Buldoza
JF-Expert Member
- May 2, 2013
- 2,306
- 980
Kwa aliyemsikiliza Mh. Wasira juzi na jana atakubaliana nami kwamba kuna mabadiliko makubwa sana kati ya Wasira huyu wa sasa na Wasira yule wa Bunge Maalum la Katiba (BMK). Washabiki wa CCM pamoja na wapinzani ambao walipata kumwita kwa majina ya kejeli juzi na jana wameungana pamoja kuunga mkono busara za Mheshimiwa huyu. Wasira, jana alizungumza toka moyoni kabisa kwamba amefurahishwa sana na busara iliyotumika ya kufikia maamuzi kwa njia ya MARIDHIANO.
Swali nililojiuliza, hivi Wasira neno Maridhiano ndio amelijua jana katika umri wa maisha yake hapa duniani? Si huyu huyu Wasira na wenzie waliokuwa wakipinga Maridhiano kwenye jambo muhimu kabisa la kuwapatia Watanzania katiba bora? (Ikumbukwe kwa maneno ya Lukuvi kwamba katiba itakayopatikana bila ya UKAWA kushiriki haitakuwa na afya).
Kwanini Wasira hakuona busara ya kufanya maridhiano na UKAWA kipindi hicho ili kutupatia katiba yenye afya?
Ni nini kimembadilisha Wasira ghafla na kuona umuhimu wa maridhiano leo ambao hakuuona kwenye Bunge la Katiba?
Kweli Ukistaajabu ya ESROW utayaona ya SIMBA TRUST.