Wasira na busara iliyochelewa

Buldoza

JF-Expert Member
May 2, 2013
2,306
980
Kwa aliyemsikiliza Mh. Wasira juzi na jana atakubaliana nami kwamba kuna mabadiliko makubwa sana kati ya Wasira huyu wa sasa na Wasira yule wa Bunge Maalum la Katiba (BMK). Washabiki wa CCM pamoja na wapinzani ambao walipata kumwita kwa majina ya kejeli juzi na jana wameungana pamoja kuunga mkono busara za Mheshimiwa huyu. Wasira, jana alizungumza toka moyoni kabisa kwamba amefurahishwa sana na busara iliyotumika ya kufikia maamuzi kwa njia ya MARIDHIANO.

Swali nililojiuliza, hivi Wasira neno Maridhiano ndio amelijua jana katika umri wa maisha yake hapa duniani? Si huyu huyu Wasira na wenzie waliokuwa wakipinga Maridhiano kwenye jambo muhimu kabisa la kuwapatia Watanzania katiba bora? (Ikumbukwe kwa maneno ya Lukuvi kwamba katiba itakayopatikana bila ya UKAWA kushiriki haitakuwa na afya).

Kwanini Wasira hakuona busara ya kufanya maridhiano na UKAWA kipindi hicho ili kutupatia katiba yenye afya?
Ni nini kimembadilisha Wasira ghafla na kuona umuhimu wa maridhiano leo ambao hakuuona kwenye Bunge la Katiba?

Kweli Ukistaajabu ya ESROW utayaona ya SIMBA TRUST.
 
Kwa mara yangu ya kwanzanimemuona Wasira akikubali wabunge wa Ccm ni vichwa maji. Ccm wanasema tumeridhiana na wenzetu wa upinzani ripoti iwe kama itakavyo somwa na PAC. ubabe mfukoni.
 
wameshikwa pabaya. Prof. Mwandosya alisema makosa yamefanyika tukubali.
 
Mabibi na Mabwana, nidhahili wazi ccm inajisabmiti kwa Ukawa.

Tutarajie mengine mengi ya ajabu. Kunakitu wanaanza kukiona huko mbeleni.

Adabu, za wassira, Lukuvi na hata U-turn ya Mwigulu sio bure, bado Nape tu.
 
Hana lolote yule! walisha soma alama za nyakati na kuona kuwa allogance isingefanya kazi katika jambo lile. Huoni kuwa imesaidia mambo mengi watu hawajaendelea kuhoji mgao wa singasinga uliwafikia akina nani na hiyo Simba Trust ni ya nani?
 
wameshikwa pabaya. Prof. Mwandosya alisema makosa yamefanyika tukubali.
mwandosya ni proffesional professor hakutaka kusha taaluma yake .si kama akina mwakembe akina tibaijuka na wengine kuogopa kusema ukweli.huwezi ukaweka mahesa ya receivables kwenye assets zako kmahazihusiani na organization yako.sasa escrow iluwa item ya receivables kwenye akaunti ya benki kuu.sasa mpka jana pinda hajui kmapesa za umma.upuuzi mtupu
 
Kwa aliyemsikiliza Mh. Wasira juzi na jana atakubaliana nami kwamba kuna mabadiliko makubwa sana kati ya Wasira huyu wa sasa na Wasira yule wa Bunge Maalum la Katiba (BMK). Washabiki wa CCM pamoja na wapinzani ambao walipata kumwita kwa majina ya kejeli juzi na jana wameungana pamoja kuunga mkono busara za Mheshimiwa huyu. Wasira, jana alizungumza toka moyoni kabisa kwamba amefurahishwa sana na busara iliyotumika ya kufikia maamuzi kwa njia ya MARIDHIANO.

Swali nililojiuliza, hivi Wasira neno Maridhiano ndio amelijua jana katika umri wa maisha yake hapa duniani? Si huyu huyu Wasira na wenzie waliokuwa wakipinga Maridhiano kwenye jambo muhimu kabisa la kuwapatia Watanzania katiba bora? (Ikumbukwe kwa maneno ya Lukuvi kwamba katiba itakayopatikana bila ya UKAWA kushiriki haitakuwa na afya).

Kwanini Wasira hakuona busara ya kufanya maridhiano na UKAWA kipindi hicho ili kutupatia katiba yenye afya?
Ni nini kimembadilisha Wasira ghafla na kuona umuhimu wa maridhiano leo ambao hakuuona kwenye Bunge la Katiba?

Kweli Ukistaajabu ya ESROW utayaona ya SIMBA TRUST.

Atataka urais
 
Back
Top Bottom