Wasimamishwa kazi kwa tuhuma za kushabikia siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasimamishwa kazi kwa tuhuma za kushabikia siasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rugas, Jun 2, 2011.

 1. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Send to a friend Wednesday, 01 June 2011 21:09 0diggsdigg

  Tumaini Msowoya, Iringa
  HALMASHAURI ya Wilaya ya Makete, imeamua kuwasimamisha kazi watumishi wake watano kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya siasa kinyume cha kanuni za kudumu za utumishi wa umma.Kusimamishwa kwa watumishi hao, kumedaiwa kuwa ni hatua za serikali kuanza kuonyesha makali yake, katika kutimiza dhana ya kujivua gamba.

  Waliokumbwa na mkasa huo Barton Sinene wa Idara ya Mipango, Naumu Tweve wa Idara ya Maji na Clemence Sanga, ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bulongwa.

  Wengine ni Yusti Konga, Ofisa mtendaji wa Kata ya Mlondwe na Happy Mahenge ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji.Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Imelda Ishuza, alikiri kuhusu kusimamishwa kazi kwa watumishi hao watano.

  Alisema pamoja na kusimamishwa, pia wamepewa muda wa siku 14, kujieleza kwa maandishi kuhusu tuhuma zinazowakabili.
  Wafanyakazi hao wanatuhumiwa kufanya shughuli za kisiasa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana."Ni kweli kwamba tumewapa barua za kuwataka wajieleze kwa maandishi ndani ya siku 14 ambazo hata hivyo bado hazijaisha…Hawa wanatuhumiwa kujihusisha na mambo ya siasa kinyume na kanuni za kudumu za utumishi wa umma,"alisema mkurugenzi huyo.

  Alisema watumishi hao wamesimamishwa kwa mujibu wa kifungu cha 21 (f) cha sheria ya mwaka 2009, ya kanuni za kudumu za utumishi wa umma.Gerace alisema halmashauri imechukua uamuzi huo, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

  Alisema kuwa wamefanya hivyo baada ya CCM kulalamika kwamba watu hao walishiriki katika kampeni za uchaguzi, kinyume na kanuni za utumishi wa umma
  HILO NI MWANANCHI!
  KWELI HATA WALE WALIOIPIGIA CCM KAMPENI IWAPO TUTAWABAINI,NAO WATASIMAMISHWA?AU HUU NI UONEVU TU KWA KUSHABIKIA SIASA ZA UPINZANI?
   
Loading...