GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,385
- 108,453
Sinema ilianzia kwa Kenya kuzuia Magari ya mizigo ya Tanzania kuingia Kwao kwenda kuuza Mahindi na Tanzania nayo ikajibu mapigo kwa kuwapandishia ' tozo ' bidhaa zao ngoma ikawa draw ( Waswahili wanasema sare )
Sinema ya pili ikaendelea tena ambapo kwa sasa kuna taarifa za chini chini kwamba Watanzania wanaoishi na kufanya Shughuli zao nchini Kenya wanapata wakati mgumu kidogo ( japo Ubalozi wetu huko unajifanya kama vile haujui kitu ) ila kuna ' jambo ' linaendelea huko nawaombeni tu fuatilieni kimya kimya mtalijua. Mara tena na huku Tanzania kupitia pale mpakani Namanga Wafanyabiashara wa Kenya nao wamekuwa wakipigwa bonge la ' pini ' kuingia bidhaa zao ' Bongo ' na hali haipo sawa.
Sinema ya tatu na ya mwisho jana tulishuhudia Mamlaka ya Tanzania ikiteketeza kwa ' moto ' Vifaranga vya Raia wa Kenya ' Mwanamama ' mmoja hali ambayo kiukweli imepokelewa kwa hisia kali sana na Wakenya wengi. Na ni leo hii hii huko nchini Kenya katika mpaka wao na Tanzania kwa upande wa Mkoa wa Mara Ng'ombe takribani 4,000 kutoka nchini Tanzania zimekutwa zimeingia katika ardhi ya Kenya kinyume cha Sheria na hivi ninavyoandika huu ' uzi ' kuna taarifa za chini chini kutokea huko Kenya zinasema kwamba huenda hao Ng'ombe nao wakachomwa moto au wakauwawa ' Kikatili ' sana ili kulipiza ' Kisasi ' cha tukio la wale Vifaranga.
Kila siku mnatuhimiza Watanzania tuwe Wazalendo hivyo basi Mimi GENTAMYCINE nawaomba Mawaziri wa Mambo za Nje wa Tanzania Balozi Mzee Mahiga na yule wa Kenya Mwanamama Balozi Amina ( kama sijakosea ) upesi sana wakae chini waweze kujadili haya mambo ambayo naona kama hayatotafutiwa ' ufumbuzi ' haraka kuna hatari ya Kenya na Tanzania kuingia ' Vitani ' au kuwa katika ' Uhasama ' mkubwa mno ambao unaweza ukaathiri hata huu ' Utengamano ' wetu wa Kikanda na wa Kijumuiya.
Tusidanganyane na kufichana hapa ukweli ni kwamba hali ya Kidiplomasia kwa sasa kati ya Tanzania na Kenya siyo nzuri na kuna wanaosema kwamba Kenya wamekuwa na ' bifu ' zaidi na Tanzania hasa baada ya kukosa lile ' dili ' la Bomba la Mafuta lakini pia inasemekana Tanzania nayo imekuwa na ' bifu ' na Kenya kupitia Raila Odinga ambaye inasemekana ana ' Urafiki ' na Mtanzania mmoja ( japo Mimi GENTAMYCINE bado sijamjua ni nani ) na pia kwa Kenya kuwa na ukaribu wa ' ajabu ' na Watu ambao Kisiasa wanaonekana kuwa na ' uadui ' na washika dola wa sasa wa Tanzania.
Naomba niishie tu hapa tafadhali ila uzuri ni kwamba nimeshatahadharisha mapema hivyo Kazi Kwenu Wahusika.
Nawasilisha.