Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura: Kwa nini darasa la saba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura: Kwa nini darasa la saba?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by uvivumwiko, Oct 29, 2010.

 1. u

  uvivumwiko Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengi wa Wasimamizi na makarani wa vituo vya kupigia kura Jimbo la MONDULI kwa uchaguzi utakaofanyika 31/10/2010 ni wahitimu wa darasa la saba. Ni ukweli dhahiri kuwa mhitimu wadarasa la saba hana uelewa wa kutosha kumwezesha kuwa msimamizi wa kituo cha kupigia kura. Madhara ninayofikiri kuwa yatasababishwa na watu hawa ni :

  1. kuchelewesha wapiga kura kupiga kura
  2. kutofuata sheria na kanuni za uchaguzi ipasavyo
  3. kudanganyika kwa urahisi na kusababisha kutolewa matokeo yasiyo sahihi
  Kwa maoni yangu tume imeogopa kuajiri watumishi wa serikali na wasomi ili kuipa CCM nafasi ya kuiba kura. Ili kudhibiti hali hii inabidi mawakala wawe makini kufuatilia hatua zote za upigaji kura na uhesabuji na ujazaji wa fomu za matokeo
   
 2. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kule form four hawezi kupewa nafasi yeyote kama hiyo kwa sababu kama hizo hizo...! Kwa sasa Lowasa anawalaumu vijana waliosoma kidogo huko Monduli kwa kisingizio kuwa wanawafumbua wengine macho, na kuwatumia vibaya....! Hii imedhihirika pale aliposhuhudia msimamo wa vijana wa Kimaasae katika kijiji cha Mti Mmoja kilichopo takribani kilomita 43 kutoka Arusha mjini...! Na kwa kusema ukweli kule Monduli huhitaji ulinzi wa hali ya juu sana, maana kizazi kipya kinahitaji mabadiliko, lakini wazee wa kimila wanatumika kuwavunja nguvu na kule mzee wa boma ndiye anayeamua kura za wake zake na vijana wake ziende kwa nani, hivyo hakuna haki inayotendeka kule kabisa....! Hata hivyo, watoto wenye miaka 15 huandikishwa kwa ajili hii na huwa hakuna ukaguzi wa kutosha, ilimradi tu awe na mwili wa kuridhisha....! Vilevile kule lazima kutakuwepo na vituo feki, na idadi feki ya wapiga kura lazima ibuniwe....! Hakika natamani ningekuwepo kule kuanzia leo...! Naamini ningekuwa na nafasi yangu...!
   
Loading...