Wasi Wasi wa Udini

Status
Not open for further replies.
zanzibar iachwe iungane na OIC iili kelele zipungue maana.

Maana mkombozi wao wanaona ni OIC!

Mimi ukiniuliza kuhusu muungano, nitasema zanzibar iachwe iwe nchi kamili. Na Tanganyika izaliwe tena na tusiwe na serikali ya tatu!

Wapemba/zanzibar wote walioko Tanga na Dar nk warudishwe tanzania visiwani.
 
hilo la mwisho ndilo gumu..!! nafikiri kuna watu Zanzibar ambao wako karibu zaidi kinasaba na waarabu kuliko watu wa bara na hivyo kujiona kuwa Tanganyika siyo mahali pao hasa, wako tayari kujiunga na Oman kuliko bara.
 
Na waende huko!..Wazaire zamani walijiona sana kuwa wao Wafaransa. Hadi Mobutu alipokuja na Uafrika walimwona kichaa. Ulimbukeni unakuja na mengi... wako wapi leo hii wanakizungumza kiswahili hadi Ikulu yao!..
 
Naona dawa ni ku-dissolve kale ka-serikali kao na kubaki na serikali moja tu... kama hawataki tuvunje muungano tubaki na tanganyika yetu. Tumezidi kuwaonea haya. Mijamaa mibishi kama nini yaani!
Halafu wamekataza kuingiza kiti-moto... damn!
Wanataka kunikosesha starehe tu!
Teh TEh!
 
labda nguruwe wamekula ndege halafu wao wakapatwa na mafua halafu binadamu wakila nguruwe waliokula ndege basi na wao wanapatwa na mafua ya ndege walioliwa na nguruwe!
 
Kitendo cha Uganda Somalia pamoja na Iran, Yemen, Libya etc kusemwa na UN kuwa inashiriki katika kuchagiza vita vya somalia NI MATOKEO YA KUJIUNGA NA OIC???
Haya sasa ngoja kwetu wsng wafanye jitihada za kutaka kujiunga na OIC!
 
Fanyeni utafiti wa kutosha kuliko kusema OIC haifai kwa hadithi za mtaani.
Nadhani Tanzania kwa hali tuliyo nayo kuacha fursa hii ya OIC ni kujirudisha nyuma kimaendeleo.
nimeona kama UK wanayo Islamic bank, islamic TV. na hata waziri wa mambo ya nje amekuwa akiwasaidia waislam wanapokwenda Hijja kwa mambo mengi tu. hapa wenzetu wana apply diplomatic Economic kwa vitendo.
jiulize kodi ngapi wanapata kwenye Benki. Tv n.k
Chukulia mahujaji 20.000 wanaondoka kila mwaka kuna kodi na pesa ngapi zinapatikana?
tuache political diplomatic na twende na wakati
 
Ndugu zangu,

Lazima nchi iwe na msimamo. Zanzibar sio nchi, na OIC ni umoja wa nchi za Kiislamu. Zanzibar kujiunga na OIC ni Zanzibar kuwa nchi, na hiyo ni kuvunja muungano. Kwa bahati nzuri, Mwalimu alitazama mbele sana alipounganisha TANU na Afro Shirazi Party. Kutokana na umoja huo, si rahisi kuvunja muungano.

Ukilegeza msimamo (principle) ili kuondoa manunguniko, basi unajitakia matatizo makubwa. Yatakuja madai mengine, na kila likikubaliwa moja, lingine litajitokeza. Yako, na tunajua mfululizo wake.

Tanzania (yote) si ya Wakristo au ya Waislamu. Haina dini. Watanzania wana dini zao, lakini nchi ya Tanzania haina dini, na kwa msimamo huo, haiwezi kuwa mwanachama wa umoja wa nchi za dini fulani. Si vizuri tuige makosa yanayofanywa na nchi nyingine.

Augustine Moshi
 
zANZIBAR wanifanya kuleta hoja ya OIC ambayo amani diria ooh sorry karume oooh babu yes amni karume ameibua hii hoja makusudi ili kuweka uuwiano kwenye mijadala yao ya ndani na kikwete[scratch my back i scratch yours] kila mara inapotokea hoja aina hii sitting president wa zanzibar huja na hoja hii kama ramsom ya kukubaliwa matakwa yao.mfano..

1.sasa hivi karume anataka ku press jk aache kumfuata fuata na issue ya kukaa na hawa CUF.SO Inabidi tuchague kati ya kumuacha atawale anavyotaka au tumuache ajiunge na OIC mwiba kwa watanganyika,.
aifha karume ameshasema hayuko tayari kuhudhuria mkutano wowote ambao kikwete ataibua hoja ya CUF hadharani.na tayari kuna kununiana kati ya wazee wa baraza la mapinduzi na kikwete.
CUF wanajipendekeza makusudi kwa kikwete ili kuendelea kuwagonganisha karume na kikwete....tangu lini maalim amsifie rais wa ccm kama sio kuwaletea sintofahamu,ambayo anaonekana kufanikiwa kidogo.

2.hoja ya pili ambayo znz wanataka kupress ili wasijiunge na OIC ni kutaka mafuta yanayodaiwa kuwepo pemba yawe yao pekee[chako changu ,changu changu]
lakini hapo kuna kasheshe kubwa ,kama mafuta yatashimbwa pemba ambayo ina wasomi na wanajua miaka yote pemba imekuwa muhimili wa uchumi znz lakini ikibakia nyuma kimaendeeo ,kumbuka karafuu ya pemba imejenga unguja tangu zamani,sasa haya mafuta yataleta mgongano sana maana pemba hawatakubali.
hata nguvu ya CUF inatokana na pemba kuachwa nyuma kimaendeleo.

suluhisho ni kuwa tusikubali zanzibar kujiunga na OIC kama wako ndani ya muungano na ukweli ni kuwa zanizibar ni moja kwa sababu ya kuwa sehemu ya muungano kama wakijitoa leo,kesho tu pemba watajitenga na unguja watakufa njaa kwa sababu watakuwa hawana shamba tena .watabakiwa na njia moja tu ya uchumi nayo ni utalii.
hoja nyingine ni kuwa wanasiasa wengi wa unguja wanafaidika na muungano kwa kupataajira za kisiasa,,angalia bzanziba yenye wananchi milioni moja inawakilishwa kwenye muungano na wabunge 70,mawaziri 5,mabalozi na maafisa wengi tuu acha wakuu wa idara nyingi tu kutoka huko,sasa lazima kila mzanzibar atakuwa na ndugu kiongozi.baraza lao lina wawakilishi 80,mawaziri 20,wakuu wa mikoa 5,wakuu wa wilaya 12,madiwani ,masheha,a wengine kama hao uande wa chama bado wana gharama za majeshi yasiyo na kazi kmkm,valantia ,mafunzo.uchumi.,mgambo,zimamoto nk
kwa kifupi maendeleo ya zanzibar yanadumazwa na gharama kubwa sana za utawala.ni kubwa mno kwa uuwiano wa watu milioni ,,angalia wilaya ya kinondoni inapata mapato zaidi ya zanziba na ina mkuu wa wilaya 1,wabunge 2,viti maalum2,madiwani 20.watendaji kata 60 basi ...karume apunguze gharama za utawala.

zanzibar leo wanaitaji muungano udumu zaidi yetu watanganyika...
 
Augustino Moshi
Mbona unaleta vioja? Msumbiji ni nchi ya kiislam? Uganda ni nchi ya kiislam? Ivory coast nayo?
majungu haya hayatawafikisha popote.
nchi za Ulaya na marekani zinahangaika kuwa karibu na UAE. sababu wanajua huko ndio kwenye turufu.
mimi sioni sababu kwanini Tanzania tusiwe wanachama wa OIC.?
WEWE MOSHI umesoma soma nini na una claim kuwa ni phd holder?au ndio nyie akina book-knowledge nje ya kitabu huwezi kupapambanua mambo.
basi na petrol na diesel tu import toka Vatican? maana kitu kinachohusu uislam kwenu ni uadui.
Kama wasomi wenyewe ndio nyinyi TZ inasafari ndefu
 
Chinga,
Tuliza boli. Kama Msumbiji wamejiunga sijui katiba yao inasema vipi. Uganda ilijiunga chini ya Iddi Amin. Tunajua Uganda waislamu ni 10%. Lakini Museveni alivyoingia mamlakani akaona hakuna sababu za kubadilisha hilo. Moshi is right, sisi katiba yetu inatufunga mikono. Nothing to do with Vatican. And I am not Catholic, for your info.
 
phillemon mikael said:
zANZIBAR wanifanya kuleta hoja ya OIC ambayo amani diria ooh sorry karume oooh babu yes amni karume ameibua hii hoja makusudi ili kuweka uuwiano kwenye mijadala yao ya ndani na kikwete[scratch my back i scratch yours] kila mara inapotokea hoja aina hii sitting president wa zanzibar huja na hoja hii kama ramsom ya kukubaliwa matakwa yao.mfano..

1.sasa hivi karume anataka ku press jk aache kumfuata fuata na issue ya kukaa na hawa CUF.SO Inabidi tuchague kati ya kumuacha atawale anavyotaka au tumuache ajiunge na OIC mwiba kwa watanganyika,.
aifha karume ameshasema hayuko tayari kuhudhuria mkutano wowote ambao kikwete ataibua hoja ya CUF hadharani.na tayari kuna kununiana kati ya wazee wa baraza la mapinduzi na kikwete.
CUF wanajipendekeza makusudi kwa kikwete ili kuendelea kuwagonganisha karume na kikwete....tangu lini maalim amsifie rais wa ccm kama sio kuwaletea sintofahamu,ambayo anaonekana kufanikiwa kidogo.

2.hoja ya pili ambayo znz wanataka kupress ili wasijiunge na OIC ni kutaka mafuta yanayodaiwa kuwepo pemba yawe yao pekee[chako changu ,changu changu]
lakini hapo kuna kasheshe kubwa ,kama mafuta yatashimbwa pemba ambayo ina wasomi na wanajua miaka yote pemba imekuwa muhimili wa uchumi znz lakini ikibakia nyuma kimaendeeo ,kumbuka karafuu ya pemba imejenga unguja tangu zamani,sasa haya mafuta yataleta mgongano sana maana pemba hawatakubali.
hata nguvu ya CUF inatokana na pemba kuachwa nyuma kimaendeleo.

suluhisho ni kuwa tusikubali zanzibar kujiunga na OIC kama wako ndani ya muungano na ukweli ni kuwa zanizibar ni moja kwa sababu ya kuwa sehemu ya muungano kama wakijitoa leo,kesho tu pemba watajitenga na unguja watakufa njaa kwa sababu watakuwa hawana shamba tena .watabakiwa na njia moja tu ya uchumi nayo ni utalii.
hoja nyingine ni kuwa wanasiasa wengi wa unguja wanafaidika na muungano kwa kupataajira za kisiasa,,angalia bzanziba yenye wananchi milioni moja inawakilishwa kwenye muungano na wabunge 70,mawaziri 5,mabalozi na maafisa wengi tuu acha wakuu wa idara nyingi tu kutoka huko,sasa lazima kila mzanzibar atakuwa na ndugu kiongozi.baraza lao lina wawakilishi 80,mawaziri 20,wakuu wa mikoa 5,wakuu wa wilaya 12,madiwani ,masheha,a wengine kama hao uande wa chama bado wana gharama za majeshi yasiyo na kazi kmkm,valantia ,mafunzo.uchumi.,mgambo,zimamoto nk
kwa kifupi maendeleo ya zanzibar yanadumazwa na gharama kubwa sana za utawala.ni kubwa mno kwa uuwiano wa watu milioni ,,angalia wilaya ya kinondoni inapata mapato zaidi ya zanziba na ina mkuu wa wilaya 1,wabunge 2,viti maalum2,madiwani 20.watendaji kata 60 basi ...karume apunguze gharama za utawala.

zanzibar leo wanaitaji muungano udumu zaidi yetu watanganyika...

BWANA PHILEMONI,
Unajua baada ya kusoma post yako jana nilishindwa nikujibuje lakini nadhani majibu yako humu humu...tena katika topiki ambazo hujajibu kitu kluhusu memorandum and articles za muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar na hili la OIC haliwezi kuendelea mpaka hapo tutakapoangalia huo muungano wenyewe ukoje

Nakushangaa unajibu hoja zako bila kujua mkataba wa muungano kati ya Zanzibar unasema nini kuhusu hii issue na sidhani kama unajua kuwa ukweli ambao wengi hawaambiwi ni kuwa Nyerere alimshawishi Karume kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ili kuifunika Zanzibar isiweze kuwa na uwezo wa kuwa na mahusiano na nchi za nje bila ya kupata ridhaa ya serikali ya muungano,ambazo kimsingi ni Serikali ya Tanganyika

Hata ukitazama muundo wenyewe na muungano utagundua kwamba unaifanya Tanganyika kuwa nchi kuu na Zanzibar kuwa chini ya Tanganyika kupitia serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kwa sababu Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ndiye Rais wa Tanganyika ndiye mkuu wa nchi ikiwemo Zanzibar na ndiye kiongozi mkuu wa viongozi wote akiwemo Rais wa Zanzibar, na pia ndiye Amir jeshi mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar.

Ni kwa sababu hizi basi Mwalimu Nyerere ilibidi awe mkali kwa mtu yeyote atakaye hoji mfumo wa serikali mbili na kama unataka kuja na hoja basi natumai kuwa utakumbukwa kwamba Nyerere alilisambaratisha kundi maarufu la Wabunge wa CCM (GSS) lililotaka mfumo wa serikali tatu mwaka 1992, kwa hoja kwamba mfumo wa serikali mbili ni sera ya CCM na anayehoji hilo basi kwanza atoke CCM!!!!!!!! Nyerere alikuwa ni mtu wa mahesabu siku zote kwa sababu aliona kwa kuleta serikali tatu kutafanya Tanganyika iwe na serikali yake

Matokeo yake ni kwamba Tanganyika itakuwa na hadhi sawa na Zanzibar jambo ambalo litaifanya Zanzibar kuwa kama nchi huru isiyo chini ya Tanganyika bali chini ya serikali ya muungano ambayo itabidi iwe na udhibiti ulio na uwiano sawa kati ya Zanzibar na Tanganyika. Hivyo mpango wa kuitawala Zanzibar kupitia serikali ya Muungano inayodhibitiwa zaidi na Tanganyika usiwezekane au kuwa mgumu.

Lakini kwa nini tuandikie mate wakati wino upo? Kwa sababu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa tarehe 26.4.1964 uliunda nchi moja iliyoitwa. "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo tarehe 11.12.1964 jina hili lilibasilishwa kuwa sheria namba 61 ya 1964 na kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Ni siku hii hii mkataba wa Muungano kati ya Serikali za Tanganyika na Zanzibar ulipitishwa naBunge la Jamhuriya Tanganyika na Sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitishwa (Act No. 22/1964 Cap 557). Katika Mkataba wa Muungano Serikali za Jamhuri ya Tanganyika na ile ya watu wa Zanzibar zilikubaliana kuunda serikali moja kamili ya Jamhuri (SOVEREIGN REPUBLIC). Kwa hiyo kwa mkataba huu hakutakiwa kuwe na nchi kamili "Sovereign state" inayoitwa Zanzibar wala Tanganyika bali kuwe na "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" ambavyo ndivyo "Sovereign Republic" au "Sovereign State" inayotambuliwa na mkataba wa muungano.

Mind you mambo yote haya yalifanywa kwa haraka sana chini ya kipindi cha miezi minane (8) wakati ambao Zanzibar hata haijakaa sawa baada ya mapinduzi ya mwaka huo yaliyoiweka madarakani serikali ya mapinduzi, ilihali wenzao wa serikali ya Tanganyika walikuwa tayari wana miaka mitatu (3) ya uhuru hivyo walishajiandaa kiutendaji ndio maana hata mkataba wa muungano uliweza kuiweka juu Tanganyika na Zanzibar kuwa chini na kutimiza mpango wa Hayati Nyerere.

Then kuna kundi lingine ambalo wanaotaka Zanzibar itambuliwe kama mkoa wa Tanzania walikuwa na kiu ya muda mrefu ya kuimwaga siri hii ya Muungano wa Tanzania, lakini inawezekana walikuwa wanamhofia Nyerere, kwa sababu kama suala la watu kushitakiwa kwa uhaini Zanzibar hii si mara ya kwanza na pia kesi hii ina zaidi ya miaka miwili siku zote hizo mbona hawakuwahi kutamka kuwa Salmin au Rais wa Zanzibar hawezi kupinduliwa kwa sababu serikali yake ni sawa na ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam?

Mwisho ningependa kukufahamisha kuwa kabla hujarukia hoja ulizitoa hapo juu ni bora ungetazama hadhi ya Zanzibar hasa linapokuja suala la mahusiano ya Zanzibar na nchi za nje katika kuinua uchumi wake kama vile kujiunga na OIC na uanzishwaji wa Bandari huru.
 
dr who,

mimesoma ujumbe wako na nimetumia muda kutafakari ili niweze kukujibu inavyopasa,awali ya yote kwenye hoja yangu ya msingi nilijaribu kuonyesha namna SMZ inavyopenda kutumia hoja tata kila mara panapokuwa na mahitaji wanayotaka[mf umeme]au wanapotaka kuweka hoja [mf maridhiano na CUF.

Katika hoja yako umejaribu kugusia suala la nyaraka za muungano,kama utajaribu kukumbaka nyaraka za muungano zimekuwa siri sana hadi kuna vijana wameonyesha na ya kwenda mahakamani ili kulazimisha articles za muungano ziwekwe hadharani.

Nimejaribu kuonyesha kwamba muungano unawaunganisha watanzania pamoja na zanzibar wanauhitaji.aidha kuhusu mkataba wa muungano pia nakubali kwamba inabidi ifanyike referendum na wananchi waweze kuchagua muungano wanaoutaka,hii itaondoa dhana kuwa muungano ulikuwa wa nyerere na karume ,kura ifanike ili kuuleta muungano kwa wanaNCHI.

Sidhani kwamba nyrere alimlazimisha karume ,ukweli upo,soma nyaraka mbali mbali kwenye vitabu na internet utaweza kuulewa presure ya muungano ilikuwa kubwa ilikuwa ni lazima tuungane kwa sababu zifuatazo.

1.kumbuka zanzibar ilipatukana kwa mapinduzi kwa hiyo sababu ya mwanzo ya karume kutaka muungano haraka ni usalama,,,alikuwa akiofia counter attack kutoka kwa serikali ya oman au serikali iliyoangushwa.,kwa hiyo muungano uliihakikishia zanzibar usalama kutoka kwa maadui wa ndani na nje.

2.suala la pili lilioharakisha muungano ni CIA ,serikali ya marikani ikimtumia afisa wake wa ujasusi[jina limenitoka], aliyekuwa congo kinshasa alitumwa kwa mwalimu kuhakikisha muungano unaharakishwa ili zanzibar isiangukie kwa makomunist,na zanzibar ipo very strategic located kwa usalama wa horn of africa hadi cape of good hope...na mkumbuke kuwa kipindi hicho nyerere bado alikuwa akiaminika kwa wamarekani,,,alikuwa hajaonana na mbatizaji wake mao tse tung.that was american influence...copled with COLD WAR era.

3.sababu ya tatu ya muungano kuharakishwa ni ya kihistoria ,wananchi wa unguja na bara tumekuwa na uhusiano wa kindugu kutokana na wazanzibar wengi kuwa na asili ya bara.hata wengi wa viongozi wa zanzibar wamezaliwa bara .

kuhusu kura ya maoni ilikuwa ni vigumu kutokana na mavo niliyokwishaaeleza na pia uelewa wa wananchi wa pande hizi mbili bado ulikuwa mdogo kuweza kufanya referendam vizuri,msisahau zamani hata uchaguzi naa si zaidi ya miaka 25 iliyopita watu walikuwa wanachagua kwa kupambanisha alama kama numba ,jembe,nyundo nk so demokrasia ilikuwa bado..mtu akipata alama ya jembe ilikuwa lazima ashinde.
Pia msisahau uchaguzi wa aina yoyote zanzibar karume alisema haungefanyika mpaka baada ya miaka thelathini,hadi anauwawa hakufanya uchaguzi.

kuhusu nyerere kupinga hoja ya G 55 ,hiyo ilikuwa ni lazima kwani nyerere alikuwa ni muumini wa muungano tena wa africa,,na pia nyerere aliudhiwa na kitendo cha malecela kumshauri mzee mwinyi vibaya.

pia nilijaribu kuonyesha kuwa serikali ya mapinduzi imeelemewa nagharama kubwa za utawala kwa uuwiano wa wananchi milioni moja ,uzalishaji ,irelevant ratio..naomna hili hujapinga

kwa kumalizia nasisitiza kuwa hali ya muungano ni vema tufanye kura ya maoni ili muungano uwe wa watu na si wa viongozi,aidha suala la OIC ni la mambo ya nje ambalo ni suala la muungano kwa hiyo zanzibar haitaweza kujiunga na OIC kama hakuna maafikiaano kimuungano,kama taasisi ya OIC inataka kusaidia zanzibar inaweza kuwatambua na kuwasaidia katika arrangement ambazo hazitufungi kama wao wataona inafaa au inavyofaa,...
 
Jasusi
Uganda haikuingizwa na Alhaji Iddi Amin nakumbuka ni kati ya 1987 na 1988 na Idd Amin aliondoka 1979, ambapo wakaingia huko na kuanza na project ya chuo kikuu ambapo serikali ya uganda ikasema 10 percent ya wanafunzi wawe wakristu.
Hiki chuo Islamic University in Uganda kina mchango mkubwa sana ktk uchumi wa uganda. na kimekuwa bega kwa bega na Makelele university. na hata ajira kwa waganda wanafunzi waliosoma hapo wana market kubwa. sababu chuo kinalipa kwa dola walimu hivyo kina walimu bora. hao ndio wanaotumia diplomatic economics sio sisi akina diplomatic ukristu.
Mfano miaka ya nyuma kidogo kilitoa scholarships 100 kwa TZ. KUSOMEA fani mbalimbali kama uhasibu, ualimu, uchumi ,mass communication,sheria .nk
jee kubishana huku kunatusaidia nini? jiulize uganda imeingiza pesa ngapi kutokana na chuo hicho? acha miradi mingine. Ndio maaana Museven akaona faida na OIC, yeye anatizama maslahi ya nchi na si kanisa katoliki tu,hiyo ndio diplomatic economic.
Msumbiji wameingia hawana ujinga kama wetu, na hata Ivory coast wameingia jee kwanini Tanzania isiingie?
Jasusi, Moshi na kundi lenu kauli mbiu ya serikali ni Diplomatic Economic na si udini.
 
phillemon mikael said:
dr who,

mimesoma ujumbe wako na nimetumia muda kutafakari ili niweze kukujibu inavyopasa,awali ya yote kwenye hoja yangu ya msingi nilijaribu kuonyesha namna SMZ inavyopenda kutumia hoja tata kila mara panapokuwa na mahitaji wanayotaka[mf umeme]au wanapotaka kuweka hoja [mf maridhiano na CUF.

Katika hoja yako umejaribu kugusia suala la nyaraka za muungano,kama utajaribu kukumbaka nyaraka za muungano zimekuwa siri sana hadi kuna vijana wameonyesha na ya kwenda mahakamani ili kulazimisha articles za muungano ziwekwe hadharani.

Nimejaribu kuonyesha kwamba muungano unawaunganisha watanzania pamoja na zanzibar wanauhitaji.aidha kuhusu mkataba wa muungano pia nakubali kwamba inabidi ifanyike referendum na wananchi waweze kuchagua muungano wanaoutaka,hii itaondoa dhana kuwa muungano ulikuwa wa nyerere na karume ,kura ifanike ili kuuleta muungano kwa wanaNCHI.

Sidhani kwamba nyrere alimlazimisha karume ,ukweli upo,soma nyaraka mbali mbali kwenye vitabu na internet utaweza kuulewa presure ya muungano ilikuwa kubwa ilikuwa ni lazima tuungane kwa sababu zifuatazo.

1.kumbuka zanzibar ilipatukana kwa mapinduzi kwa hiyo sababu ya mwanzo ya karume kutaka muungano haraka ni usalama,,,alikuwa akiofia counter attack kutoka kwa serikali ya oman au serikali iliyoangushwa.,kwa hiyo muungano uliihakikishia zanzibar usalama kutoka kwa maadui wa ndani na nje.

2.suala la pili lilioharakisha muungano ni CIA ,serikali ya marikani ikimtumia afisa wake wa ujasusi[jina limenitoka], aliyekuwa congo kinshasa alitumwa kwa mwalimu kuhakikisha muungano unaharakishwa ili zanzibar isiangukie kwa makomunist,na zanzibar ipo very strategic located kwa usalama wa horn of africa hadi cape of good hope...na mkumbuke kuwa kipindi hicho nyerere bado alikuwa akiaminika kwa wamarekani,,,alikuwa hajaonana na mbatizaji wake mao tse tung.that was american influence...copled with COLD WAR era.

3.sababu ya tatu ya muungano kuharakishwa ni ya kihistoria ,wananchi wa unguja na bara tumekuwa na uhusiano wa kindugu kutokana na wazanzibar wengi kuwa na asili ya bara.hata wengi wa viongozi wa zanzibar wamezaliwa bara................
phillemon mikael said:
BWANA PHILEMONI

Unajua baada ya kusom majibu yako kwa kirefu nimeweza kuuunganisha mambo ambayo ni kiini cha mjadala huuu na naweza kusema haya mambo ni naTANO nayo ni; la kwanza ni MUUNGANO la pili ni ZANZIBAR tatu ni OIC nne ni NYERERE na tano ni UDINI

Unajua hatuwezi kuenda mbele bila kuangalia huko nyuma kulitokea mazingira gani yaliyopelekea kutokea kwa conspiracy hizi 2006

Huwezi kuzungumzia ya Zanzibar kujiunga na OIC bila kuangalia huyo Nyerer ambaye japo ni mfu lakini ana IMPACT ndani ya chama tawala...in otherwords wanaogopa kufanya maamuzi kwa sababu mwalimu asingelipenda hilo na naweza kusema kuwa they are right

Halikadhalika hata kama ungekuja na hoja ya namna gani on how innocent NYERERE alikuwa kuhusu huu muungano huwezi kuwaconvnce watu wa visiswani ambao ni 99% waislam MWALIMU na serikali zilizofuata zilikuwa na nia nzuri nao mfano ni pale punde tu baada ya uhuru Kilichofuata kilikuwa ni kukamatwa, kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislamu wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Nyerere.

Mashuhuri miongoni mwao walikuwa: Abdillah Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba na Shariff Adnan ,Rajab Kiguu cha Mbuzi na wengine wengi.

sasa unajua sitotaka kuipeleka hii topiki katika mabaya ya Mwalimu na Mchango wake katika hili ila nitaangalia zaidi upande wa KATIBA YA ZANZIBAR ambako ndiko tunaangalia hoja zinaendaje

Bwana PHILEMONI,Ukweli uko wazi, kiini cha tatizo hili la sasa kuhusu Zanzibar na katiba yao ni ukiukwaji uliofanywa makusudi, wa kutokutekeleza vizuri vifungu vitatu muhimu vya mkataba wa muungano wa mwaka 1964.

1. Kutokutekelezwa kwa kifungu namba (m)(b) kilichotaka kuwepo na taasisi za makamu wawili wa Rais ambapo mmoja kati yao aliye mkazi wa Zanzibar ndio anakuwa kiongozi wa Serikali ya Zanzibar na msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa kazi za kiserikali kwa upande wa Zanzibar.

2. Kutokutekelezwa kwa kifungu namba (vii)(b) kilichomtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamu wa Rais ambaye ni kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, kuitisha baraza la kutunga katiba likiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakari mapendekezo ya tume ya katiba na kupitisha katiba ya Jamhuri ya Muungano

3. Kutokutekelezwa kwa kifungu namba (viii) kilichotaka mkataba wa muungano kuthibitishwa kwa kutungiwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri la Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri na mkataba kupitishwa na kuundwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufuata masharti yaliyokubaliwa.

Bunge la Tanganyika lilitunga sheria ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Namba 22 ya 1964, Baraza la Mapinduzi la Jamuhuri ya watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na baraza lake la mawazi halikutunga sheria iliyotakiwa.

Hii ndio hali halisi ya muungano wetu, japokuwa tulizotaja hapo juu ni baadhi ya dosari nyingi zilizopo.

Huu si wakati wa kuendelea kukwepa ukweli, watu wa kulaumiwa katika hali hii ya kisiasa tuliyonayo sasa ni wale waliochangia au kusababisha kuwepo kwa hali hii ya utata kati ya katiba ya nchi na sera za chama, hali inayoonyesha jinsi dhamira zinazodaiwa kuwa ndizo zilizozaa muungano zilivyokuwa za bandia.

Nidhahiri sasa kuwa waasisi wa muungano tunaotakiwa kuulinda kwa gharama zozote kama ulivyo, kila mmoja alikuwa na sababu nyingine za ziada zilizomfanya aukubali muungano tofuati na ile iliyotajwa ya kudumisha udugu wa asili uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Hali tuliyokuwa nayo ya mfumo wa chama kimoja cha siasa wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza, haikuruhusu wala haikutoa fursa kwa wananchi kuweza kufahamu ukweli au jambo lolote kuhusu muungano, ilikuwa ni mwiko wa kisiasa kuutaja muungano kwa kuudodosa.

Mambo yaliyowapata wananchi wenzetu waliokuwa viongozi wa juu kabisa katika serikali ya Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe na Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuonyesha dalili tu za kutaka dosari zilizojitokeza katika muungano wetu ziondoshwe, sote tunazijua. WatanzAnia wote tukalazimishwa kukumbatia bomu lililokwisha washwa utambi huku hatufahamu ni lini litalipuka kisa Kumuenzi Mwalimu ambaye alikuwa hana nia nzuri nawaislamna zanzibar kujiunga na OIC.

Vile vile mwaka 1992 Mheshimiwa Jaji, sasa ni Mstaafu Francis Nyalali alieleza wazi katika ripoti yake kuwa muundo wa Serikali mbili una matatizo mwengi, muundo muafaka ni wa serikali tatu. Vigogo walipokutana Chimwaga wakasema hapana, Jaji Kisanga nae kama utakumbuka alirudia yale yale katika ripoti yake, nae pia aliameambiwa hapana sera za Chama Cha Mapinduzi hazibadiliki

Inashangaza leo kusikia mtu akisema kuwa upo uwezekano wa usultani kurudishwa Zanzibar wanataka kurekebisha katiba yao ili kumuwezesha rais wa Zanzibar, wanaemchagua kwa kura zao, kuwa na vipindi zaidi ya viwili atamshi ya aina hii ni ya watu waliofilisika kifikra ambao wanadhani wananchi wote ni wajinga.

Katika mkutano, Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika Dodoma, chama kilipitsha azimio kwamba suala la Urais wa Zanzibar na katiba likajadiliwe katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar. Je unajua kuwa wananchi walihoji ni lini Kadinali na wanasheria wa Chuo Kikuu na Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi wa Tanganyika walipewa mamlaka ya kutengua maamuzi ya mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Na kama si hivyo, hizi chuki za wazi zinazoonyeshwa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na Rais wao sababu yake nini? Haya mayowe tunayoyasikia kila kukicha ni kwa niaba na maslahi ya nani? Na kama watadai kuwa wanatumia haki yao ya msingi kama raia katika kutoa maoni kuhusu mambo ya nchi, ni lini wananchi wa Zanzibar - walinyang'anywa haki hiyo ili wasiwe na uwezo wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi yao, pale wanapoona inafaa.

Ni kawaida ya wakati kuwa ndio muamuzi wa kweli na huu ni wakati wa ukweli na uwazi, kwa hivyo ni wakati muafaka kuachana na tabia mbaya tunayotaka kurithi ya kuendesha nchi kwa ngonjera, Propaganda za magazeti na vitisho.

Viongozi waache hofu. Kinachotakiwa kufanywa ni kuilea demokrasia inayoanza kukua kwa faida na maendeleo ya nchi yetu na mojawapo kuaruhusu waZanzibari kujiunga na jumuia ambazo wanaona zitakuwa na mafufaa wao kama OIC
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom