Wasiolipia kodi viwanja kunyang’anywa Januari 2021

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema wamiliki wote wa ardhi walio na viwanja visivyoendelezwa na kulipiwa kodi ya ardhi kuhakikisha wanalipia viwanja vyao ndani ya siku 14 baada ya kupokea ankara ya madai na wasipotekeleza watanyang’anywa viwanja vyao na kupatiwa watu wengine.

Wizara hiyo imesema ankara zote zitakuwa zimeshawafikia wamiliki wa ardhi ifikapo Desemba mwaka huu na Januari mwakani watu wote wenye viwanja visivyoendelezwa ndani ya miaka mitatu na havijalipiwa kodi ya ardhi inayotozwa kwa mwaka, watanyang’anywa viwanja hivyo na kupewa watu wengine wenye mahitaji.

Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Denis Masami wakati wa kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi katika Mtaa wa Chidachi jijini Dodoma, ikiwa ni mkakati wa wizara kuhakikisha wamiliki wote wa ardhi wanalipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati.

Alisema Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia ofisi zake za ardhi za mikoa imeanzisha utaratibu wa kuwatembelea wamiliki wa ardhi kila mwisho wa wiki kwa lengo la kuhamasisha ulipaji kodi na kutoa elimu ili kuwawezesha wamiliki wa ardhi nchini kutekeleza jukumu hilo bila shuruti.

“Maeneo mengi nchini yana viwanja visivyoendelezwa na wakati huo wamiliki wake hawavilipii kodi ya pango la ardhi jambo linaikosesha mapato serikali, baada ya siku 14 tutaanza utaratibu wa kuzitwaa, kuvinadi ili kufidia deni na kumilikishwa kwa watu wengine,'' alisema Masami.

Mkuu huyo wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliongeza kwa kusema Wizara ya Ardhi inatekeleza mkakati wake wa kuhamasisha ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kushirikisha wataalamu wa sekta ya ardhi na makamishna wasaidizi wa ardhi katika mikoa kwa kupita nyumba kwa nyumba na kuwapelekea wadaiwa ankara za madai ya ulipaji kodi ya pango la ardhi na maduhuli mengine yatokanayo na sekta ya ardhi ili waweze kulipa.

Akiwa eneo la Chidachi jijini Dodoma na timu yake, Masami alibaini maeneo kadhaa yasiyoendelezwa na wamiliki wake kudaiwa kodi ya pango la ardhi sambamba na ukubwa wa eneo la Shule ya St Merys Dodoma kuonesha kuwa na ukubwa wa mita za mraba 900 wakati uhalisia ni hekta 3.5, jambo alilolieleza kuwa limeifanya shule hiyo kulipia kiasi kidogo cha kodi ya pango la ardhi.

Kwa upande wake, Ofisa Ardhi wa Jiji la Dodoma, Ruta Rwechugura alisema wakati wa kuwafuatilia wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi walibaini kukiukwa kwa baadhi ya taratibu na wamiliki wa ardhi na kutolea mfano ubadilishaji matumizi ya umiliki sambamba na baadhi ya wananchi kuuziana viwanja bila kubadilisha jina.

Aliwataka wamiliki wote wa ardhi walionunua viwanja kwenye maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha wanabadilisha umiliki kwa kufika ofisi za ardhi katika halmashauri husika ili kuiweka ardhi yao salama na kuwasisitizia wamiliki kutobadili matumizi ya viwanja vyao bila kufuata taratibu.

Hata hivyo, wakati wa kuwafikia wadaiwa wa kodi ya ardhi mmoja wa wananchi aliyefikiwa, Faustine Mwakalinga aliipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa uamuzi wake wa kuwafikia wamiliki wa ardhi kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha ulipaji kodi ya ardhi.

Alieleza kuwa utaratibu huo unapaswa kuigwa na watendaji wengine wa serikali katika kudai kodi kwani ni utaratibu ulio rafiki na unamhamasisha mdaiwa kulipa badala ya kuogopa.

Hivi naomba kujua, wajane hawana msamaha wa kodi, maana naona kuna wengine wanapata wanatumia masharti yapi kuwapatia wajane hawa unafuu wa kulipa kodi za ardhi
 
Mliotupangisha kwenye nyumba zenu mjiandae mtalipa mali,bikizo yote
Jiandae kuumia wewe, mimi serikali ikinipandishia makodi mengi na mimi napandisha kwa malipo yako ya kodi ya mwezi ili nipate unafuu na faida, mpangaji ndiyo una hali mbaya nimeshangaa ulivyojitoa hapo haraka
 
Kwa maoni yangu viwanja vyote vilivyo pimwa na vina hati miliki hivyo ndiyo vinapaswa kutozwa kodi, kodi inayo leta usumbufu lidogo Kwa wananchi ni kodi ya majengo haswa majengo ya kawaida ya wananchi wa kipato cha chini ambao wamejenga vijumba vyao Kwa kuunga unga. TRA hii kodi ya makadirio ya majengo iangalieni upya ili iendane Na uhalisia sio ilimradi tu, kuna madai mengi ya kodi ZA majengo yamelundikana ktk ofisi ZA serikali Za mitaa.... Wadaiwa hawajui,,
Nashauri utaratibu wa kodi ZA majengo uanze upya Kwa taratibu nzuri ambao utamfikia kila mwenye jengo/nyumba Na kodi italipika kirahisi Na bila bughudha.
 
Back
Top Bottom