Wasira: Siachii ubunge kwa vijana ni wavuta bangi..!!!

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,702
Huyu Wasira kadata, yaani, sababu anayosema kuwa hataki kuachia madaraka kwa vijana ati ni vijana wanakula bangi! Nchi kibao wanakula mjani; Holland kule wanakula mjani, Jamaica na sehemu kibao. Sisemi hivi natetea wanala mjani, la hasha! Sababu aliyotoa ni mufilisi kwa mtu mzoefu kama Tyson ni fedheha sana na matusi kwa vijana; ni aibu kubwa kwa mtu mzima kama Wasira.

Sababu yake ya kutoachia madaraka ni selfishness yake. Nilimsikia akisema alianza kuwa mbunge tangu mwaka 1970 na anajisifia kwa masifa kede kede; miaka zaidi ya 30 yuko bungeni ati haachii kiti cha ubunge kisa vijana wanavuta majibangi. Mzee kama Wasira waliokaa bungeni zaidi ya 30 sitategemei awe na kauli kama hizi; kafanya nini Tyson bana mpaka aseme kuwa haachii madaraka kisa vijana wanakula mjani?

Hii kwa Wasira naiita ni kutokojiamini, hofu, ubinafsi; hana lolote anaweza kufanya zaidi ya kukaa bungeni. Yaani, jitu kama Wasira anaona hamna watu zaidi yake wanaweza kuwakilisha watu bungeni?

Hakuna uhusiano wa umri na madaraka aachie madaraka; kauli ya hofu hizo. Kudadadeki naenda chukua fomu; kuniloga hamuwezi, niko fiti.

1701849970035.jpeg
 
sio hofu tu huenda ikawa na yeye mwenyewe anavuta bangi ndo maana anajua kuwa wavuta bangi wakoje.by the way kwani kuvuta bangi kuna tatizo gani?
 
Kwa hiyo yeye alivyopata akiwa kijana alikuwa anakula bangi? na ana watoto amabao ni vijana je nao wanakula bangi? na kama ni ndio je ameshindwa kuwastopisha kwa hivyo hafai kuwa kiongozi.
 
Yaelekea Wassira anataka watu wamchambue maisha yake! Alafu adai ni udaku.
 
Huyu wasira kadata yaani sababu anayosema kuwa hataki kuachia madaraka kwa vijana ati ni vijana wanakula bangi…..!!!! nchi kibao wanakula mjani,Holland kule wanakula mjani,Jamaica na sehemu kibao.Sisemi hivi natetea wanala mjani ,la hasha! Sababu alioitoa ni mufilisi kwa mtu mzoefu kama Tyson ni fedheha sana na matusi kwa vijana…ni aibu kubwa kwa mtu mzima kama Wasira

….sababu yake ya kutoachia madaraka ni selfshiness yake....nilimsikia akisema alianza kuwa mbunge tangu mwaka 1970 anajisifia kwa masifa kede kede…. miaka zaidi ya 30 yuko bunge ati haachii kiti cha ubunge kisa vijana wanavuta majibangi.Mzee kama wasira waliokaa bungeni zaidi ya 30 sitetegemei awe na kauli kama hizi..….kafanya nini Tyson bana mpaka asema kuwa haachii madaraka kisa vijana wanakula mjani…...

Hii kwa wasira naiita ni kutokojiamini, hofu,ubinafsi hana lolote anaweza fanya zaidi ya kukaa bungeni…..yaani jitu kama wasira anaona hamna watu zaidi yake wanaweza kuwakilisha watu bungeni?
Hakuna uhusiano wa umri na madaraka aachie madaraka …….kauli ya hofu hizo….. kudadadeki naenda chukua fomu….kuniloga hamuwezi niko fiti….

Inabidi aeleweshwe kuwa kuna watu wanavuta bangi na bado wana akili nzuri tu kuliko watu wasiovuta bangi. Tatizo la jimbo lake sio vijana kuvuta bangi au la ila ni kutokuwa na watu wasiovuta ambao hawako committed na maendeleo ya sehemu hiyo mawazo yao ni hela tu.

Kama amekuwa mbunge toka miaka ya 1970 na hajafanya lolote jimboni katika miaka 40 iliyopita anaweza kufanya nini katika kipindi kifupi cha muda uliobaki???? Sidhani kama anaweza kuwa na mawazo mapya i dont think.
 
Wasira anazidi kuzeeka vibaya, mimi nafikiri kumrudisha bungeni hii 2010 ni kutomtendea haki hata kidogo, naona viashiria vya kupungukiwa akili, utashi na adabu, kweli amekua na matusiu kwakila anaepinga wazo lake, anawafanya waTanzania kua watoto wake, Wasira mara kadhaa amekua akinukuliwa akiwatusi wainzani wake kisiasa, kumbukeni kaulizake kule BUNGENI. Dawa yake ni kumng'oa.
 
Nikiyakumbuka maisha aliyokuwa nayo miaka minne iliyopita ana haki kung'ang'ania ubunge hadi mauti yamkute hapo. Siasa inalipa jamani na hasa unapoukwaa uwaziri.
 
Nikiyakumbuka maisha aliyokuwa nayo miaka minne iliyopita ana haki kung'ang'ania ubunge hadi mauti yamkute hapo. Siasa inalipa jamani na hasa unapoukwaa uwaziri.
kwa macho yangu niliwahi kugongana na Wasira mahala fulani analia baada yakuhenyeshwa na watumishi wa umma juu ya huduma ambayo ni haki yakeila kila mtu anamuogopa kumuhudumia kwasababu ni mpinzani, jitu lenye mwilimkubwa vilelinalia, kweli nakuelewa kwanini hataki kung'oka kwenye madaraka.
 
Wavuta bangi bwana, utawafahamu tu.

Jah People Never Die.
If Die never Decay.
If Decay Never Smell.
If Smell, Smells perfume................................... RAST-A-FARIAN.
 
Bila ya Katiba kubadilishwa na kuweka limit ya vipindi vya kugombea ubunge kama ilivyo limit ya kugombea urais, basi ni hakika hakuna ambaye ameshika ubunge ataachia nafasi yake kabla hajafa. Kila Mmoja atakapopata ubunge atajihesabia amefika kwa kuwa kugombea tena ili upite ni kazi rahisi sana. hiyo itaendelea hivyo hadi afe ndipo wengine watapata nafasi ya kuongoza.

I think awamu mbili (kama urais ) iwe ni maximum ya mtu kuwa mbunge then aachie ngazi na asigombee tena, hiyo italeta changamoto. (BUT SHERIA IWEKWE KUTHIBITI KUJILIMBIKIZIA MALI KTK KIPINDI KIFUPI BEFORE HAWAJATOKA)
 
Jamani msaada kwenye tuta.......huyu Wasira ndiye yule alikuwa NCCR? kuna wakati NCCR waliandamana pale kwenda kwenye ofisi za UN Dar yeye na akina Marando wakamwagiwa maji ya upupu, hebu nisaidieni nimjue zaidi.
 
Kulalamika kwamba mtu fulani mzee aachie ubunge sii uungwana na zaidi ni ubaguzi kwa huyu

senior citizen , ubaguzi ambao ni mbaya sana! Ni lazima tutambue ya kuwa uzee ni part and

parcel ya maisha mwanadamu ,na sisi siku moja tutapitia hiyo njia kama Mungu atapenda. Kama

kuna kijana anayeona Wasira hafai kutokana na umri wake, basi achukue nafasi hiyo kwenda

kupambana naye huko kwenye jimbo la huyo muhusika.
 
Yo Yo heshima mbele kamanda..naona leo umeibukia pande hizi..

Sasa mkuu ningeomba utuwekee source au kama inawezekana tuwekee habari kamili ili tuweze kuijadili kinaga ubaga hapa.

Wasalaam

MJ
 
Anajiita Tyson wa kuvuta bangi, yeye na makweta wakiachwa waendelee watafia ndani ya bunge, huwezi amini ndie yule wasira wa NCCR aliye kuwa anaongea mpaka anakuwa mweupe tofauti na rangi yake ya sasa.
 
Politically bankrupt!!! Kwani kuvuta bangi kuna uhusiano gani na ubunge au busara kwa jumla? Hajui kuwa hata marais wa marekani akina Clinton, Bush na Obama walishavuta bangi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom