_Pole, Apr 28, 2011.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  NA DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
  WATU wapatao 82 raia wa Somalia wamekamatwa jana mchana kwenye msitu wa moja ya vijiji vya Wilaya ya Gairo mkoani hapa wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam kutafuta maisha.

  Akizungumza na mtandao huu kwenye kituo kikuu cha polisi mkoani hapa, askari mmoja wa kikosi cha kutuliza ghasia wilayani Gairo maarufu kwa jina la 'voda fasta'alisema Wasomali hao walikamatwa baada ya polisi kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

  "Tumepokea taarifa kutoka kwa raia wema wakitujuza kuwa kuna kundi la wasomali wanakata mbuga katika misitu ya Vijiji vya Gairo hivyo baada ya kuwafuatilia tumewakamata na kuwaleta hapa mkoani," alisema afande huyo aliyekataa kutaja jina lake kwa kuwa sio msemaji mkuu wa jeshi la polisi.

  Mwandishi wetu aliwashuhudia Wasomali hao wakishushwa kwenye roli huku wakiwa na matope hali inayoonesha kuwa huenda wana muda mrefu hawajaoga kutokana na kutembea kwa muda mrefu.

  Source: Globalpublishers

  wasomali.JPG
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Jamani waachieni manake kuna watu watajasema wamekamatwa kwa sababu ya dini zao 'JK at work'
   
 3. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  waachieni hao ndugu zetu, wasilete ujinga wa udini tu, kwao kuna vita na wafanyabiashara wazuri hata wakibaki wataongeza nguvu kazi tu, japo kama wana msimamo mkali kidini ni kilema kikubwa.
   
Loading...