Wasipokaa chini na kumaliza tofauti zao, naiona Vita kati ya Nairobi na Dodoma inakaribia

Sinema ilianzia kwa Kenya kuzuia Magari ya mizigo ya Tanzania kuingia Kwao kwenda kuuza Mahindi na Tanzania nayo ikajibu mapigo kwa kuwapandishia ' tozo ' bidhaa zao ngoma ikawa draw ( Waswahili wanasema sare )

Sinema ya pili ikaendelea tena ambapo kwa sasa kuna taarifa za chini chini kwamba Watanzania wanaoishi na kufanya Shughuli zao nchini Kenya wanapata wakati mgumu kidogo ( japo Ubalozi wetu huko unajifanya kama vile haujui kitu ) ila kuna ' jambo ' linaendelea huko nawaombeni tu fuatilieni kimya kimya mtalijua. Mara tena na huku Tanzania kupitia pale mpakani Namanga Wafanyabiashara wa Kenya nao wamekuwa wakipigwa bonge la ' pini ' kuingia bidhaa zao ' Bongo ' na hali haipo sawa.

Sinema ya tatu na ya mwisho jana tulishuhudia Mamlaka ya Tanzania ikiteketeza kwa ' moto ' Vifaranga vya Raia wa Kenya ' Mwanamama ' mmoja hali ambayo kiukweli imepokelewa kwa hisia kali sana na Wakenya wengi. Na ni leo hii hii huko nchini Kenya katika mpaka wao na Tanzania kwa upande wa Mkoa wa Mara Ng'ombe takribani 4,000 kutoka nchini Tanzania zimekutwa zimeingia katika ardhi ya Kenya kinyume cha Sheria na hivi ninavyoandika huu ' uzi ' kuna taarifa za chini chini kutokea huko Kenya zinasema kwamba huenda hao Ng'ombe nao wakachomwa moto au wakauwawa ' Kikatili ' sana ili kulipiza ' Kisasi ' cha tukio la wale Vifaranga.

Kila siku mnatuhimiza Watanzania tuwe Wazalendo hivyo basi Mimi GENTAMYCINE nawaomba Mawaziri wa Mambo za Nje wa Tanzania Balozi Mzee Mahiga na yule wa Kenya Mwanamama Balozi Amina ( kama sijakosea ) upesi sana wakae chini waweze kujadili haya mambo ambayo naona kama hayatotafutiwa ' ufumbuzi ' haraka kuna hatari ya Kenya na Tanzania kuingia ' Vitani ' au kuwa katika ' Uhasama ' mkubwa mno ambao unaweza ukaathiri hata huu ' Utengamano ' wetu wa Kikanda na wa Kijumuiya.

Tusidanganyane na kufichana hapa ukweli ni kwamba hali ya Kidiplomasia kwa sasa kati ya Tanzania na Kenya siyo nzuri na kuna wanaosema kwamba Kenya wamekuwa na ' bifu ' zaidi na Tanzania hasa baada ya kukosa lile ' dili ' la Bomba la Mafuta lakini pia inasemekana Tanzania nayo imekuwa na ' bifu ' na Kenya kupitia Raila Odinga ambaye inasemekana ana ' Urafiki ' na Mtanzania mmoja ( japo Mimi GENTAMYCINE bado sijamjua ni nani ) na pia kwa Kenya kuwa na ukaribu wa ' ajabu ' na Watu ambao Kisiasa wanaonekana kuwa na ' uadui ' na washika dola wa sasa wa Tanzania.

Naomba niishie tu hapa tafadhali ila uzuri ni kwamba nimeshatahadharisha mapema hivyo Kazi Kwenu Wahusika.

Nawasilisha.
 
Alichokifanya waziri wetu hakikuwa cha busara, kuweka zaidi vizuri sakata wamasai kukamata wale ng'ombe 4000 ni kulipiza kisasi kwa ng'ombe zao(wakenya) ,zilizoamriwa na mahakama ya tanzania kupigwa mnada ati kwa kisingizio kuingia nchini pasipo halali wakati ni kitu cha kawaida toka enzi na enzi.

Swala la vifaranga hili payback yake bado haijafika inakuja,tusubiri.....
Kafuata sheria na wao wafuate sheria zao hakuna shida yoyote.
 
Wakenya hatuwawez kwa lolote!

Ninachojua katika nchi za Afrika ya Mashariki hakuna nchi hata moja yenye ' ubavu ' wa Kijeshi kupambana na Tanzania iwe ni usiku au mchana au iwe ni ardhini, angani na majini au hata kwa ' Ngumi ' tu za mmoja mmoja nazo tunawapiga mapema tu. Nilibahatika kusoma na Wakenya wengi tu nchini Uganda na nilikuwa nawapiga na kuwaonea hadi Watanzania wenzangu tuliokuwa nao huko wakawa wananiambia GENTAMYCINE ' doze doze '. Labda kidogo ungeniambia Waganda ni ' ngangari ' ila siyo kwa Wakenya halafu ni ' waoga ' mno.

Nakumbuka tukiwa Shule huko huko Uganda tulikuwa na utaratibu wa kucheza mechi za mpira wa Miguu kati ya Wanafunzi wa kutoka nchi mbalimbali na bahati nzuri Shule niliyosoma hata Wasomali nao walikuwepo vile vile bila kusahau na Wasudani sasa unaambiwa kila tulipokuwa tunacheza mechi ya Tanzania na Kenya halafu Mimi GENTAMYCINE nikiwa ndiyo ' Nahodha ' wa Team ya Tanzania halafu nimelikamata dimba la kati ( Midfield ) na Kichwani nina bonge la ' Para ' nimelipaka ' Wese ' linang'aa unaambiwa Wakenya walikuwa wanaanza Kwanza kwenda kwa Mwamuzi na kumwambia awe ananiangalia sana Mimi kwakuwa nilikuwa nawatembezea ' Viatu / Rafu ' hadi wakawa wanamkumbuka Rais wao Moi wakati ule. Na hakuna mechi ambayo Kishule shule pale Tanzania tulicheza na Wakenya halafu Mimi nipo wakatufunga. Ebhana Wakenya walikuwa wananiogopa hadi raha.

Ili sasa uone kwamba Wakenya ni ' waoga ' unaambiwa baada tu ya Kugundua kuwa kati ya Watanzania tuliokuwepo katika ile Shule Mimi ndiye nilikuwa ' mkorofi ' na ' mbabe ' kila wakati wa Mtihani au Jaribio darasani kwa kuniogopa tu Wakenya walikuwa wanajibu maswali ' fasta ' halafu wananipa majibu kisha wananiambia GENTAMYCINE umeridhika nawaambia ndiyo au nikiona kuna ' Wabongo ' wenzangu Mtihani umewapiga / umewashinda mule mule ndani ya Chumba cha Mtihani natembeza ' mkwara / biti ' kwa Wakenya kwamba wawasadie na Wabongo wenzangu na walikuwa wakitekeleza amri mara moja.

Mkuu nina mengi ya kuwahusu Wakenya ila kwa leo ngoja tu niishie hapa ila narudia tena kukuambia kwamba hakuna Watu ' waoga ' kama Wakenya halafu pia ni ' Mambwigira / Washamba ' sana kwani hata ' Ujanja ' tu Sisi Watanzania ndiyo tumewafundisha. Ila Waganda kweli ' Mafia ' kwani nilikuwa napambana nao hadi sometimes ' Mwanamume ' natoka ' Nduki / Baru ' kwenda kujipanga upya.
 
Watizamaji tunaskilizia af tunapima 2020 ina umbali gani kwa mbio za bosa to boda.
 
Aliyekamatwa na vifaranga ni binti wa kitanzania havina uhusiano na Kenya. Wananchi wa nchi yoyote lazima wafuate sheria ya nchi wanazoishi kutembelea ama kusoma.

Watanzania walifukuzwa Mozambique kwa sab hawakuwa na vibali vya kuishi na nchi nyingi zinadeport watanzania kama Tanzania inavyodeport wageni.

Kufuata sheria ya nchi yako dhidi ya RAIA au bidhaa za kigeni sio chuki uhasama au kisasi.

Asante kwa masahihisho kwamba ni Binti wa Kitanzania na siyo wa Kenya ila hapo uliposema kwamba kukamatwa kwa hivyo Vifaranga havina uhusiano na Kenya ndipo kidogo sijakuelewa Mkuu. au hao Vifaranga hawakutokea nchini Kenya na wametokea Vijijini Kwenu Kyaka Nkunde na Ikupilipa Nkoba?
 
Kama hali iko hivyo ni kweli viongozi wetu wanatakiwa kutafuta suluhu kidoplomasia kuliko kuendelea na huo ubabae ambao mwisho wa siku utatuumiza wananchi wa pande zote mbili. Sisi ni majirani tunaishi kwa kutegemeana kwa mamna moja au nyingine.
 
Kutokea Kenya haimaanishi ni vya Kenya vilishanunuliwa na huyo binti kwahiyo wakenya hawawezi kukasirika kwa sab si vyao tena isitoshe wanaheshimu sheria ya nchi zingine.
 
Hivi wale nyumbu wa Serengeti, wako nchi gani sasa hivi? Kama wako Tz tujenge ukuta fasta ili wasiende tena Kenya! (kidding)

Kama hali iko hivyo ni kweli viongozi wetu wanatakiwa kutafuta suluhu kidoplomasia kuliko kuendelea na huo ubabae ambao mwisho wa siku utatuumiza wananchi wa pande zote mbili. Sisi ni majirani tunaishi kwa kutegemeana kwa mamna moja au nyingine.

Ushauri wako huu ni mzuri sana Mkuu. Heko!
 
Ninachojua katika nchi za Afrika ya Mashariki hakuna nchi hata moja yenye ' ubavu ' wa Kijeshi kupambana na Tanzania iwe ni usiku au mchana au iwe ni ardhini, angani na majini au hata kwa ' Ngumi ' tu za mmoja mmoja nazo tunawapiga mapema tu. Nilibahatika kusoma na Wakenya wengi tu nchini Uganda na nilikuwa nawapiga na kuwaonea hadi Watanzania wenzangu tuliokuwa nao huko wakawa wananiambia GENTAMYCINE ' doze doze '. Labda kidogo ungeniambia Waganda ni ' ngangari ' ila siyo kwa Wakenya halafu ni ' waoga ' mno.

Nakumbuka tukiwa Shule huko huko Uganda tulikuwa na utaratibu wa kucheza mechi za mpira wa Miguu kati ya Wanafunzi wa kutoka nchi mbalimbali na bahati nzuri Shule niliyosoma hata Wasomali nao walikuwepo vile vile bila kusahau na Wasudani sasa unaambiwa kila tulipokuwa tunacheza mechi ya Tanzania na Kenya halafu Mimi GENTAMYCINE nikiwa ndiyo ' Nahodha ' wa Team ya Tanzania halafu nimelikamata dimba la kati ( Midfield ) na Kichwani nina bonge la ' Para ' nimelipaka ' Wese ' linang'aa unaambiwa Wakenya walikuwa wanaanza Kwanza kwenda kwa Mwamuzi na kumwambia awe ananiangalia sana Mimi kwakuwa nilikuwa nawatembezea ' Viatu / Rafu ' hadi wakawa wanamkumbuka Rais wao Moi wakati ule. Na hakuna mechi ambayo Kishule shule pale Tanzania tulicheza na Wakenya halafu Mimi nipo wakatufunga. Ebhana Wakenya walikuwa wananiogopa hadi raha.

Ili sasa uone kwamba Wakenya ni ' waoga ' unaambiwa baada tu ya Kugundua kuwa kati ya Watanzania tuliokuwepo katika ile Shule Mimi ndiye nilikuwa ' mkorofi ' na ' mbabe ' kila wakati wa Mtihani au Jaribio darasani kwa kuniogopa tu Wakenya walikuwa wanajibu maswali ' fasta ' halafu wananipa majibu kisha wananiambia GENTAMYCINE umeridhika nawaambia ndiyo au nikiona kuna ' Wabongo ' wenzangu Mtihani umewapiga / umewashinda mule mule ndani ya Chumba cha Mtihani natembeza ' mkwara / biti ' kwa Wakenya kwamba wawasadie na Wabongo wenzangu na walikuwa wakitekeleza amri mara moja.

Mkuu nina mengi ya kuwahusu Wakenya ila kwa leo ngoja tu niishie hapa ila narudia tena kukuambia kwamba hakuna Watu ' waoga ' kama Wakenya halafu pia ni ' Mambwigira / Washamba ' sana kwani hata ' Ujanja ' tu Sisi Watanzania ndiyo tumewafundisha. Ila Waganda kweli ' Mafia ' kwani nilikuwa napambana nao hadi sometimes ' Mwanamume ' natoka ' Nduki / Baru ' kwenda kujipanga upya.
Hapo Wakenya walikuwa wanakuogopa ww kwa kuwa walijua na ww ni kisiki cha mpingo,lakn hawakuwa wakiliogopa Taifa (Tanzania)
Pia,ukumbuke kuwa nyote mlikuwa wanafunzi na mlikuwa ugenini
Kenyans are so smart in every aspects...,we can't stand on the same line with them 4 competition!
 
Kidiplomasia sio.sahihi serikali iliyomadarakani kuunga mkono upinzani ktk nchi jirani. Bila kisingizio chochote serikali ya Tz iombe msamaha watawala wa kenya na figisu itaisha. Msituletee ya Marehemus Nyerere na Obote dhidi ya Iddi Amini. Pls! Pls! Pls Wakenya na Watz tunahitajiana sana kuliko mnavyofikiri nyie!
 
Vingine JPM yupo sahihi.

Mf. Kwasasa serikali imeziagiza kampuni zote, Hoteli, shule na vyuo kvikuu nchini vyote. Kutowapa (kuto waajiri wageni) ajira wageni....iwapo kazi hiyo wazawa wana uwezo wa kuifanya. Ktk hili tuzalisha si chini ya ajira 10,000. Ni nufaa kubwa sn kwa rasilimali watu wetu na pato kwa Taifa letu (PAYE, Investment Multiplier, Family Care, nk).

Iwapo hakuna mtaalam huyo Tz, basi mgeni huyo aajiriwe kwa muda usio zidi miaka 3 tu (not renewable contract). Binafsi kwa hili nampongeza JPM. Mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera imejaa Wakenya sn tena wanamiliki hadi ardhi!!!

Hilo la uhasama kati ya Kenya na Tz kwa sasa ni kweli hata mm naliona lipo. Ila tukiacha ushabiki wa kisiasa hawa Wakenya huwa wanatuchukulia sisi watanzania kama mamburura hivi!! Wajingawanjinga!! Kwahiyo wapo radhi kutuibia au kuchuma mali zetu tena kwa dharau sn.

Mm huwa naamini dawa ya moto ni moto. Ngoja JPM awapitishe kwanza ktk moto, ili akiri ziwarudi. Heshima na usawa wa kufaidika utarudi tu (Mutual benefit).

Tunapoteza kidogo sn kuliko wao wanavyo tuibia.
 
Back
Top Bottom