sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Kila jambo lina wakati,wakati wa magamba kukwanguliwa umefika.Wasifikiri Mh G Lema yupo pekee yake!amebeba ujumbe mzito nyuma ya pazi.Ujumbe huo ni kilio cha wanyonge.hata ikitokea akatangulia mbele ya haki athari atayoiacha ni pigo kubwa kwa wanan wa magamba na madhalimu wote katika nchi hii.Fikra mgando hazina mashiko mbele ya jamii iliyodharauliwa na kupuuzwa na kikundi cha watu wachache wenye kuitumia taasisi hii ya uaris vibaya.Ikulu si mahali pa kucheka cheka na kukaribisha washoga.Ikulu ni mahali patakatifu.ukitaka kwenda ikulu uwe na uthubutu wa kuwaambia watoto wako kuwa urais wangu si wa familia yangu,dhamana niliyopewa na Watanzania si dhamana ya kujilimbikizia mali na kuwapachika watoto wa shangazi,mashemeji na nyumba ndogo.Ikulu si sehemu ya kulipiza kisasi kisa waziri mkuu wako kaambiwa muongo.Ukiweza kuwaambia watoto wako na mkeo hivyo basi hata wale matapeli hawatathubutu kukusogelea na kukuletea dili za kuiangamiza nchi
Mwisho,mwacheni G.Lema afanye kazi yake,anatumwa na dhamira iliyojaa uzalendo na mapenzi kwa wananchi na taifa lake.Interejensia itumike vizuri kuwakamata Al shabab na siyo kudhibiti demokrasia nchini.Lema ni mtu mdogo sana ila mwenye dhamira ya kweli kwa ukombozi wa kifikra toka mikono dhalimu ya wakoloni weusi.Wamepita wanaharakati wengi kama Che Guevera na wenzake,harakati zao zilipingwa na madhalimu wote wenye lengo baya lakini athari yake imesimama miongo kwa miongo.Matunda ya kina Che Guevera ni mazalia mapya ya chimbuko la kina Lema.Atapita Lema impact atayoiacha ni kubwa kuliko nguvu zinazotumika kuzima fikra pevu za wanaharakati wachepuao.viva Lema viva.Aluta Continua mapambano ndo kwanza yanashika kasi