Wasiolipia maji Kutangazwa kwenye vyombo vya habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasiolipia maji Kutangazwa kwenye vyombo vya habari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Mar 24, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WATEJA wanaotumia maji yanayosambazwa na Dawasco ambao hawalipii maji hayo kwa kipindi kirefu wataanza kutangazwa kwenye vyombo vya habari ili waweze kulipia maji hayo.

  Mbinu hiyo imekuja baada ya uongozi wa DAWASCO kuona ni mbinu mbadala itayowawezesha wananchi wasiolipia ankara zao za maji waweze kulipia kwa kuwa watakuwa wameumbuliwa kwenye vyombo hivyo.

  Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa DAWASCO Bi.Mary Lyimo amesema kuwa mbinu hiyo itawasaidia wateja kulipia bili kwa kuwa ile ya kukata maji imeshazoeleka kwa wateja wengi.

  Amesema shirika hilo lilikuwa likiwakatia maji wateja wake ambao wale wadaiwa sugu na matokeo yake baadhi wanarudisha maji hayo kinyemela na kubainisha kuwa kwa kuwataja kwenye vyombo vya habari itasaidia sana kutatua tatizo hilo.

  Amesema watawataja wale wote ambao wanaolisumbua shirika hilo kwa kutolipia maji kwa muda mrefu kwa kuwataja majina yao magazetini na sehemu nyingine na kutoa anuani zao ikiwemo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

  Source:Nifahamishe.com
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Laughable,

  Na mtu asipolipa je? Mtu mzima hatishiwi nyau, inabidi watu waanzishe collection agencies hapo wapewe deal la kucollect.
   
Loading...