Tume ya Taifa ya uchaguzi imekataa maombi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) ya kuitaka tume hiyo kuruhusu watu waliopoteza vitambulisho vya kupiga kura wajaze FORM NO 17 kisha waruhusiwe kupiga kura katika uchaguzi wa ubunge Arumeru Mashariki.Hii ni kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi hasa vijana wa CDM wamepoteza vitambulisho vya kupiga kura na hivyo kukosa uhalali wa kupiga kura.
Haijajulikana ni kwa nini tume ya uchaguzi imekataa kuruhusu Form hizo kutumika kwani sheria ya uchaguzi inaruhusu kufanya hivyo kwa yeyote aliyepoteza kitambulisho cha kupigia kura.
My Take:Kwa tamko hili la NEC kuna hatari watu wanaonunua shahada za kupiga kura kutoka kwa wananchi watazidisha kasi yao kwani wanafahamu sasa tume ya uchaguzi imepiga marufuku matumizi ya FORM NO 17
Source:Nipashe