Uchaguzi 2020 Wasimamizi wa Uchaguzi (Wakurugenzi) wanachafua sura ya CCM, Jimbo la Kibamba Msimamizi wa Uchaguzi awajibishwe

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Wanabodi, nilianzisha uzi hapa kuhusu watendaji wa Serikali kuharibu taswira ya CCM, Watendaji wa Serikali wao hawana uchungu na chama wanaangalia mishahara na familia zao tu, Makosa ya watendaji wa serikali yanageuzwa kuwa CCM imewatuma kuvuruga upendo na Amani. Kuna baadhi ya mambo yamefanyiwa kazi mfano lile la kuruhusu vyombo vya BBC na Voa kuendelea na matangazo Katika uzi huu,

CCM hatuna hoja za kumjibu Tundu Lissu, tunakwamishwa na watendaji wa Serikali

Leo kuna kosa tena la Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kibamba Mama Beatrice ameanza kukichafua chama kwa kuficha fomu halisi ya mgombea ubunge wa CHADEMA Jimbo la Kibamba.

Ni dhahiri ameanza kutengeneza chuki dhidi ya chama cha mapinduzi.

Mamlaka chukueni hatua kali juu ya hawa watu kama hawa, Huyu Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kibamba wanatuchafulia chama mbele ya wananchi.

Kuna mbinu nyingi za kushinda uchaguzi ila sio za chuki na kuwakasirisha wananchi kama hii aliyotumia Mama Beatrice Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kibamba.

Mama Beatrice ameficha fomu mwenyewe anasingizia amempa mtu asiyemfahamu.

Mbinu kama hizi ndizo Tundu lissu a nazidi kupata wafuasi wengi huko Tunduma Mbeya.

Leo Tundu Lissu amewaaminisha malaki ya wananchi Tunduma kuwa TRA inatumwa na CCM kufilisi wafanyabiashara na kubambika kesi kwa wafanyabiashra.

Kosa la watendaji wa TRA sasa CCM inabeba mzigo usiobebeka.

Hili la Kibamba Msimamizi wa uchaguzi tayari anampa nguvu Tundu Lisu Kuhubiri kuwa wasimamizi wa uchaguzi wanakibeba chama chetu cha ccm hivyo hatakubali matokeo.

Kuna mambo ya msingi chama changu cha CCM kinapaswa kufanya.

Mosi, Kujitenga hadharani na watendaji kama hawa wa Kibamba kwa kuwakalipia na kuwaambia wananchi kuwa ccm hakijawatuma kuficha fomu za mgombea wa Chadema.

Pili, CCM itamke hadharani kuwa haiusiki na utekaji au kupiga watu risasi, Kama watendaji ndio walifanya CCM ijitenge nao, Tundu Lisu amegeuza makosa ya watendaji wa serikali kuwa ni ya CCM na wananchi wanayaamini huko Tunduma.

Huko Tunduma CCM imegeuzwa kama genge la utekaji, ufilisi wa mali za wakulima na wafanyabiashara na kundi la kihalifu kwa hoja alizozijenga Tundu lissu, Kosa sio CCM bali washauri na watendaji wa serikali.

Msimamizi wa uchaguzi Kibamba anakiabisha chama chetu cha CCM kwa kujenga chuki mbele ya wananchi
 
Kiongozi huyu Mama anafanya kwa maslahi ya nani?

Leo hii ugumu huu wa siasa kosa sio la Rais bali ni baadhi ya watendaji wa serikali kupotosha ushauri kwa Rais

Juzi walianza kuzuia BBC na Voa tulionya hapa

Leo tena wanahamia taasisi ya haki za binadamu ili kuwaaminisha ulaya uchaguzi haukufuata haki za binadamu

Hawa watendaji wanawaza kitu gani sijui
We jiulize tu ni kwanini hawachukuliwa hatua?

CCM iko Siku mtakuja juta kumuogopa mtu fulani ambae ndio anakimaliza chama chenu.
 
Kwa faida ya wanajf na wengine Sura yake huyo mkurugenzi Anayeitwa Beatrice Dominic hii hapa
2244685_Mkurugenzi_wa_manispaa_ya_Ubungo_Beatrice_Dominic__amekiandikia_barua_chama_cha__640_X...jpg
 
Kilichofanywa na huyu mama ni uzembe mkubwa sana na in aibu kwa tume, hivi inakuwaje unampa MTU fomu asiyekuwa na anuani? Tume makao makuu washughulikie changamoto ya kibamba, ni moja ya kiashiria cha uvunjifu wa amani

Kama sio tume inahusika na hiyo hujuma tunatarajia kuona hatua. Hapa ndio nitajua kama tume ni huru ama la.
 
Nikuhakikishie kwa asilimia 100000000% hakuna mwana kibamba anayeweza kumpigania mtu, usijpe matuma ini hewa
Unawafanya Wananchi wa Kibamba hawawezi kufahamu hila zenu?Hiyo fomu DED anayosema hawezi kutoa mbili,ameitoa kienyeji mno as if haina thamani anayoitetea mbele ya Viongozi halali wa CDM.Amepewa options ya kupelekewa barua inayokanusha kuwa hakuwa mgombea wao na DED kakataa?

Hiyo fomu ni kifo ambacho hutokea Mara moja maishani?Je,kwa nini asiwape CDM fomu nyingine,zikirejeshwa zote mbili yeye kama msimamizi atampata hiyo aliyemtapeli ili sheria ichukue mkondo wake?Anafahamu alivyo haribu zoezi mapema kwa kumnyima mgombea halali fomu ya ugombea.
 
Mama anatoa fomu kienyeji utadhani anagawa uchi fomu kweli unatoa kirahisi tu Hakuna namba ya simu, Hakuna vitambulisho vingine, hakuna anuani hakuna uthibitisho wowote means kumbe muhuni yeyeto tu anaweza chukua tu fomu. Pili ataki kutoa ushirikiano
 
Huyu mama amatrend kinyama Dunia nzima inaangalia uhuni ulitokea huko kibamba
 
Back
Top Bottom