Wasikilize makamanda wa M4C vs V4C Live on Wapo Radio

by default

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
839
215
Leo Jumatano tar. 03 OCT 2012 saa nne asubuhi katika kipindi cha meza ya busara, Wapo Radio fm 98.00 DSM au sikiliza http://www.ustream.tv/channel/wapo-radio-fm Kipindi cha meza ya busara utawasikia Makamanda wa Chadema wakifafanua juu ya M4C na Tuhuma za Kukifanyia Vurugu Chama Cha CUF.

Nayo Majembe ya CUF, yatakuwa yakifafanua juu ya V4C ''Dira ya Mabadiliko' na kujibu tuhuma za kutumiwa na CCM, kuisambaratisha chadema.

Usikose!
 
Leo jumatano tar. 03 OCT 2012 saa nne asubuhi katika kipindi cha meza ya busara, wapo radio fm 98.00 DSM au sikiliza www.gosplekitaa .blogspot.com Kipindi cha meza ya busara utawasikia Makamanda wa Chadema wa kifafanua juu ya M4C na Tuhuma za Kukifanyia Vurugu Chama Cha CUF. Nayo Majembe ya CUF yakifafanua juu ya V4C'''Dira ya Mabadiliko'''na kujibu tuhuma za kutumiwa na CCM, kuisambaratisha chadema.usikoseee

Je atakayewakilisha V4C (Vote4Chadema) ni Mtatiro au ni nani?
 
Thomas malima naibu ktbu mtendaji vijana wa cuf na Tumaini makene wa cdm ndio wapo ndani.
 
Wakuu tunaomba muwe mnatupa updates za ukweli kama Mungi alivyofanya jana!
Wengi tupo mbali na Dar halafu tunatumia simu za mchina.
 
Jamaa wa cuf wanasema cdm wameiga hadi rangi za bendere,kauli ya people power ilikuwa yao,anasema cuf ndio imeilea cdm mwaka 95,vision for change cdm wamecopy na kuwa movement 4 change.sera ya majimbo ni ya cuf na serikali 3
 
jamaa wa cuf anasema chadema wanawaiga wao kila kitu kuanzia m4c,rangi za bendera,suala la serikali tatu,katiba nk
 
Jembe Makene anashusha point za nguvu hapa.....CUF wameleta V4C kuanzisha ligi na CDM.
 
jamaa wa cuf anawaponda chadema,anasema Arusha sio ngome yao....anasema ata CCM wanamajimbo na madiwani arusha..anaifagilia ccm na kuisahau cuf yake.
 
kuna mwananchi kapiga anauliza maalim seif anaingia kwenye kamati kuu ya cuf kama kiongozi wa serikali au kiongozi wa upinzani???

mwingine anauliza cuf mbona siku izi hawapiganii haki sawa kwa wote uko zanzibar au kila kitu kiko sawa siku izi???

mwingine anatoa masikitiko yake jinsi kiongozi wa cuf anavyotoa kashfa kwa chadema as if yuko upande wa utawala..
 
tena makamanda wa chadema mkuu maana hata ccm wanaitana makamanda siku hizi!
kweli nimesikia magamba wanaitana kamanda!nilishangaa.eti mmoja kapata mtoto sas mwenzie anampomgeza na kumtabilia mtoto yule atakuwa kamanda wa ukweli!
 
duh inafurahisha sana wadau....!!yani watu wanavyomshambulia jamaa wa cuf kweli siku izi udanganyi mtu.

Makene alichomuweza yeye kwenye maelezo yake hakuwa anaizungumzia Cuf bali ali base kwenye sera na M4C..jamaa wa cuf alichokosea ni kuiponda chadema mwanzo mwisho sasa haeleweki yeye ni mtawala au mpinzani.
 
Swali limeulzwa kwa nini Cuf wamejkita kuiponda Cdm kulko kuwasemea wananchi&kunadi sera zao.
 
uyu jamaa wa cuf sijui wamemuokota wapi!!awezi kabisa kujieleza.

ameulizwa mafanikio ya V4C....anasema mafanikio yake ni mlinzi wa Lema kujiunga na CUF.
 
Back
Top Bottom