Wasifu wa Julius Nyerere: Hotuba ya Kuaga Ukumbi wa Diamond Jubilee 1985

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,861
30,213
WASIFU WA JULIUS NYERERE: HOTUBA KWA WAZEE WA DAR ES SALAAM KUWAAGA WATANZANIA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE NOVEMBA 5 MWAKA,1985

"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania.

Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli.

Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma.

Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua.

Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa.

Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama.

Januari nikarudi Dar es Salaam.

Nikaanza kazi.

Nikataka kujua habari za African Association.

Mzee Mwangosi anakumbuka.

Yeye ndiye aliniambia habari za African Association.

Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima.

Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo.

Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo.

Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya?

Kipo chama.

Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

Hivyo ndivyo tulivyofanya.

Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere.

Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo) nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora.

Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association.

Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA.

Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam.

Nikauliza nani wanaongoza TAA?Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes.

Sasa ni marehemu.
Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano).

Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo.

Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation).

Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari.

Kufika Aprili, TAA ikafufuka.

Tukafanya mkutano hapo Arnautoglo.

Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee.

Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni.

Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA.

Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes.

Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi.

Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya.
Wazee wakaniamini upesi sana.

Tukawa na uhusiano mkubwa sana.

Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abbas Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu!

Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU.

Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa!

Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka.

Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru!

Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi.

Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu.

Huko wazee walinipokea na kunielewa.
Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima.

Nilikwenda Mbeya.

Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini?

Nikawaambia natafuta uhuru.

Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari.

Tulifanya mkutano wa makini kweli.

Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru?

Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

Tulielezana.

Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi.

Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile.

Sisi siyo koloni lao.
Wamepewa dhamana tu.

Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu.

Tuwaseme tu!

Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana?

Nikasema inawezekana.

Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo.

Hilo lilikuwa la kwanza.

Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana.

Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo.

Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza.

Hawakuogopa kufukuzwa kazi.
Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikwua mfanyabiashara na kaidi kidogo.

Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara.

Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja.

Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.

Imani hujenga imani.

Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi.

Magumu sana.

Wanasema ngoma ya watoto haikeshi!

Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani.
Tangu awali kabisa.

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam).

Akasema: Leo wazee wanakutaka.
Wapi?

Kwa Mzee Jumbe Tambaza.
Wanakutaka usiku.

Nikasema haya, nitakuja.
Nikaenda.

Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua.

Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu.
Wakaniombea dua za ubani.

Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao.

Basi wakanitoa nje.
Tukatoka.

Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi.
Wamechimba shimo.

Wakaniambia simama.
Nikasimama.

Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo).

Ndipo nikaambiwa: Tambuka!
Nikavuka lile shimo.

Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu.

Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika).

Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao.

Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama.

Twaining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo.

Kwenye makaburi kule!

Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa.

Tukasema tuwasaidie.
Tuwasaidie vipi?

Tukasema tufunge.
Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo.

Tufunge! Tukafunga.
Hakuna kula.

Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko.

Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu).

Hapa ndipo tulikuwa tumefikia.
Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro?

Akajibu: Kwa nini unataka Aspro?

Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli.
Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu.
Tukafuturu vizuri.

Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro?

Nikajibu kichwa sasa hakiumi.
Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana.

Tulishirikiana sana na wazee.
 
Kuna mazuri ya J.kikwete agharabu siyaoni katika utawala huu, kukutana na wazee wa dar es salaam Ni shukrani ya uhuru iliyopaswa kuenziwa siku zote, siku hizi tunadharau dharau tuu labda kwa vile uhuru hauna maana kwetu.

Wakati wa J.Kikwete wazee wengi walipewa tuzo kwa kumbukumbu ambazo hata taifa tulizisahau, Kuna ile medali ya heshima sijaiona kwa mtawala huyu labda mnikumbushe.

Hata kina Shamsi vuhai nahodha hawakuwa wa kusahaulika mapema hivi
 
Natamani uendelee na hotuba tamu hii Ni kama namuona Mwalimu?
Silasuga...
Hii hotuba huko mbele Mwalimu anasema kuwa yeye amerekebisha upogo baina ya Waislam na Wakristo katika kutawala nchi kiasi kwamba hajui kwa kutazama majina kama huyu ni Muislam au ni Mkristo.

Prof. Njozi katika kitabu chake, "Mwenbechai "Killings.. ."(2002) ambacho kimepigwa marufuku Tanzania katoa maelezo ya kufikirisha sana kuhusu kipande hiki cha hotuba ya Mwalimu.

Lakini katika hotuba yenyewe kila ninapoisoma nakuwa na maswali mengi sana kiasi huwa najiuliza hivi Abdul Sykes alipata kumweleza Nyerere historia yake yeye mwenyewe binafsi na historia ya TAA kabla hawajaunda TANU 1954?

Najiuliza swali hili kwa pale Nyerere anaposema TAA ilikuwa "inasinziasinzia," yeye ndiyo akaiamsha mwaka wa 1953 alipochaguliwa kuwa President.

Ukiingia katika Nyaraka za Sykes utakutana na mambo makubwa yaliyofanywa na TAA kuanzia 1950 wakati wa uongozi wa Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes.

Kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyopeleka mapendekezo ya katiba kwa Gavana Edward Twining.

TAA katika mapendekezo yake muhimu walilopendekeza ni kuchaguliwa kwa kura kwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria badala ya kuteuliwa achilia mbali kuundwa kwa Kamati Ndogo ya Siasa ndani ya TAA.

Hilo la kwanza.

Pili namna Abdul Sykes alivyomwingiza rafiki yake, Wakili Earle Seaton ndani ya TAA kukishauri chama vipi waliendee suala la Tanganyika kama nchi chini ya udhamini UNO kuanzia 1950 na jinsi alivyoshirikiana na Seaton na Japhet Kirilo akiwa kiongozi wa Meru Citizens Union katika Meru Land Case.

Haya matatizo ya ardhi ya Wameru yalimalizikia kwa Kirilo kuhutubia UNO 1952 Seaton akiwa mkalimani wake.

Tatu Abdul Sykes alivyofanya mkutano wa siri na Jomo Kenyatta na viongozi wenzake wa KAU Nairobi mwaka wa 1950.

Waingereza walitaka kumnyima Kirilo pasi ya kusafiria na Abdul Sykes alikuja juu hadi serikali ikampatia Kirilo pasi na kumwezesha kusafiri kwenda New York.

Nne kulikuwa na juhudi kuanzia mwaka wa 1950 za Abdul Sykes kutaka kuunda TANU Chief David Kidaha Makwaia wa Siha akiwa Territorial President.

Mazungumzo baina ya Abdul Sykes na Chief Kidaha yalikwenda kwa kiasi cha miaka miwili lakini hayakuwa na mafanikio.

Mwalimu kaeleza kuwa alichaguliwa kuongoza TAA katika mkutano Ukumbi wa Arnautoglo mwaka wa 1953.

Ukweli ni kuwa uamuzi wa yeye kukabidhiwa uongozi wa TAA ulifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe na waliofanya uamuzi huo ni Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Uchaguzi wa Arnautoglo ulikuwa ni kukamilisha taratibu za demokrasia.

Bahati mbaya Mwalimu hakueleza aligombea na nani nafasi ya urais wa TAA.

Nyerere aligombea nafasi ile na Abdul Sykes.

Nyerere akachaguliwa rais na Abdul Sykes makamu wake.

Inaelekea Mwalimu hakuwa anayajua haya ndiyo maana akasema TAA ilikuwa usingizini.

Yapo ya katiba, safari zake majimboni baada ya kuundwa TANU ambazo Mwalimu anazichanganya si kuwa alianza kwenda wapi na alizungumza na nani bali hata maudhui ya mazungumzo anayaweka sipo.

Lakini kuna suala la kupokewa ambalo yeye kaweka umuhimu mkubwa kwa wazee ambao kwa bahati mbaya hawajulikani kwani hakuwataja majina.

Nyerere hakupokewa na wazee Nyerere alipokewa na Abdul Sykes 1952 na aliishi nyumbani kwa Abdul Sykes 1955 alipoacha kazi na mipango yote ya TANU siku za mwanzo ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul.

Hii ndiyo sababu kadi ya Abdul Sykes ya TANU ni no. 3, Ally Sykes no. 2 na ya Rais wa TANU Julius Nyerere ni card no. 1.

Wazee walimjua Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes kwa maana ya Baraza la Wazee wa TANU baadae baada ya TANU imekwishaundwa na sasa mambo yako wazi hadharani si ya kujifichaficha tena.

Siwezi kueleza yote lakini haya niliyoeleza yanatoa picha ya mambo yalivyokuwa wakati ule kuelekea kuundwa kwa TANU na siku zake za mwanzo.
 
Silasuga...
Hii hotuba huko mbele Mwalimu anasema kuwa yeye amerekebisha upogo baina ya Waislam na Wakristo katika kutawala nchi kiasi kwamba hajui kwa kutazama majina kama huyu ni Muislam au ni Mkristo.

Prof. Njozi katika kitabu chake, "Mwenbechai "Killings.. ."(2002) ambacho kimepigwa marufuku Tanzanis katoa maelezo ya kufikirisha sana kuhusu kipande hiki cha hotuba ya Mwalimu.

Hii ndiyo sababu kadi ya Abdul Sykes ya TANU ni no. 3, Ally Sykes no. 2 na ya Rais wa TANU ni no. 1.

Wazee walimjua Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes kwa maana ya Baraza la Wazee wa TANU baadae baada ya TANU imekwishaundwa na sasa mambo yako wazi hadharani si ya kujifichaficha tena.

Siwezi kueleza yote lakini haya niliyoeleza yanatoa picha ya mambo yalivyokuwa wakati ule kuelekea kuundwa kwa TANU na siku zake za mwanzo.
 
Nashukuru Nyerere baada ya uhuru hakuwatupa hawa wazee, aliwajali kwa hali na mali, wale wachache wasaliti ndio aliwashughulikia.
 
Nafikiri nyerere aliposema TAA ilikuwa inasinzia sinzia alimaanisha mambo yalikuwa hapelekwi kisomi na ukichukulia yeye alikuwa ametoka huko kwa mabeberu.
 
Laki...
Hii ni habari ningependa sana kuijua.
Tafadhali hebu tueleze historia hii tafadhali.
Baraza la wazee wa TANU liliendelea kuheshimiwa na Nyerere hata baada ya uhuru. kwenye masuala nyeti Nyerere alikuwa hawezi kutoa maamuzi mpaka awaulize wazee wa TANU, hata vita vya Kagera alizungumza na wazee kwanza, huoni kwamba aliwathamini sana wazee?
 
Baraza la Wazee wa TANU lilivunjwa mwaka wa 1963 kwa kuchanganya dini na siasa au Uislam na siasa.

Hili baraza lilikuwa na wajumbe 120 Waislam watupu.
 
Mohamed Said asante kwa historia nzuri, umegusia swala la Japhet Kirilo ningependa kufahamu ikiwa ni kweli Nyerere alitaka kumchezea rafu ili asiende kuhutubia UNO au ni uzushi wa watu?
 
Silasuga...
Hii hotuba huko mbele Mwalimu anasema kuwa yeye amerekebisha upogo baina ya Waislam na Wakristo katika kutawala nchi kiasi kwamba hajui kwa kutazama majina kama huyu ni Muislam au ni Mkristo.

Prof. Njozi katika kitabu chake, "Mwenbechai "Killings.. ."(2002) ambacho kimepigwa marufuku Tanzanis katoa maelezo ya kufikirisha sana kuhusu kipande hiki cha hotuba ya Mwalimu.

Lakini katika hotuba yenyewe kila ninapoisoma nakuwa na maswali mengi sana kiasi huwa najiuliza hivi Abdul Sykes alipata kumweleza Nyerere historia yake yeye mwenyewe binafsi na historia ya TAA kabla hawajaunda TANU 1954?

Najiuliza swali hili kwa pale Nyerere anaposema TAA ilikuwa "inasinziasinzia," yeye ndiyo akaiamsha mwaka wa 1953 alipochaguliwa kuwa President.

Ukiingia katika Nyaraka za Sykes utakutana na mambo makubwa yaliyofanywa na TAA kuanzia 1950 wakati wa uongozi wa Dr. Kyaruzi na Abdul Sykes.

Kulikuwa na TAA Political Subcommittee iliyopeleka mapendekezo ya katiba kwa Gavana Edward Twining.

TAA katika mapendekezo yake muhimu walilopendekeza ni kuchaguliwa kwa kura kwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria badala ya kuteuliwa achilia mbali kuundwa kwa Kamati Ndogo ya Siasa ndani ya TAA.

Hilo la kwanza.

Pili namna Abdul Sykes alivyomwingiza rafiki yake, Wakili Earle Seaton ndani ya TAA kukishauri chama vipi waliendee suala la Tanganyika kama nchi chini ya udhamini UNO kuanzia 1950 na jinsi alivyoshirikiana na Seaton na Japhet Kirilo akiwa kiongozi wa Meru Citizens Union katika Meru Land Case.

Haya matatizo ya ardhi ya Wameru yalimalizikia kwa Kirilo kuhutubia UNO 1952 Seaton akiwa mkalimani wake.

Tatu Abdul Sykes alivyofanya mkutano wa siri na Jomo Kenyatta na viongozi wenzake wa KAU Nairobi mwaka wa 1950.

Waingereza walitaka kumnyima Kirilo pasi ya kusafiria na Abdul Sykes alikuja juu hadi serikali ikampatia Kirilo pasi na kumwezesha kusafiri kwenda New York.

Nne kulikuwa na juhudi kuanzia mwaka wa 1950 za Abdul Sykes kutaka kuunda TANU Chief David Kidaha Makwaia wa Siha akiwa Territorial President.

Mazungumzo baina ya Abdul Sykes na Chief Kidaha yalikwenda kwa kiasi cha miaka miwili lakini hayakuwa na mafanikio.

Mwalimu kaeleza kuwa alichaguliwa kuongoza TAA katika mkutano Ukumbi wa Arnautoglo mwaka wa 1953.

Ukweli ni kuwa uamuzi wa yeye kukabidhiwa uongozi wa TAA ulifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio Ukerewe na waliofanya uamuzi huo ni Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Uchaguzi wa Arnautoglo ulikuwa ni kukamilisha taratibu za demokrasia.

Bahati mbaya Mwalimu hakueleza aligombea na nani nafasi ya urais wa TAA.

Nyerere aligombea nafasi ile na Abdul Sykes.

Nyerere akachaguliwa rais na Abdul Sykes makamu wake.

Inaelekea Mwalimu hakuwa anayajua haya ndiyo maana akasema TAA ilikuwa usingizini.

Yapo ya katiba, safari zake majimboni baada ya kuundwa TANU ambazo Mwalimu anazichanganya si kuwa alianza kwenda wapi na alizungumza na nani bali hata maudhui ya mazungumzo anayaweka sipo.

Lakini kuna suala la kupokewa ambalo yeye kaweka umuhimu mkubwa kwa wazee ambao kwa bahati mbaya hawajulikani kwani hakuwataja majina.

Nyerere hakupokewa na wazee Nyerere alipokewa na Abdul Sykes 1952 na aliishi nyumbani kwa Abdul Sykes 1955 alipoacha kazi na mipango yote ya TANU siku za mwanzo ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul.

Hii ndiyo sababu kadi ya Abdul Sykes ya TANU ni no. 3, Ally Sykes no. 2 na ya Rais wa TANU Julius Nyerere ni card no. 1.

Wazee walimjua Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes kwa maana ya Baraza la Wazee wa TANU baadae baada ya TANU imekwishaundwa na sasa mambo yako wazi hadharani si ya kujifichaficha tena.

Siwezi kueleza yote lakini haya niliyoeleza yanatoa picha ya mambo yalivyokuwa wakati ule kuelekea kuundwa kwa TANU na siku zake za mwanzo.
nimekusoma shehe.

ulichoandika hapo juu ni sawia kabisa na hutba ya Mwalimu, sema umeongezea details ambazo katika speech zingeweza kuwa redundant na kurefusha speech ya Mwalimu unnecessarily.
 
M...
Redundant historia ya Abdul Sykes na Nyerere?

Kama huijui historia ya udugu wao hutoshangaa lakini ukiijua utakuwa kama mimi.

Ndiyo najiuliza hivi Abdul hakupata kumweleza Nyerere hata historia ya baba yake katika TAA?
 
Back
Top Bottom