Wasipoiba wale wapi;??kama wanaoiba wanaendelea kula kuku!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasipoiba wale wapi;??kama wanaoiba wanaendelea kula kuku!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 30, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Justice Katiti, anayekabiliwa na kesi ya kula njama, kuiba na kutakatisha fedha haramu za mamlaka hiyo, ameunganishwa katika kesi mpya yenye mashtaka 10 ya kula njama na kutapeli zaidi ya Sh. milioni 338.9, mali ya Benki ya Barclays Tanzania Limited ya jijini Dar es Salaam.Pia, Katiti ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, anatuhumiwa kuidanganya TRA kwa nia ya kufanikisha utapeli wa fedha hizo.Kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, inawakabili pia washtakiwa wengine watano, akiwamo mtumishi wa Benki hiyo, Godwin Paulla na Joseph Kaplamai Rutto, ambaye ni raia wa Kenya.Rutto ni mshtakiwa wa sita, wakati Paulla ni mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo. Wengine ni Fortunatus Muganzi, ambaye ni mshtakiwa wa pili, Robert Mbetwa wa tatu na Gideon Otulla mshtakiwa wa nne.Wote kwa pamoja, wanatuhumiwa kutenda makosa hayo dhidi ya benki hiyo na TRA, katika tarehe tofauti kati ya Septemba na Oktoba 2008, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria.Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Aloyce Katemana, Wakili Mkuu wa Serikali, Frederick Manyanda, alidai jana kuwa katika shtaka la kwanza, kati ya Septemba 29, 2008 na Oktoba 6, mwaka huo (2008), washtakiwa wote walikula njama kwa pamoja na kuitapeli benki hiyo, kinyume cha sheria.Manyanda alidai katika shtaka la pili, Septemba 29, 2008, mshtakiwa wa tano na wa sita, kwa makusudi ya kurubuni na kudanganya, walighushi fomu namba E. 17 ya Benki ya Barclays Tanzania Limited ya maombi ya kuhamisha fedha za mteja na kuonyesha kwamba, kampuni ya Tourism Promotion Services (Tanzania) Limited, iliiomba benki hiyo kuilipa kampuni ya East Africa Procurement Services Limited Sh. 338,935,337.46 kwa ajili ya kuiuzia mahema na vifaa vya hoteli.Katika shtaka la tatu, Manyanda alidai kuwa Septemba 29, 2008, washtakiwa hao (wa tano na sita) katika Ofisi Kuu ya Benki ya Barclays Tanzania Limited, iliyoko Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kwa ufahamu na udanganyifu, waliwasilisha fomu hiyo kuonyesha kwamba, kampuni ya Tourism Promotion Services (Tanzania) Limited iliomba benki hiyo kulipa kampuni ya East Africa Procurement Services Limited kiasi hicho cha fedha kwa madai ya kuiuzia vitu hivyo.Manyanda alidai pia kuwa katika shtaka la nne, kati ya Oktoba 6 na 30, 2008, washtakiwa wote sita, kwa makusudi ya kurubuni na kudanganya, walijipatia kutoka Benki ya Barclays Tanzania Limited kiasi hicho cha fedha kwa madai kwamba, kampuni ya East Africa Procurement Services Limited ilikuwa imelipwa na kampuni ya Tourism Promotion Services (Tanzania) Limited kwa ajili ya kuiuzia vitu hivyo.Alidai katika shtaka la tano, Septemba 30, 2008, mshtakiwa wa kwanza, Katiti, akiwa mwajiriwa katika Ofisi Kuu ya TRA, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam kwa makusudi ya kudanganya, aliandaa na kuwasilisha kwa mwajiri wake taarifa potofu kujaribu kuonyesha kwamba, kampuni ya Tourism Promotion Services (Tanzania) Limited ilikuwa imelipa kiasi hicho cha fedha kwa TRA kama Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Agosti, 2008, wakati akijua kuwa haikuwa kweli.Manyanda alidai katika shtaka la sita, Oktoba 6, 2008, mshtakiwa huyo akiwa mwajiriwa katika ofisi hiyo, aliandaa na kuwasilisha kwa mwajiri wake (TRA) nyaraka feki na kuonyesha kwamba, kampuni ya Tourism Promotion Services (Tanzania) Limited ililipa kiasi hicho cha fedha kwa TRA kama VAT Agosti, 2008 wakati akijua kwamba, haikuwa kweli.Alidai katika shtaka la saba, kati ya Septemba 29, 2008 na Oktoba 6, mwaka huo (2008), washtakiwa wote sita kwa pamoja walikula njama kufanya kosa la kutakatisha fedha haramu, kinyume cha sheria.Manyanda alidai katika shtaka la nane, kati ya Oktoba 6 na 30, 2008, katika Benki ya CRDB Tawi la Holland, lililoko Wilaya ya Ilala, washtakiwa wote sita kwa pamoja, walitakatisha kiasi hicho cha fedha na kuzihamisha kutoka kwenye akaunti namba 0121186000 ya benki hiyo inayomilikiwa na kampuni ya East Africa Procurement Services Limited kwenda kwenye akaunti namba 1065822, namba 600283 ya Benki ya Barclays Tanzania Limited na namba 240603610 ya Benki ya Biashara ya Kenya (KCB) na ya watu binafsi, wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la fedha haramu.Katika shtaka la tisa, Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru), Benny Lincoln, alidai kuwa Oktoba 6 na 30, 2008, mshtakiwa wa tatu na wa nne, kwa pamoja walihamisha kiasi hicho cha fedha kutoka kwenye akaunti namba 0121186000 inayomilikiwa na kampuni ya East Africa Procurement Services Limited katika Benki ya CRDB Tawi la Holland, hali wakijua kuwa fedha hizo ni pato linalotokana na rushwa.Lincoln alidai katika shtaka la kumi, Oktoba 6 na 30, 2008, washtakiwa wote sita walijipatia na kutumia kiasi hicho cha fedha hali wakijua kuwa fedha hizo ni zao linalotokana na rushwa.Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kurudishwa rumande kutokana na kesi za aina hiyo kutokuwa na dhamana kisheria.Wakili Manyanda aliiambia mahakama kuwa wako katika hatua za mwisho za upelelezi
   
 2. r

  rapamsomi90 Member

  #2
  Mar 1, 2014
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Watu wabaya sana. Niliisikia hii kesi. Iliishaje?
   
 3. Tembele

  Tembele JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2014
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 1,147
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndio Maana Mtu anaingia TRA yani baada ya mwaka ana pesa utafikiri anauza Madawa.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 4. r

  rapamsomi90 Member

  #4
  Mar 2, 2014
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni kweli. Kuna loopholes nyingi naona. Hawa jamaa walikuwa ndani bado. Sijui kama walishatoka
   
 5. D

  D_waziri Member

  #5
  Mar 2, 2014
  Joined: Nov 20, 2013
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  sema musipo iba mkale wapi!!!? maana we mwenyewe mwizi km sio mwizi unakula wapi na wenyewe wameshindwa vp kula unako kula,Hamasisha wenzio kufanya wa si kuiba tokomeza ualifu.
   
Loading...