Wasimamizi wa Uchaguzi wanatumiwa na CCM

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
609
1,540
CHAMA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT – WAZALENDO)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) kimekuwa kikifuatilia kwa karibu mwenendo wa Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano, Wabunge na Madiwani hapa nchini ambao kwa sasa upo katika hatua ya Uteuzi.

Kama ilivyo kawaida katika Chaguzi zote zilizopita, tumeanza kushuhudia mizengwe, njama na hujuma mbali mbali zinazofanywa na wasimamizi wa Uchaguzi waliokosa maadili ya Uchaguzi wakishirikiana na vyombo vya Dola.

Ndugu Waandishi, nyote ni mashahidi kuwa katika chaguzi za hivi karibuni, Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na uoga na udhaifu wake wa kutopenda kushiriki katika Uchaguzi kwa hofu ya kukataliwa na Wazanzibari na Watanzania kama ilivyotokea katika Uchaguzi wa 2015, wameasisi sera ya “Ushindi wa Bao la Mkono” ambao ni mjumuisho wa matendo yote maovu yanayowawezesha kushinda Uchaguzi kwa njia zilizo kinyume na utaratibu wa Uchaguzi.

Ndugu Waandishi, katika utekelezaji wa Sera hiyo, CCM wanashirikiana na baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi na Wasaidizi wao kuwaengua wagombea wa baadhi ya Vyama vya Upinzani kwa kuwaekea pingamizi zisizokuwa na mantiki huku wakijinasibu kuwa wamepita bila ya kupingwa. Matendo haya ya kihuni hayajaanza leo na nyote mnakumbuka kuwa yalishamiri sana katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wagombea wa upinzani walienguliwa kwa kisingizio cha kukosa sifa.

Ndugu Waandishi, CCM na baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi wamenogewa na mchezo wao mchafu wa mwaka 2019 wakati wa Serikali za Mitaa na sasa wanaurudia tena Kwenye Uchaguzi Mkuu.
Kama hiyo haitoshi, mbinu hizo chafu sasa zimehamishiwa Zanzibar na watekelezaji wa mikakati hiyo ni Wasimamizi wa Uchaguzi ambao wengi wao wameletwa kutoka Tanzania Bara na kupangiwa vituo vya kazi Kisiwani Pemba, kwa lengo la kuchafua mchakato mzima wa uchaguzi na pia kuvuruga amani ya Nchi.

Ndugu Waandishi, Chama chetu hakipingi mgombea yoyote kuwekewa pingamizi dhidi ya wagombea wetu ikiwa hoja za pingamizi ni zenye mashiko na za wazi huku utaratibu wa uwekaji na usikilizaji wa pingamizi hizo ukizingatiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni kama kinavyoelekeza Kifungu cha 51(1) – (8) cha Sheria ya Uchaguzi Na 4 ya Mwaka 2008.

Kinachojitokeza sasa katika majimbo ni hujuma na mitego dhidi ya wagombea wa ACT-Wazalendo na kwamba wasimamizi hao ni wazi kabisa wameshindwa kusimamia Kanuni na Sheria za Uchaguzi kama ambavyo nitaeleza hapa nchini.

Tunazo taarifa mathalan kwamba;

 Wilaya ya Micheweni
Afisa wa Uchaguzi amewajulisha Wagombea wetu kuwa wote wamewekewa pingamizi na taarifa za pingamizi zao watapatiwa asubuhi ya leo (27/08/2020).

 Wilaya ya Mkoani
Afisa wa Uchaguzi amewaambia Wagombea wetu kuwa waende leo asubuhi, kama kuna pingamizi atawajuilisha

 Wilaya ya Chake Chake
Wagombea wa Majimbo manne (Chake Chake, Ole, Wawi na Chonga) wamewekewa pingamizi.

- Wagombea wa Wilaya ya Chake Chake wamepingwa kwa kuambiwa hawana sifa za kugombea.

- Jimbo la Chonga: Mgombea amebambikiziwa sababu ya kutokuwa na risiti ya malipo ya Mahkama

- Jimbo la Chake Chake: Mgombea pia amebambikiziwa sababu ya pingamizi kuwa hakuwasilisha Tume barua ya udhamini kutoka Chama chake.

 Wilaya ya Wete
Wagombea wa Majimbo matatu (Kojani, Mtambwe na Pandani) wamewekewa pingamizi kwa visingizo vya kuwahi kushtakiwa.

UNGUJA (Mathalan):

Katika hali inayodhihirisha unyama wa Juu kabisa, wameshuhudiwa Msimamizi wa Uchaguzi wa NEC Ndugu Hassan Abdalla Ali na Mgombea wa CCM Jaffr Sanya Jussa kwa pamoja wamemvamia, Kumshambulia na kumsababishia maumivu makali Mgombea wetu wa Jimbo la Paje Ndugu Sabah Khamis Abdulla. Tukio hili limetokea ndani ya ofisi ya NEC Wilaya ya Kusini-Unguja. Lengo la kumvamia huko ilikuwa ni kumnyang’anya barua ya pingamizi aliyopewa na Msimamizi mwenyewe. Mgombea wetu ameripoti Kituo cha Polisi Makunduchi na kupewa RB 1069 pamoja na kujaza fomu nambari Tatu ya Polisi (PF 3) kwa ajili ya matibabu.

Ndugu Waandishi, Hiyo ni mifano michache ambapo yapo matukio mengi ya namna hiyo, pamoja na kwamba pingamizi zote hizo hazikufuata taratibu za kisheria, ambapo Wagombea wetu hawakupewa hata nakala za Barua, Fomu za Pingamizi wala Barua za Wito, badala yake wakipewa maelezo ya mdomo au wachache kwa njia ya simu.

Hayo yanatendeka ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles S. Kaijage ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa na Makamo wake Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Wote hao ni wazoefu katika masuala ya Sheria za Nchi hii na pia za Kimataifa.

Hayo pia yanatendeka wakati ambao viongozi wanahubiri amani, utulivu na kuwahakikishia wananchi uchaguzi huru na waki ambapo hata nyinyi waandishi ni mashahidi wa hilo; kwa hali ilivyo sasa hatuamini kwamba tunaelekea huko.

Sisi tunasema AMANI NI PAMOJA NA IMANI ambayo kwa sasa inaanza kufifilizwa na mwenendo huo; Kwa hivyo hatunabudi kusema na kukiri BILA YA HAKI HAKUNA AMANI! Sisi ACT Wazalendo tunaamini usemi huo kwani mahala isipotendwa haki na amani haiwezi kuishi.

WITO WETU
Ndugu Waandishi, Watanzania na hasa kwa Upande wa Zanzibar bado wanayo kumbukumbu ya maumivu ya kuzimwa sauti yao katika Uchaguzi Mkuu 2015 uliosababishs Jecha Salum Salum kuufuta Uchaguz ule. Hivyo tunainasihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuheshimu Sheria, katiba na Kanuni zilizopo na kamwe wasikubali kutumika kama mawakala wa kuitafutia CCM ushindi wa kupita bila kupingwa. SISI HATUTAKUBALI NA TUTAUPINGA USHINDI WA NAMNA HIYO KWA NJIA YOYOTE ILE.

Ndugu Waandishi, Chama cha ACT Wazalendo kinainasihi Tume ya Uchaguzi NEC kuchukua hatua za haraka kutumia mamlaka yake chini ya Kanuni ya 11 ya Kanuni za Uchaguzi, kuwabadilisha Wasimamizi wa Uchaguzi walioshindwa kutekeleza majukumu yao na hatimae kuangukia kuwa mawakala wa Chama cha Siasa. Wsimamizi hawa na hasa waliopangiwa kusimamia kisiwani Pemba wasipochukuliwa hatua za haraka za kuondolewa ipo hataru ya kuingiza Nchi kwenye machafuko kutokana na mienendo yao.

Pamoja na yote na ndivyo ilivyo kwamba Uchaguzi ni zoezi la kisheria chini ya misingi ya katiba na ambalo linabeba sauti ya umma katika kufanya maamuzi juu ya uongozi bora, sambamba na kujipatia viongozi na serikali halali ya kuoiongoza nchi.

Bali, kwa mwelekeo wa sasa ni dhahiri kwamba vitendo vyote hivyo havidhihirishi dhamira njema, bali kinachodhihiri ni utashi wa baadhi ya watu kuichelewesha, kuidhoofisha kama siyo kuipora kabisa sauti kubwa ya haki ya umma, jambo ambalo bila kusita wala kupepesa, sisi kama Chama na Taasisi iliyobeba matumaini makubwa ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla tunasema SASA BASI, INATOSHA!.

Indhari yetu ni pamoja na mambo yafuatayo:

1. Tunaelewa kwamba Wasimamizi wa Tume ta Taifa ya Uchaguzi (NEC) waliopo Zanzibar wameletwa kwa kazi maalum ya kuchafua zoezi hili la kidemokrasia na kudhoofisha Sauti ya haki ya Wazanzibari; Hivyo lazima ieleweke kwamba Umma hautoridhia na hautalikubali hilo asilan abadan!

2. NEC wasijivishe joho la uamuzi wa haki ya umma, bali ni vyema wakachukua jukumu la kusimamia na kuratibu zoezi la Uchaguzi wa Haki, kupitia misingi ya uadilifu ili kuruhusu ushindani wa hoja na sera katika sanduku la kura, na hivyo TUNAITAKA TUME WATUWACHIE TUPAMBANE NA CCM KWA HOJA NA SIYO KUWAPA MBELEKO.

3. Ni vyema NEC na mamlaka zote za kusimamia Uchaguzi wakatambua kwamba bila ya kuwepo wagombea hapatokuwa na Uchaguzi; Hivyo tunasema BILA YA WAGOMBEA, NO ELECTION!

4. Kufuatia mwenendo unaoshuhudiwa sasa wa kuendelea kuipinda haki, tunaiambia NEC: MUSIWASHE KIBERITI KATIKA DUMU LA PETROLI kwani yatakayojiri nyinyi ndio mtakaowajibika na mtabeba dhima.

Mwisho tunasisitiza kwamba BILA YA WAGOMBEA, NO ELECTION!

Ahsanteni sana!

IMETOLEWA NA:
NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU - ZANZIBAR


IMG-20200827-WA0048.jpg
 
CCM wameshasema hawawezi kuondoka kwa amani lazima imwagwe damu Kwanza. Sasa ni suala la.kusuka ama kunyoa
 
Mahakama kuu ililiona hilo, lakini vibaraka wa CCM walioko mahakama ya rufani wakaamua kupindisha haki.

Amani ikivurugika tutaanza nao wasaliti wakubwa wa katiba na viapo vyao hao.
 
Chama Cha Mapinduzi(CCM), Nanukuu " Hatuwezi kutoka madarakani kwa makaratasI(kura) "
 
Ulalamishi ufike kikomo--- fanyeni haya:
Ndugu ndugu wapinzani,
Mumeona jinsi munavyo enguliwa na hao NEC bila sababu za msingi.
Mumeona jinsi haki yenu ya uchauguzi isivyopatikana kwa watu wetu kuengulia kwa sababu ya msingi (Breaches of Fundamental rights)
Mumeona jinsi mapingamizi yenu yanatupwa bila sababu za msisngi...
Hivi kweli mnavyoona mtapa haki sawa huko mbeleni? Thubutu

Kwa nini msiwafunguliwe kesi ya ubaguzi hao NEC na muiombe mahakama iistopishe NEC kuendesha au kusimamia zoezi zima la uchaguzi huu?

Kuendelea nayo hii NEC ya sasa maana yake ni kwamba :
1. Mumekubaliana na figisu zote za NEC za sasa
2. Mumekubali kwamba wakisha tangaza matokeo (Uraisi) hamtaweza kuyapinga au kuyahoji mahala popote Tanzania maana ni kinyume na sheria
3. Mumekubali kwamba uchaguzi utakuwa free na fair ingawaje yale yale yaliyotokea serikali za mitaa yanajirudia.
4. Mkiishitaki NEC kwa certificate of urgent (breaches of fundamental rights ) kwa kuwapendelea CCM au kwa kutofuata sheria za uchaguzi na kanuni zake kinachoweza kufanyika ni kati ya haya yafuatayo:

1. Mahakama kuwarudisha wagombea wote walionguliwa kwa sababu za magumashi
2. Mahakakam kuisimamisha NEC kuendela na zoezi zima la uchaguzi mpaka hapa watakopo kuwa wameonyesha kwamba wao sio biased
3. Mahakama kuagiza tume huru itayounda na watu huru...

Hii ndio njia pekee iliyobakia kwa sasa hadi 28 October.
Tarehe nyingine ya uchaguzi inaweza kupangwa (kama itakavuo amuliwa na mahakama) ili kurekebisha dosari zote za uchaguzi kurekebishwa...
Hamuwezi kuendelea na ushaguzi huu ili hali ubaguzi wa haki zenu za msingio ziko wazi... referee wenu- NEC- hana uwe3zo tena wa kusimamia zoezi zima la uchaguzi utao kuwa free an fair maana tayari amekwisha onesha uwezo wake - hana uwezo huo kwa kuusimamia

Ni ushauri tu na maoni yangu binafsi... si lazima mmchukue... msipotaka hivyo, hakuna njia ya kuyahoji matokeo wala ukiukwaj wa taratibu maana mtakuwa mmekubaliana na yote NEC iliyowafanyia...
 
Back
Top Bottom