Wasifu,Picha na Tabia za warembo hawa wa JF hadharani; Lara 1.,Kasinde na Miss. Chagga-Dalalitz

dalalitz

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
2,749
2,000
Hisia inaweza ikajenga Picha.
Picha inaleta Sura/Taswira.
Sura/Taswira inakupa mfanano ambao kwa mbaali kama si sana ikawa na uhalisia wa Kitu au Mtu na pengine kupitia Sura hiyo tunaweza kujaribu kujenga uelekeo wa tabia za Mtu au Kitu hicho.

Huwa nafuatilia kwa ukaribu michango mbalimbali ya wadau bila ya kubagua.
Lakini, Kwa ukaribu nimekuwa nikishikwa zaidi na michango ya wachache ambao misimamo ya hoja zao mara nyingi kama si mara zote imeweza kuzaa mijadala ya nyongeza juu yao.

Watu hawa mara zote wamekuwa hawakosi cha kuitetea misimamo yao na hawatetereki,
bila soni kabisa ingawa kwa baadhi yetu imetuletea ukakasi mwanzoni na sasa tumelazimika kuwazoea.

Ingawa wapo miongoni mwetu wanaoamini kuwa watu hawa wanaigiza kwa kuwa na misimamo hii,
Na kuwa uhalisia wao na kinachotafsirika humu ni tofofauti.

Bila shaka wadau mtaniunga mkono kuwa kisaikolojia kuna HISIA lazima mtu unakuwa unaijenga unapoona mtu fulani katika michango yake humu mara zote anakuwa na mlengo fulani ambao haubadiliki na mara zote amekuwa akiutetea na kuonekana kuwa hana hata dalili ya kuwa atabadilika.

Sasa basi, Kwa wadada hawa niliowataja kutokana na michango yao mbalimbali hisia zangu zimenipelekea kujenga picha ambazo mwishowe kunipa Sura na kuhisi hata tabia zao pengine zinaweza kufananaje.

Naweza nisipatie vyote lakini kwa kiasi fulani kuna ambayo yatakuwa sahihi na wadau mnaowafahamu kiuhalisia ama kwa hisia kama mimi tutasahihishana kama si kuongozea na tukipata ushuhuda pia haitakuwa mbaya.

UCHAMBUZI:

1.Lara 1.

Huyu atakuwa ni anti wa makamo,
Most probably age above 40,
ELIMU:Kama hana Ka-master's Kichwani basi,
atakuwa Mtoto wa fisadi fulani aliebahatika kusoma kwa kipindi fulani Ulaya kama Si Amerika,
na baada ya Kumaliza akalazimishwa na wazazi Kurudi kuijenga Bongo kama hakuharibu huko.
Ana umbo la Ki-miss, Mweupe pee na mwenye kupenda Uzungu mwingii.
Kwenye mambo ya kilauri humtoi hata kidogo,
MAHUSIANO:Akikupenda umekwisha,
Hana ndoa, na anaitamani sana ingawa life style yake na maisha ya Kiswahili haviendani.
Kwahiyo atasubiri sana swala la ndoa.

-Ni mhongaji mzuri lakini ni gandaganda balaa mwanaume hutapumua,
Atatamani awe na wewe kila sehemu na aku-control kama remote.
Ana tabia ya kutaka aonekane kwa watu na mara nyingi hapendi kuonewa.
Ni mcheshi na msemaji sana lakini ni wale wanaohubiri wasichokitekeleza.
Wadau msihadaike, Si kweli kuwa anapenda kupokea ndipo atoe, la hasha,
Huyu badala yake ndie mtoaje mkuu-Bahati ikikudondokea lakini.


Miss.Chagga.

SHULE:Huyu atakuwa ni graduate ambae bila shaka anajuta hata shule alifuata nini,
Kama alichelewa vile-Kwa kuwa kashaijua Pesa basi pesa kwake ni kila kitu.
UHUSIANO:Ni mama mtu mzima mwenye mtoto mmoja,
yupo kwenye ndoa yake yenye furaha na mara zote nia yake ni kuchokonoa mijadala kunogesha mazungumzo,Si binti mdogo kama wengi tunavyoweza kufikiria.
Mpenda kuzitafuta Chapaa haswaa na anazo kimtindo ingawa anatamani hata Chapaa za Dunia nzima ziwe zake.
Umri zaidi ya 35.
Ni mpole, Mfupi wastani na Tipwatipwa, Mwenye ngozi nyeusi ya kung'ara pia anaechukia kujipura.
-Yaani mpenda mambo ya natural tu hanaga muda wa kupoteza.
Ni mpenda watu na anaependa sana urafiki na wanaume zaidi kuliko wanawake wenzake.


Kasinde.
Haka ni kabinti ka chini ya miaka 30, kasomi kazuri lakini kanakotamani utu uzima sana.
Kanasotea ndoa kwa udi na uvumba bila kujua kuwa waliomo kama miss. chagga wanatamani kutoka ili wakatengeneze pesa kwa nafasi - masikini hakafahamu.
Kasi- Ni karefu ka wastani, maji ya kunde na umbo la kumtega mwanaume mroho.
Ila, Kwa kuwa nimuoga hategeki kirahisi.

Mikasa yote ya kimapenzi anayoiletaga humu kiukweli anatamani ingekuwa inamtokea kweli lakini si hivyo kiuhalisia.

Wadau najua hata ninyi mnaweza kuwa na Picha zenu juu ya hawahawa niliowataja au wengine ruksa kudondosha na kisha tupate ushuhuda kama itawezekana.

Nawasilisha.

 

Shy land

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
5,944
1,250
MKUU BWAi Dalalitiz kama wewe kweli unahisi kutokana na commeti za mtu naomba uniambie Shy land, nikoje na ninapenda nini??.
 
Last edited by a moderator:

Uni mwanitu

Senior Member
Oct 25, 2014
197
195
Shy land bhana wee lazima utakuwa msomi unae penda kuchunga mifugo na unapenda sana wanawake weweee.!
 

Tarime one

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
2,249
2,000
Pale kwa lara1 naweza kukubaliana na wewe,she is strong woman,ambae anasimamia kwenye jambo analoliamini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom