Wasiofunga mwezi wa Ramadhani Nigeria wakamata na polisi

Status
Not open for further replies.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria kuna kikosi maalum cha polisi, Hizbah, kinawatia mbaroni baadhi ya waumini wa dini ya kiislaam wanaokula na kunywa mchana katika kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani.
923bb02ab960210fdf9862c6e5fbfca0.jpg

Tangu kuanza kwa mfungo juni 6, kikosi hicho cha polisi kimetawanya askari wake katika maeneo ya kimkakati kwa lengo la kuhakikisha mfungo wa mwezi wa ramadhani nguzo ya tatu katika dini ya kiislaam inatekelezwa kwa ukamilifu.

Wale wote wa wanaobainika kutotimiza masharti ya mfungo huwa wanapelekwa katika makao makuu ya kikosi hicho ambako wanapaswa kujieleza.

Naibu kamanda wa Hizbah, Nabahin Othuman amesema wale wote wanaokamatwa katika kipindi hiki kutokana na ukiukwaji wa kanuni, za mfumo wa ramadhani na hasa kuhusiana na kula na kunywa ovyo hadharani, watashtakiwa na adhabu yao inakuwa kucharazwa viboko hadharani.

Othuman amesisitiza kuwa kila muislam mwenye uwezo wa kiafya na anayewajibika lazima afunge ramadhani vinginevyo akabiliane na adhabu hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa kikosi hicho maalum cha polisi wanaosimamia utekelezaji wa dini ya kiislaam Hizbah kufanya msako huo kwa wasiofunga mwezi wa ramadhani katika jimbo la Kano.

Watu ambao wamekuwa wakiuza vyakula katika nyakati za mchana nao vilevile wanatiwa mbaroni, malalamiko kwa wasiokuwa waislamu ambao wamekuwa wakisumbuka kutokana na marufuku hiyo yamekuwa yakipuuzwa.

Chanzo DW kiswahili.
 
Muda si mrefu wataanza kuwakamata wale ambao watakuwa hawaendi kuhiji Mecca na Madinna.
 
Hivi huko Kano hakuwa watu wa dini zingine nje ya uislamu!? Je kama wapo wanakuwa treated vipi?
 
Kumbe unafunga kwakua wenzio wamefunga na sio kufuata maagizo ya Allah haina noma
 
Kumbe unafunga kwakua wenzio wamefunga na sio kufuata maagizo ya Allah haina noma
Sio hivyo mkuu wanaangalia sababu yenyewe ambazo ni kuumwa na safari au mama mwenye mtoto mchanga hao wameruhusiwa.
 
Dini nyingine ni ujunga.

Starehe yako unataka na mwingine aifuate.
 
Dini na Imani ni vitu viwili tofauti kabisa

Watu wengi Wana dini kwa sababu wamejikuta wamezaliwa kwenye hiyo dini,ila wengi kati yao hawana Imani. Kosa wanalofanya waislamu ni kuwalazimisha watu wenye dini na Majina ya kiislamu kufuata sharia wakati Imani hakuna.

Matokeo yake ni watu kuishi kinafiki. "Naomba mtusamehe kuanzia kesho tutafunga".. unafiki!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom