Wasifu Wa Marehemu Ditopile

Nadhani mwandishi anatumia wasifu wa marehemu kutetea shutuma za mauaji. Lakini mantiki anayo tumia imepinda, na analeta uchambuzi wa mambo ya kichawi, ikiwa ni pamoja na kutumia sana assumptions.
Ditopile- The saint or a sinner?

…Na kwamba kule kupangiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, zilikuwa njama za mafisadi kuhakikisha anakaa mbali na Rais Jakaya Kikwete, ili asiweze kumpatia habari za haraka za wanaoiba fedha za Serikali.

Nani alimpangia kazi Tabora? Kuna mtu kweli anaweza kumshawishi Kikwete asimpe swaiba wake kazi anayotaka yeye Kikwete?

…Hawakumbuki kumwona Dito akiwa na hasira kiasi hicho katika maisha yake. Wengi wanaamini alirogwa na mafisadi! Alitupiwa juju, akili yake ikabadilika! Wenye imani hizi za kurogwa wanalishikia hili bango na wanamtaja kabisa mlengwa! Maana, kuna habari za mitaani kwamba Dito, alipowekwa gerezani, kuna mafisadi walifanya sherehe. Na walikuwa wakifanya kila njama ili aendelee kubaki ndani.

Sasa hapa alipoleta nadharia za 'uwanga' ndio alipoanza kuniacha !

Katika karne ya leo kutetea mtuhumiwa wa mauaji kwa vile kuna watu wanadhani amepigwa kipapai ni kudata. Samahani, lakini nashindwa kujizuia. Dunia sasa hivi inakuna kichwa kujiuliza tutatumia vipi Sayansi na Teknolojia kutafuta vyanzo vipya vya mali asili, na nishati ambavyo vimepungua duniani, vinakwisha. Uchawi hauna nafasi hapa. Mwaka jana nilikuwa kwetu kijijini nikaona watu wanalalamika siku hizi wananunua mpka kuni. Huko Bushi, intiria kabisa, misitu imekwisha! (Bahati mbaya kila siku Wabongo tunaimba ooh, tuna utajiri wa asili na ule na huu. Hii hadithi itatutokea puani siku za mbele). Dunia inajiuliza tutapigana vipi na magonjwa yasio na tiba - mikorogo ya madawa makali ya Ukimwi (Highly Active Antiretroviral Treatment) siku hizi nayo virusi wameanza kujenga sugu kwayo. Tutafanyaje. Uchawi hauna nafasi hapa. Ungekuwa na nafasi Waafrika tusingekuwa tunaongoza kwa vifo kwa sababu tuna wachawi wengi kwa hekta ya mraba kuliko jehanamu kwenyewe wanga wanakozalishwa. Kwa hiyo, hizo nadharia za Ditopile kulogwa, nasema, tafadhali, tafadhali!

…Wengi tulifikiri alifanya kitendo kile cha kumfyatulia Hassan Mbonde risasi kwa kiburi cha kuwa karibu na Rais Jakaya Kikwete na kwamba labda hakujuta kwa kitendo hicho. Lakini ukweli nilioupata kwa watu waliokaribu naye ni kwamba kitendo hicho kilimtesa sana na hakukikubali wala kukipokea rohoni mwake hadi siku ya kufa kwake. Hakuamini kama yeye ndiye aliyetenda kitendo hicho. Ilimtesa sana!

Unawezaje kujuta halafu hapo hapo huamini wewe ndio ulifanya? Kujuta katika dini, katika sheria za bin Adam, na katika maisha ya kila siku ni kusikitika, kujilaumu na kile unacho jua umekifanya. Nadhani ‘denial’ sio sawasawa na ‘remorse.’

Na hata kama alisikitika, hiyo haina maana hakukusudia kuua. Masikitiko yanaweza kuonyesha kujilaumu kwa kile unacho jua umekifanya!

Mungu amlaze mahali pema peponi, kwa vile yeye ndiye mwenye kupima, tumwachie yote! Ipo siku atawafichua wabaya wa Marehemu Ukiwaona (Usiwaulize) Ramadhani Mwishehe Ditopile wa Mzuzuri.

Tumwachie yote Mungu, ni lugha ya kuto kuwa na upande. Lakini ukisoma katikati ya mistari, anamtetea Ditopile kiujanja ujanja.

Binafsi, namshukuru Ditopile kwa mchango wake kwa nchi yetu. Siwezi kufanya robo ya aliyo yafanya kama mtumishi. Lakini tusitetee shutuma za mauaji kwa sababu eti yeye mwenyewe anaamini hakufanya, kwa sababu Tanzia zimesema zimemchora vizuri. Tanzia maana yake sifa za marehemu!

Unajua ukisema kitendo alichoshutumiwa kukifanya ni kibaya hii haitapunguza mema mengine aliyoyafanya kwa Taifa. Kwa hiyo, haina haja ya kutetea alichofanya ili tujue kwamba alikuwa kiongozi mzuri. Yote mema na uadiifu wake naukubali, lakini tusitetee maovu kwa sababu yeye mwenyewe 'alikataa moyoni,' au kwa sababu Tanzia zimesema. Tanzia maana yake sifa za marehemu. Waandishi hao hao siku Ditopile alipo ua walikosoa. Na mwisho uchambuzi wa mambo ya kishirikina umeniacha hoi, kusema machache.

Ahsante.
 
Wataongea mengi mazuri au mabaya kuhusu huyu marehemu,Tumwachie Mungu ambaye tayari ameshamweka mahali pake anapostahili.
 
Watanzania, sote tunajua kifo, hatuna haja ya kukumbuka yaliyotendwa na Brother Dito, kaka yetu alikuwa mtu wa watu siku zote, nadhani jamaa wamempiga ndonga ili afanye yasiyo, brother siku zote alikuwa mtu wa kuchekesha, laa !!!! Dito lala baba !!! tuko nyuma yako kaka.
 
ebwana hata mie ninaunga mkono kwamba sio uungwana kumhukum maana kashafika mbele ya haki...aliyoyatenda duniani ameyaacha na sasa atapata stahili yake mbele ya muumba wake
 
ebwana hata mie ninaunga mkono kwamba sio uungwana kumhukum maana kashafika mbele ya haki...aliyoyatenda duniani ameyaacha na sasa atapata stahili yake mbele ya muumba wake

Ni kweli, tena Watanzania tuna utamaduni wa kuto kuwasema marehemu vibaya. Tuseme mazuri aliyo fanya kama binadamu na kama kiongozi.

Lakini unapoanza kutetea matendo yake fulani ambayo yana utata, hapo unafungua milango kwa mashitaka. Kumbuka, sio haki kwa wale wafiwa wa yule marehemu mwingine tukikaa hapa tunajaribu kumtetea Ditopile kama mwandishi wa ile makala alivyofanya - kwamba alijuta akiwa jela kwa hiyo hakukusudia, au alichezewa na wachawi!

Utamaduni wa kutosema mabaya ya marehemu maana yake tatasema mazuri mabaya tutayaacha kama yalivyo. Haina maana tutaanza kutetea mabaya. Ahsante.
 
It is one thing to "not speak ill of the dead" and quite another to sing songs of hypocrisy disguised as the civilization of "not speaking ill of the dead.

Hivi mtu akiandikiwa eulogy iliyo balanced kuna tatizo gani? Msi focus kwenye mabaya, elezeni mazuri with sanity and not this hypocrisy ya kumuita muuaji aliyemtwanga mtu risasi kwa sababu ya a traffic nuisance kwamba ni mtu mzuri sana ambaye ukigombana naye ataenda to any length kutafuta usuluhisho, mbona hakutafuta usuluhisho na yule kijana wa daladala.

I am sick of this malady of hipocrisy masquerading as civilized tradition.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom