Wasilisha maoni yako hapa kuhusu kujitoa kwa star tv kwenye star times na haki zako za msingi

  • Thread starter mjasiriamali mdogo
  • Start date
mjasiriamali mdogo

mjasiriamali mdogo

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Messages
231
Points
225
mjasiriamali mdogo

mjasiriamali mdogo

JF-Expert Member
Joined Mar 15, 2013
231 225
TCRA WANAJIBU MASWALI MBALIMBALI NA KUTOA UFAFANUZI WA MAMBO MENGI PAMOJA NA HAKI ZAKO ZA MSINGI kama za visimbuzi, gharama za simu na mengineyo. Haya yote utayapata baada ya kulike page yao fb inaitwa TANZANIA COMMUNICATION REGULATORY AUTHORITY hapa wanapokeo kero pamoja na maoni.
 
WA-UKENYENGE

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Messages
2,906
Points
1,500
WA-UKENYENGE

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2011
2,906 1,500
TCRA wanafanya nini watu tunaibiwa kila kukicha na makampuni ya simu haswaaa unakuta mteja wa kampuni fulani unapokea ujumbe wa tangazo ukiusoma tu tayari unakatwa salio, huu siyo uonevu ila ni wizi.
 
WA-UKENYENGE

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Messages
2,906
Points
1,500
WA-UKENYENGE

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2011
2,906 1,500
TCRA mnafanya nini ukienda Loliondo unakutana na ujumbe kwenye simu kuwa: "karibu katika falme za kiarabu" TCRA mtujibu na kutuweka sawa katika hili maana ukijiloga ukapiga simu eneo hilo, tayari unaingizwa katika roaming with high charging rates.
 
WA-UKENYENGE

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2011
Messages
2,906
Points
1,500
WA-UKENYENGE

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2011
2,906 1,500
TCRA pamoja na changamoto mlizonazo, lakini bado hamtundei haki watanzania katika sekta ya mawasiliano. Mfano: utakuta kituo cha matangazo ya radio au TV kinaenda kinyume na maadili ya kitanzania, ina maana hamuoni hayo jamani, litendeeni taifa hili haki kwani watoto wetu wanapata madhara makubwa kutokana na baadhi ya vipindi visivyokuwa na maadili mazuri kuonyeshwa aidha mapema wakati watoto wakiwa bado wangali macho.
 
bornagain

bornagain

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
3,385
Points
1,225
bornagain

bornagain

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
3,385 1,225
Hakuna maoni tena hapo kwa sababu Tanzania imeshakuwa nchi ya ving'amuzi kwa taarifa yako.The only thing we face is lack of centralization
 
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
7,747
Points
2,000
Pancras Suday

Pancras Suday

Verified Member
Joined Jun 24, 2011
7,747 2,000
Hakuna maoni tena hapo kwa sababu Tanzania imeshakuwa nchi ya ving'amuzi kwa taarifa yako.The only thing we face is lack of centralization
umenena mkuu
 
TCRA

TCRA

Verified Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
94
Points
95
TCRA

TCRA

Verified Member
Joined Aug 14, 2012
94 95
Mamlaka ya Mawasiliano itatoa Tamko na Agizo la Kidhibiti saa saba Kalili mchana Kwa saa za Afrika ya Mashariki kuhusu "kujitoa Kwa Star TV" katika platform ya dijitali katika Star Media Tanzania Limited, kulingana na Sheria ya EPOCA na Kanuni zake.

Fuatilia JF baada ya saa saba Mchana.
 
TCRA

TCRA

Verified Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
94
Points
95
TCRA

TCRA

Verified Member
Joined Aug 14, 2012
94 95
Sio kweli kuwa Loliondo kuna Roaming Messages. Uchunguzi uliofanyika ulithibitisha kuwa huo ulikuwa ulushawapa wakati Wa mawasilisho ya Bajeti ya Wizara ya Utalii. Hakuna ukweli kuhusu hilo Jambo na uchunguzi uliofanyika Kwa mwezi mzima.
 
figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,519
Points
2,000
figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,519 2,000
mengi angewagawia bure ving'amuzi vyake ili watu waendelee kupata habari coz watafanya watu wanunue ving'amuzi upya. mia
 
M

musubati

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Messages
218
Points
195
M

musubati

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2013
218 195
Mtwara hatupati haki ya kuona TBC je hiyo ni sahihi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Messages
5,016
Points
2,000
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2009
5,016 2,000
Mamlaka ya Mawasiliano itatoa Tamko na Agizo la Kidhibiti saa saba Kalili mchana Kwa saa za Afrika ya Mashariki kuhusu "kujitoa Kwa Star TV" katika platform ya dijitali katika Star Media Tanzania Limited, kulingana na Sheria ya EPOCA na Kanuni zake.

Fuatilia JF baada ya saa saba Mchana.
Tunashukuru kwa taarifa, hivi sasa ni saa 2:15PM, tunaopmba update ya kilichojiri maana nilikuwa nikanunue kingamuzi cha Continetal Leo hii.
 
Rutunga M

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Messages
1,687
Points
1,500
Rutunga M

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2009
1,687 1,500
BAADA ya Televisheni ya Star TV kutangaza kujitoa kurusha matangazo yao kupitia kingamuzi cha Star Times, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema sheria na leseni ya huduma, inazuia kuchukua hatua hiyo.

Hata hivyo, TCRA imesema inafanya uchunguzi na leo itakutana na uongozi wa Star TV na Star Times, kuzungumzia suala hilo ili hatua za udhibiti, zichukuliwe kuwezesha wananchi kupata haki ya msingi ya kupata matangazo ya kitaifa kupitia televisheni hiyo.


Star TV walitangaza kutoonekana kupitia Star Times siku chache zilizopita. Uchunguzi wetu umebaini kuwa, jana waliwasilisha barua ya hatua hiyo kwa kampuni ya Star Times kupitia mwanasheria wa kampuni yao.


Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy aliliambia HabariLeo jana kuwa na wao wamesikia taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari Lakini, alisema Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, haitoi fursa kwa watu wenye televisheni kujitoa ama kujiweka kwenye ving’amuzi watakavyo.


“Kwa ujumla chaneli zile tano za kitaifa, zinapaswa kuonekana bure kwenye ving’amuzi vyote, nasi tumesikia habari hizi na lazima tufanye uchunguzi, lakini pande zote mbili pamoja na sheria, pia wanafungwa na mkataba wa huduma kwa jamii na matakwa ya leseni,” alisema Mungi na kuongeza:


“Sheria inawataka wawe na makubaliano, huwezi kusema mimi najitoa, leseni ina matakwa yake lazima yafuatwe. Lakini kesho (leo) tutawaita kujua kilichotokea ni nini na hatua zaidi zitachukuliwa baada ya hapo”.


Aliwahakikishia wananchi ni haki yao kupata matangazo kupitia televisheni ya Star TV, hata bila kulipia ving’amuzi, kama ilivyo kwa televisheni nyingine nne za ITV, TBC, Channel 10 na EATV.


Msaidizi wa Meneja wa Star Times, Hellen Elisa alithibitisha kujitoa kwa Star TV. Alieleza ni kweli walipokea barua mbili juzi, zikieleza kuhusu hatua yao hiyo kwamba wamejitoa kwa matakwa yao.“Walituletea barua jana (juzi) kupitia mwanasheria wao wa kampuni, wao ni wamiliki wa chaneli, na sisi tunahusika kurusha matangazo, jambo lolote kama hili likitokea lazima kwanza kutii sheria, tumewasiliana na TCRA na wakubwa wetu wa kazi wametueleza kuwa wanalishughulikia kwa karibu,” alisema Elisa.


Kwa upande wake, Msimamizi wa masuala ya Ving’amuzi wa Sahara Media Group, wamiliki wa Star TV, Steve Diallo alipoulizwa kwa simu kuhusu kujitoa kwao Star Times, alisema yeye si Msemaji na kumtaka mwandishi kuwasiliana na watu wengine.Miezi kadhaa iliyopita, Clouds TV nayo ilijitoa, lakini ikarejea tena. Jana, Mkurugenzi wa Utafiti wa Redio Clouds FM, Ruge Mutahaba alisema sheria inawabana wamiliki wa televisheni za kijamii kujitoa na wanapaswa kuonekana katika ving’amuzi vyote.

chanzo:habarileo
 

Forum statistics

Threads 1,326,378
Members 509,496
Posts 32,219,781
Top