Wasichana 40 kwenda Swaziland kujifunza Reed Dance!! - TAMKO FEMACT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasichana 40 kwenda Swaziland kujifunza Reed Dance!! - TAMKO FEMACT

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kisendi, Jun 19, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  HII NI KWELI MLIOSOMA DAIL NEWS

  Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa jinsia, haki za binadamu, maendeleo na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct) hapa nchini,tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti la Daily News la tarehe 11 June 2011 , kwamba Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameridhia mkataba wa makubaliano na Mfalme Mswati 111, wa Swaziland unaohusu wasichana 40 toka Tanzania kwenda Swaziland mwezi Oktoba mwaka huu, kwa ajili ya kujifunza na kusherehekea ‘ reed dance’(utamaduni wa Waswaziland ambao unaruhusu wasichana waliyo bikira kucheza dansi hii ya jadi mbele ya mfalme, malikia na viongozi wengine. Kila mwaka takribani wasichana 40,000 husherekea siku hii, ambayo hapo awali ilikuwa ni njia moja ya kumuezi malkia. Baadaye dansi hii imekuwa ikitumiwa na mfalme kuchagua mke kutoka kwa mabinti hawa ambao kwa hali ya kawaida sheria zetu zingalikataza kwani ni ukiuakwaji wa haki za watoto wa kike.
   
 2. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wanyama wanapakizwa kwenye madege tume kaa kimya, sasa hii ya mabinti zetu akiyanani atadhurika mtu
   
 3. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huu muungano wa wana harakati wangeanza kukomboa kwanza dada zetu pale mitaa ya Meeda,Ambience, Maisha na kwingineko penye ishu kama hizo ndo ningewaona wa ukweli zaidi. Vinginevyo tamko lao hili ni nothing but unafiki wao tu hawa wanaharakati.
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  sasa serikali yetu hii jamani, mipango gani hii? mila za waswazi na sisi wapi na wapi? nafikiri kuna watu wana senti zao hapo, si bure!
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Yaani wanaenda kukaa nusu uchi kama mabinti wa kule?
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Mkwer.e anataka wakajifunze ili aje ajipakulie kiulaini
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wanaoenda mitaa ya Meeda, Ambience, Maisha etc hawajepelekwa hapo na mkuu wa wilaya, mkoa au kiongozi yeyote wa serikali. Kama hii habari ni kweli kuwa Rais wetu ame-sign mkataba wa kupeleka mabinti wadogo Swaziland naweza kusema kuwa anafanya kazi ya u-pimp!
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Kuna tamaduni za kiafrika za kuiga ila si hii Reed dance. Yaani kweli Rais anaweka mkataba wa kuwapeleka mabinti zetu kujifunza uchafu huo? Ina maana watenda mabikra au?
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  amepelekewa King kuchagua mke
   
 10. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,830
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli ****** ameingia mkataba huo na king mswati,basi hana busara wala hekima...shortly RAIS 'WETU' NI MWEHU!
   
 11. f

  fazili JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hicho ndicho kikomo cha akili ya viongozi wetu, mambo ya ufisadi, wizi wa wanyama na kuuwawa kwa watu Mara hakuwafanyi wafanye chochote lakini kwenda kucheza ngoma uchi wanatuma watu mara moja!

  Tuombe Mungu atusaidie walah!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Niliongea siku moja kwenye thread fulani kwama kuchanganyikiwa si kuokota makopo tu, inategemea na hadhi ya mtu. Sasa hii ya kufanya makubaliano na King Mswati kupeleka wasichana kucheza dance mbele yake ili achague anayempenda maana yake anataka King Mswati awe shemeji yake? Angekuwa ni dini nyingine wangeongea mengi lakini Mwislamu kukubali utamaduni huo natilia shaka kama alituliza vizuri akili yake kabla ya kumwaga wino.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kanisa la Assembles of God ni wakarimu sana, washauri wa Rais Kikwete wampeleke Rais wetu akaombewe, maana hali inavyozidi ndo mambo yanaharibika zaidi hata kuamua kupeleka wasichana kujifunza utamaduni wa kigeni kinyeme cha maadili ya kitanzania na dini ya kiislam
   
 14. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hivi wazazi watawaruhusu binti zao waende huko kweli?
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kama wazazi wanaruhusu mabinti kwenda Big Brother, hali wakijua wanaenda kuwowana live mbele ya makamera, watakataa kwenye hili lenye mhuri na saini ya RAIS wa Jamhuri? Kwakweli Nimeamini ****** haachi asili...
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Lotus na bhoke walirusiwa na nani kwenda kumugwa hadharani?
   
 17. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Lotus na bhoke walirusiwa na nani kwenda kumegwa hadharani?
   
 18. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kama mabinti zetu watapelekwa huko dunia nzima itatushangaa kwani hata hapa kwetu kunamakabira ya ngoma za jadi na matamasha yanayofanyika kila mwaka na bado watoto wetu hawayajui- kwa ufupi: yanakufa, sasa inashangaza kupeleka watoto wakajifunze foreign culture.
   
 19. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  marais wanaraha dunia hii
  yaani wanaona kitu live bikira mmmmmmh

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli wazazi tuna mitazamo tofauti. Mimi katu siyawezi haya ya kuruhusu kuona binti zangu waninyanyase kiasi hicho. Ofcourse kuna uwezekano wa mabinti kwenda bila ruhusa - hapo mzazi anakosa control.
   
Loading...