Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,041
- 39,988
Ma ladies na ma gentlemen.....
Kama nilivosema hapo juu hiki nikisimuliacho nimekosa jina au neno la kuweka kama kichwa cha habari au uzi.
Iko hivii......
Week end hii iliyoisha nilienda Mbeya na nilikuwa maeneo ya pale pale town. Nilipofika kuna mwenyeji wangu alikuja nipokea na nikakarimika ila tuu nilikataa kulala kwake maana angenizuia mambo yangu ya kupopo. Mwenyeji wangu ameolewa na anaishi na mume wake na watoto 5. Huyu tulifahamiana huko kitambo na tunawasiliana vizuri, nilipokwambia nakuja mbeya akaniambia niwe mgeni wake. Sikumkatalia ila nilijipanga na kusema sitalala kwake. Hapo kwake nilikuta anaishi na mschana wa kazi ambaye ni mja mzito ila tumbo lake halikuonesha kuwa ni la kukuibia kujifungua.
Siku ile alinikirimu nikamuaganaenda kulala hotelini maana mambo ya kutoka na kurudi saa nane usiku uanze kumgongea mlango mtu na kwake si ustaarabu.Mishe mishe zangu zilipoisha nikapita kumuaga mwenyeji wangu ndo nielekee airport. Kufika pale namkuta mumewe namuuliza wapi rafiki yangu akasema yuko hospitali kampeleka mschana wake u changu umemshika na hivi tuongeavyo kujifungua mtoto wa kike. Nilikuwa na taxi na bado nilikuwa na muda nikaaga na kumwambia taxi driver anipeleke hospital waliyokuwa.
Kufika hapo ndo rafiki yangu ananisimulia kuwa.Huyo mschana alikuwa anafanya kazi Dar walipogundua ana mimba wakamfukuza kurudi kwao alipofika kijijini mama yake na huyo mschana ndo akamuomba mwenyeji wangu kuwa huyo msichana aje afanyekazi hapo kwake apate vihela vya kujikimu akijifungua. Sasa hapo akawa anampigia simu mama wa yule mschana aje town kumchukua mschana wake akalee mjukuu......
Siku kama sana nikaaga zangu kuelekea airport. Njia nzima nikawa nawaza....
Hawa waschana wa kazi wanapata shida sana, wanavumilia mengi kwenye nyumba za watu. Sikupata nafasi ya kuongea na yule mschana ila nikawaza kuwa......Baba mwenye nyumba alipokuwa akifanya kazi alimbaka au walikuwa na mahusiano sasa mimba imekamata mschana anatimuliwa arudi kwao na huko anaonekana muhuni kuwa karudi na mimba.
Yawezekana alikuwa msichana kiburi na vijana wa mtaani ndo wamemmimbisha.
Yaweza kuwa hiyo mimba alitoka nayo kijijini na ilipogundulika mwajiri wake akamtumia.
Yaweza kuwa kamimbishwa na mtoto wa mwajiri wake ila mama akamtimua mschana ili mwanae aje kuoa mschana wa level yake.
Yawezekana ni ndugu au jirani wa mwajiri ndo alimrubuni kuwa watakuwa wote ila baada ya mimba kamkimbia na mwajiri kam fukuza.
Nachowaza. ........
Watoto wanaozaliwa vijijini baada ya mschana wa kazi kutiwa mimba mjini au alikokuwa anafanya kazi wanaume huwa wanawakumbuka watoto wao?
Watoto wa hivi wako wengi sana tena sana na si sawa na si haki kuwaacha walelewe mazingira hayo huku wao wakiendelea kumimbisha wengine wanaokuja.
Sijui...... nimeishia hapo kuwaza......
Asante mods kwa kunipatia kichwa cha uzi huu. Ujumbe maridhawa.
Ila...... kuna wanaosifika kwa kubeba mizigo mizito zaidi ya wanyamwezi? nauliza tuu.....