Wasimamizi wa uchaguzi wana mamlaka ya kuamua uraia wa mgombea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasimamizi wa uchaguzi wana mamlaka ya kuamua uraia wa mgombea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Aug 23, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau – kuna masuala yananitatiza hapa kuhusu hawa wasimamizi wa uchaguzi ambao tunaambiwa ni wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa hivyo wako huru. Lakini pia tunajua hawa ni watumishi wa umma yaani wakurugenzi wa wilaya (ma-DED) walioteuliwa na serikali ya CCM katika nyadhifa hizo.

  Maswali yangu - na mkazo nimeweka katika suali la mwisho:

  1. NEC yenyewe ina mamlaka kiasi gani katika maamuzi ya kutwateua hawa au katika kuwahamisha vituo? Yaani NEC huwa inashirikishwa katika maamuzi hayo?

  2. Hivi wapo hawa ma-DED ambao ni wa vyama vya upinzani yaani CUF au Chadema?

  3. Nakumbuka katika uchaguzi wa 2005 kuna msimamizi mmoja wa NEC mkoani Tanga ambaye alikuwa DED aliondolewa katika kazi hiyo ya usiomamizi wa uchaguzi kwa sababu alikuwa waziwazi anamshabikia mgombea wa CCM. Hiyo hatua ilikuwa sawa – lakini jee, yule mbadala aliyeteuliwa, NEC ilishirikishwa?

  4. Mwaka huu CCM imevunja rekodi kwa wagombea wake wa Ubunge kupita bila kupingwa na kati ya hao kuna baadhi wameenguliwa kutokana na pingamizi zilizowekwa na wagombea wa CCM ambazo zilikubaliwa na hawa ma-DED na zile za wapinzani kutupwa (isipokuwa moja ya Mbowe). Jee hii haitii wasiwasi ya maamuzi ya hawa ma-DEd ambao ni makada wa CCM?

  5. Katika jimbo la Nyamagana ambako pingamizi la mgombea wa CCM – Lawrence Masha (ambaye ni waziri wa Mambo ya Ndani) lilikubaliwa kwamba yule mpinzani wake wa Chadema siyo raia wa Tanzania. Jee, Msimamizi wa uchaguzi ana mamlaka ya kuamua (baada ya kupata vielelezo) kwamba fulani ni raia au la? Haya mamlaka kayapata wapi? Navyofahamu mimi mamlaka ya masuala ya uraia panapokuwa na utata ni mahakama. Isitoshe, tusisdahau hapa kwamba Masha ni Waziri ambaye Idara ya Uhamiaji iko chini yake. Kweli haki imeonekana kutendeka, achilia mbali iwapo imetendeka?
   
 2. c

  chama JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mdau Zak malang hii mada ni tamu sana hebu jaribu kututafutia sifa za mgombea wa chadema ili tuone alikuwa tishio kiasi gani inawezekana kabisa huu ni umafia mtupu uliofanyika, ccm imetumia umafia huu kuwaengu wagombea wasiowataka ndani ya chama chake inawezekana kabisa huu ni muendelezo wa umafia. Hii NEC isikuumize jiulize inatekeleza kazi zake chini ya serikali ipi nadhani jibu unalo; NEC haitakuwa huru mpaka mabadiliko ya katiba yatakapofanyika !
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nilimsikia yule Msimamizi wa NEC kule Nyamagana akisema kuwa kosa alilolifanya Mgombea wa CHADEMA ni kutokanusha madai ya Masha.
  Eti malalamiko hayo yalipotolewa na Masha yeye (Mgombea wa CHADEMA) alikaa kimya tu na ndio maana wakaamua kumwengua kwani kwao NEC silence means 'Tuhuma juu yako ni za kweli'
   
 4. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nyamagana (Kabwe) alisema mgombea wa CHADEMA hakupeleka vithibitisho kukanusha tuhuma za zilizokuwa zinamkabili.
  Ila hakutaja ni vithibitisho gani alitakiwa kupeleka kukanusha madai ya Masha.

  Swali la msingi hapa ni, Je msimamizi wa uchaguzi anaruhusiwa kuthibitisha uraia wa mtu na kutoa maamuzi kama alivyofanya Bwana Kabwe?!

  Hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo...
  Mpaka raha...
   
 5. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mpenzi wa siasa na mara nyingi ukisiliza mazungumzo ya watu wa kawaida tunapenda kusema ni mchezo mchafu. Lakini kwa haya yanayotokea sioni kama kuna hata mchezo. Nahisi ni nguvu tu inayotumika kumpitisha huyu au yule bila kupingwa bila hata kutumia akili.

  Tuseme siasa ni akili. Na kweli akili itumike badala ya nguvu na upuuzi huu tunao uona.

  Unaweza ukakuta kwamba hata hizo tuhuma hata hakupelekewa rasmi kwa makusudi kabisa! Ni kama ulivyosikia mgogoro wa TUCTA na kikwete. TUCTA wanaaalikwa waende mkutanoni mchana kwa barua, inafika mchana wanaambiwa mkutano umefanyika asubuhi!

  Lakini hata hivyo, naamini kabisa kwamba Chadema wana wanasheria wazuri akiwemo Marando aliyejiunga hivi karibuni. Nadhani kuna kitu wanachoweza kufanya kurekebisha upuuzi wa kiwango hiki.
   
 6. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ni upuuzi usio kifani mana masha ndiye aliyemsaidia mtot wa jk kuarchive certificate yake ya advocate kwa kumfanyia mtihani na huyo wilson kabwe ndiyo mkurugenzi wa jiji la mwanza tena fisadi wa kutupa.we unafikiriaje apo?
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani hilo linchi sijui limelaaniwa? Katika mazingira haya ambayo CCM imefanya kila kitu kuwa na bei mgombea atashindwaje kuwanunua wagombea wengine ili apite bila kupingwa?

  Mimi nilifikiri kwa demokrasia yetu changa NEC na Tendwa wafanye kazi ya kuhakikisha demokrasia inakua lakini naona wao ndiyo kwanza wanajifanya wanfuata taratibu, ukiuliza utaambiwa hata Marekani wanafanya hivyo. Lakini huwa wanasahau ni Marekani huko huko raisi akianguka, akikoswakoswa na kiatu wanachi wanaonyeshwa kwenye TV.
   
 8. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Masha ni muoga kwa nini hakupenda washindane kwa sera za vyama akakimbilia kuwa huyu jamaa sio raia, je kuna ukweli hapo na Masha alipeleka vielelezo au katoa malalamiko tu.Kweli ukisikia uchu wa madaraka ndio huu.Ila hio sio dawa ni lazima CCM wang'olewe mwaka huu.
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Zak, hii thread imekuja wakati muafaka, na inabidi tujiulezemasuala kadhaa kwa mfano:

  1. Je bado tunahitaji sheria ya uchaguzi kama ilivyo sasa, hasa tukizingatia kuwa sheria hii ilitungwa wakati wa mfumo wa chama kushika hatamu na sasa ni mfumo wa vyama vingi.

  2. Je tume ya uchaguzi wanasimamia utashi wa wananchi au utashi wa watawala, nani anasimamia daftari, nani anasimamia uchaguzi, nani anatoa elimu ya uraia kwa wapiga kura nani anateua waangalizi wa uchaguzi na mwishoni kabisa na anacheki abuses katika sehemu zote hizo?

  3. nani anafanya checks kuhusu wajumbe wa tume na sifa za kuwa mjumbe wa tume ni nini?

  Kwa ujumla je Tume inaweza kuonekana kuwa inatenda na au imetenda haki?
   
 10. c

  chama JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii kali sijawahi kusikia, kwa mtaji huu wengi tutakuwa sio raia wa Tanzania
   
 11. G

  GEOMO Senior Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mpaka hapo Masha anazidi kudidimia kwenye tope zito la kutofaa kuwa hata kiongozi wa kundi la mbuzi. Hivi unadhani hata kama malalamiko ya masha yangepelekwa uhamiaji, bado haki isingepata nafasi ya kutendeka maana ili kufikia itimisho la maamuzi ya idara ya uhamiaji bado masha huyohuyo ambaye ni mlalamikaji angeshiriki ktk kutoa maamuzi. Si mnakumbuka alivyoitwa fasta kutoka mwanza kurudi dar ili akadhibitishe maamuzi ya uraia wa Bashe? Sasa ndo watu makini wataelewa kwa nini mradi wa vitambulisho vya uraia umezungushwa kwa mda mrefu wote huo. Potelea mbali hata wakisema mm si mtanzania lakini ukweli ni kwamba Kikwete na serikali yake yote chini ya mwavuli wao wa c c m wanatakiwa kupelekwa dhieg kama walivyopelekwa waharifu wengine.
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Maswali ni mengi zaidi:
  1. Masha aligundua lini kuwa mpinzani wake sio raia wa Tanzania?
  2. Kama waziri wa mambo ya ndani ya nchi alichukua hatua gani?
   
 13. D

  Dopas JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maswali ya msingi haya mkuu. Ila kwa nchi hii iliyojaa ufisadi nani anahangaika na uraia wako kama huingilii kula yao. Wewe hujiulizi katika siku 366 kwanini swala la uraia lijitokeze wakati huu tu. Subiri 1/11 kama kuna mtu hata huyo Masha na idara zote zitasema chochote kuhusu uraia wa mtu. Ni bahati mbaya wengine hushindwa kujitetea hata pale wanapokuwa na haki ya kufanya hivyo. Ukitaka kujua kama wewe ni raia wa nchi hii kweli jaribu kujiingiza kwenye kula ya hao majamaa..... kitakachokutokea......:lol:
   
Loading...