Wasimamizi wa ndani wathibitisha madai ya Dr. Slaa


R

Rugemeleza

Verified Member
Joined
Oct 26, 2009
Messages
668
Likes
6
Points
35
R

Rugemeleza

Verified Member
Joined Oct 26, 2009
668 6 35
waangalizi wabaini kasoro katika kuhesabu kura Send to a friend Friday, 05 November 2010 08:45 0diggsdigg

Geofrey Nyang'oro
WAANGALIZI wa ndani wa wameeleza kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 ulikuwa huru na wa haki lakini kulikuwa na kasoro kwenye kuhesabu kura, kwa mujibu wa ripoti yao ya awali.

Waangalizi hao pia wamependekezwa kufumuliwa kwa Tume ya Uchaguzi na kuundwa upya ili isishirikishe wakurugenzi wa halmashauri ambao imewaelezea kuwa ni watumishi wa serikali ambao daima wanakitii chama kilicho madarakani.
TACCEA, muungano unaoundwa na mashirika 17 na unaofanya kazi chini yab uratibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), imesema ingawa kasoro zilianza kujitokeza wakati wa kuhesabu kura.
Akisoma ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Msemaji mkuu wa TACCEA, Martina Kabisa alisema hali hiyo inatokana na mchakto huo kukumbwa na vitendo vinavyokiuka haki za binadamu.

"Uchaguzi huu ulifanyika katika mazingira huru. Watu walishiriki kampeni na hata kupiga kura. Lakini kumekuwa na matukio mengi yaliyofanya uchaguzi mzima kutokuwa wa haki," alisema Kabisa katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya LHRC.

Kabisa alitaja baadhi ya mambo yanayofanya uchaguzi huo kutokuwa wa haki kuwa ni pamoja na kuchelewesha matokeo katika maeneo ambayo upinzani una nguvu na ambako upinzani ulikuwa na uwezekano wa kushinda.
Kabisa alisema malalamiko ya Dk Slaa dhidi ya uchakachuaji wa kura pia yamethibitishwa na waangalizi hao waliosambaa kila jimbo. Aliitaka Tume ya Uchaguzi (Nec) kutopuuza malalamiko hayo na badala yake iyafanyie kazi ili haki itendeke.

"Madai ya kuwapo kwa tofauti za kura yamethibitishwa na waangalizi wetu walioko kwenye vituo mbalimbali kote nchini. Wametueleza kuwa kura zinazotangazwa ni tofauti na kura za vituoni. Sasa tunaomba Nec iyafanyie kazi madai hayo kama mhusika atakuwa amefuata taratibu za kisheria katika kuyawasilisha," alisema Kabisa.

Katika hatua nyingine umoja huo umependekeza Nec ifumuliwe na kufanyiwa marekebisho ili iwe huru na haki.
Walisema tume hiyo inayosimamia uchaguzi mkuu siyo huru na haitendi haki. Hali hiyo ndiyo inatia shaka kuwa ndio chanzo cha kasoro mbalimbali zilizofanywa kwa lengo la kukibabeba chama tawala, walisema.

"Maafisa wa tume wako chini ya serikali na wengi wao wameteuliwa na rais. Watendaji hawa si rahisi kuona aliyewateua anaanguka na hiyo inaweza kuwa ndiyo moja ya sababu za kufanya kazi kwa upendeleo," alisema Kabisa.
Aliendelea kueleza kuwa kumekuwa na tofauti ya idadi ya kura zilizojumulishwa vituoni na zilizokuwa zikitangazwa na Nec, jambo ambalo linachangia kuwanyima watu haki yao ya kupata viongozi waliowachagua.

Mjumbe wa TaCCEA, Hebron Mwakagendi alisema muungano huo umependekeza wakurugenzi watendaji kuondolewa kazi ya usimamizi wa uchaguzi kwa kuwa ni watumishi wa serikali na hivyo hawawezi kuwa huru na kutenda haki.
Alisema maofisa hao wa serikali kutumika kwenye uchaguzi imekuwa chanzo cha kushamili kwa vitendo vinavyokwamisha haki ya mpigakura.

"Pendekezo jingine ni kuwekwa hadharani kwa daftari la wapigakura ili kila mtu aweze kulipitia. Hii itapunguza usumbufu wa kutafuta majina wakati wa uchaguzi," alisema.

Kuhusu matumizi ya vifaa vya kisasa ambavyo maafisa wengi walionekana kushindwa kuvitumia, mjumbe huyo alisema TACCEA ilipendekeza wahusika kupatiwa mafunzo mapema ili kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia hiyo.
"Sambamba na hilo tume imetakiwa kuajiri wafanyakazi wake watakaoshiriki mafunzo mbalimbali, zikiwamo taratibu za uchaguzi ili kuondoa usumbufu uliojitokeza katika uchaguzi wa awamu hii," alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu wasimamizi walikuwa na uelewa mdogo na baadhi yao walilazimika kufundishwa wakiwa kazini.

Mjumbe huyo alieleza pia kuwa kitendo cha ujumlishaji kura kufanywa na watu wachache ni kasoro nyingine walioibaini katika uchunguzi wao.
"Tume inatakiwa kufanya majumuisho ya kura kwa uwazi kwa kushirikishi wadau mbalimbali zikiwamo asasi za kiraia badala ya kujifungia kama ilivyo sasa ili kuondoa matatizo ya kutoa kura zinazotofautiana na zile za vituoni," alisema.
Baadhi ya taasisi zinazounda muungano huo ni Leadership Forum, ForDIA, TANLAP, WiLDAF, SAHRiNGON, TAHURIFO, MPI, ACCORD, ZLSC, HAKIMADINI, LEAT na Hivos na Sida.
Chanzo: Mwananchi 05 Novemba, 2010
 
futikamba

futikamba

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2010
Messages
243
Likes
0
Points
33
futikamba

futikamba

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2010
243 0 33
Jamani, na kelele zote hizi bado tu wanaapishana?? Kweli dikteta ni dikteta tu. Lakini akae akiju kwamba uvumilivu wa watanzani umefika MWISHO. Asubirie tu kwa yatakayojiri. C wanajidai wanatetea Amani??
Na hiyo amani itadumishwa ikiwa wao watatoweka kwenye uso wa TZ na dunia hii. Yetu macho na masikio
 
Azimio Jipya

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
3,370
Likes
17
Points
135
Azimio Jipya

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
3,370 17 135
Hivi baada ya rais kuapishwa...kuna uwezakano wa kufanya chochote cha maana..!
 
MWANA WA UFALME

MWANA WA UFALME

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2010
Messages
578
Likes
0
Points
0
MWANA WA UFALME

MWANA WA UFALME

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2010
578 0 0
Kasoro ni nyingi na zinafanya zoezi zima kuwa null and void.
 
R

Rugemeleza

Verified Member
Joined
Oct 26, 2009
Messages
668
Likes
6
Points
35
R

Rugemeleza

Verified Member
Joined Oct 26, 2009
668 6 35
TACCEO: Uchaguzi ulikuwa huru, lakini haukuwa haki
Na Richard Makore
5th November 2010
TACCE.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Francis Kiwanga (aliyesimama) akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu ripoti ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita. Kwa mujibu wa TACCEO, uchaguzi mkuu huo ulikuwa huru lakini haukuwa wa haki.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Uangalizi wa Uchaguzi ulioundwa na vyama vya kiraia (TACCEO), Martina Kabisama (katikati) na Hebron Mwakagenda.(Picha: Tryphone Mweji).

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mtandao wa Asasi za Kiraia unaoundwa na mashirika 17 yasiyokuwa ya Serikali (TACCEO) umetoa ripoti yao na kusema kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ulikuwa huru lakini haukuwa wa haki kwa kuwa watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilitoa matokeo ya uongo kutokana na kutojua matumizi ya kompyuta kwa ajili kujumlishia kura.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kadhalika, ripoti hiyo imeeleza kuwa baadhi ya watumishi wa Nec hawakuwa na uelewa wa namna ya matumizi ya fomu mbalimbali walizopewa na pamoja na baadhi kuwasaidia wapiga kura wasiojiweza kuweka alama ya vyema kwa mgombea wanayemtaka wao.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akisoma ripoti yao kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa timu ya waangalizi iliyoundwa na TACCEO, Martina Kabisama, alisema kutokana na kuwepo kasoro nyingi kulichangia watumishi wa Nec kutoka matokeo yasiyo sahihi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbali na waandishi wa habari, maofisa wa Kituo cha Sheria na Hakiu za Binadamu LHRC pamoja na wajumbe kadhaa wa TACCEO walikuwepo katika mkutano huo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, alisema watumishi hao walitumia muda mrefu kutafuta majina ya wapiga kura hatua iliyodhihirisha kwamba wengi wao walikuwa hawajui kitu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alifafanua kuwa baadhi ya watumishi waliozungumza na waangalizi wa TACCEO walikiri kuwa walipata mafunzo kabla ya kufanyika kwa Uchagzui Mkuu na hivyo wengi walikuwa hawajajua nini walichokuwa wakikifanya.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kabisama alieleza kuwa baadhi ya vituo havikuwa na fomu namba 3A na 18 ambazo zilikuwa muhimu kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za matokeo hususani katika vituo vya kupigia kura vya Kimara ambapo kituo ha Mwananyamala karatasi za kupigia kura zilipelekwa jioni.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kutokana na kasoro hizo, TACCEO ilitoa mapendekezo manane yatakayosaidia kuboresha chaguzi zingine zijazo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mapendekezo hayo ni pamoja na kuitaka Nec kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura, kuifanyia marekebisho Nec ili kupata chombo huru kinachojitegemea, Daftari la wapiga kura lazima liwe wazi ili wananchi waweze kuliona na kutafuta majina yao wakati wote na Wakurugenzi wa Wilaya kutokuwa mawakala wa Nec kusimamia uchaguzi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, Mapendekezo mengine ya ni pamoja na kutaka wasimimizi wa uchaguzi wapatiwe mafunzo kuhusu matumizi ya Teknolijia ya Habari (ICT), Nec iache kukalia matokeo ili kuondoa vurugu zisizokuwa za lazima kwa jamii.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Pendekezo la mwisho walitaka mabadiliko ya sheria ili ijulikane muda wa kupiga kura na matokeo yake kutangazwa hadharani badala ya sasa ambapo wasimamizi wanaweza kuyakalia kwa zaidi ya siku mbili bila kuyatoa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Waangalizi wa uchaguzi wa ndani walioteuliwa na TACCEO walifikia 1744 ambapo walitawanywa katika mikoa, majimbo na kwenye vituo vya kupigia kura.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mtandao huo uliandaa utaratibu wakati wa uchagzui ambapo wananchi walikuwa na fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa waratibu wa kitaifa waliokuwa Dar es Salaam kupitia namba 15540 kwa mitandao ya Vodacom, Tigo, Zain na Zantel ili kutoa taarifa kwao juu ya mambo mbalimbali yaliyokuwa yanatokea katika vituo vya kupigia kura.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kati ya waangalizi hao, 270 walikuwa katika majimbo na kila mkoa ulikuwa na mratatibu mmoja ambaye alikuwa anaratibu shughuli zote za uangalizi na kutoa taarifa makao makuu ya mtandao huo yaliyokuwa jijini Dar es Salaam.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Asasi hizo za kiraia ni pamoja na Tamwa, SAHRINGON Tanzania, WLAC, TANLAP, WILDAF, Fordia, HakI Madini, MPI, ACCORD, ZLSC, PF, Tahurifo, YPC, LEAT na LHRC.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]TACCEO ilipata kibali cha kufanya kazi hiyo kutoka Nec ambapo lengo la uangalizi huo lilikuwa ni kuainisha mapungufu ambayo yangeweza kujitokeza siku ya uchaguzi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Maeneo yaliyoangaliwa na waangalizi hao ni pamoja na kujua kiwango cha wananchi kuelewa masuala ya uchaguzi, elimu ya uraia kwa wananchi, ushiriki wao katika uchaguzi, ushiriki wa wadau mbalimbali kama Nec, vyombo vya habari, vyombo vya usalama na asasi za kiraia zinavyoelimisha jamii.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mengine ni namna ambavyo sheria ya gharama za uchaguzi inavyozingatiwa pamoja na kanuni na taratibu za uchaguzi zinavyozingatiwa na wadu mbalimbali.[/FONT]
CHANZO: NIPASHE
 
YeshuaHaMelech

YeshuaHaMelech

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
2,624
Likes
4
Points
0
YeshuaHaMelech

YeshuaHaMelech

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
2,624 4 0
Sioni kama ni kasoro. It is my belief that it was planned and implemented, period!
 

Forum statistics

Threads 1,237,027
Members 475,398
Posts 29,276,017