Washukiwa watatu wa mauaji Tanga wauawa wakati wa majibizano ya risasi na askari

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Watu watatu wanaodaiwa kuwachinja watu 8 katika eneo la Kibatini lililopo kata ya Mzizima jijini Tanga wameuawa na Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi katika majibizano ya risasi wakati walipokuwa wakitaka kutoroka baada ya kukamatwa kisha kuwapeleka askari katika pori kuwaonesha silaha aina mbali mbali walizokuwa wamezifukia.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msadizi wa Jeshi hilo nchini Leonard Paul amesema silaha zilizokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na Jambia ambalo limetumika kuwachinja watu hao,SMG mbili, bastola moja yenye risasi 7 pamoja na risasi za SMG 35.

Baadhi ya wananchi wa Jiji la Tanga wakielezea hatua hiyo wamepongeza vyombo vya usalama kwa jitihada za kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu kutoka maeneo ya nje ya jiji la Tanga kwa kushirikiana na baadhi ya wakazi wa jiji.

13516699_931240120320296_1971963057433150867_n.png

Jeshi.JPG

Silaha walizokutwa nazo.
 
Sielewei, Kila siku wanauawa tu. Kwa nini hakuna hata mmoja anayenusurika ili akashtakiwe? Kwa nini hatusikii askari kauawa katika mapambano? Tena walijuaje hao majambazi ndo walihusika na katika tukio tajwa? Kwa hiyo siku hizi polisi ndio wakamataji, waendesha mashtaka, mahakimu/majaji, na tena watekeleza hukumu (kunyonga). Hapa utawala wa kisheria uko wapi?
 
Wanastahili,ila kuna kitu kinanukia kama extrajudicial excution hapa,
kwamba walikuwa mikononi mwa polisi,wakawachukua kwenda kuwaonyesha walipoficha silaha,kisha ghafla baada ya kuwaonyesha wakataka kutoroka na kuanza kurushiana risisi na polisi,ndo wakauwa.

Something is not adding here.
 
Naona majambia yamenyang'anywa haraka haraka
Hivi mkubwa alisema na majambia nayo YANYANGANYWE haraka-haraka? Au alisema bunduki tu? By the way, yaelekea wakati wanakamatwa hawakuwa na hizo silaha. Si wamesema hizo silaha walikwenda kuwaonyesha porini?
 
Sielewei, Kila siku wanauawa tu. Kwa nini hakuna hata mmoja anayenusurika ili akashtakiwe? Kwa nini hatusikii askari kauawa katika mapambano? Tena walijuaje hao majambazi ndo walihusika na katika tukio tajwa? Kwa hiyo siku hizi polisi ndio wakamataji, waendesha mashtaka, mahakimu/majaji, na tena watekeleza hukumu (kunyonga). Hapa utawala wa kisheria uko wapi?
ndo maana nimesema kinachofanyika sasa ni EXTRA JUDICIAL EXCUTION
 
Wanastahili,ila kuna kitu kinanukia kama extrajudicial excution hapa,
kwamba walikuwa mikononi mwa polisi,wakawachukua kwenda kuwaonyesha walipoficha silaha,kisha ghafla baada ya kuwaonyesha wakataka kutoroka na kuanza kurushiana risisi na polisi,ndo wakauwa.

Something is not adding here.
Mukulu amesharuhusu extrajudicial execution. na alitamka hadharani, wala si suala la kudhania.
 
Hivi mkubwa alisema na majambia nayo YANYANGANYWE haraka-haraka? Au alisema bunduki tu? By the way, yaelekea wakati wanakamatwa hawakuwa na hizo silaha. Si wamesema hizo silaha walikwenda kuwaonyesha porini?
inaonekana walijifungua pingu,wakanyakua silaha na kuanza kuwashambulia askari wetu huku wakijaribu kutoroka
 
Juzi walisema wale waliouwawa mabibo ndio waliohusika na mauaji ya watu nane Tanga,na hawa wengine leo tumaelezwa story hiyo hiyo.Au wameuwawa mabibo wakapelekwa Tanga kwa maonyesho?
 
Sasa hv naona wameamua kuwamaliza tuu wakiwakamata. Mahakamani watakusikia tuu.
 
Wanastahili,ila kuna kitu kinanukia kama extrajudicial excution hapa,
kwamba walikuwa mikononi mwa polisi,wakawachukua kwenda kuwaonyesha walipoficha silaha,kisha ghafla baada ya kuwaonyesha wakataka kutoroka na kuanza kurushiana risisi na polisi,ndo wakauwa.

Something is not adding here.
kwa mara ya kwanza nakuona ukiitumia akili yako productive. tukiacha uchadema na uccm pembeni nchi hii itasonga. pale ambapo makosa yamefanyika tuwe pamoja
 
Kila juhudi inayofanywa na serikali mnapinga! du! mwishowe hata mkisikia baba kabaka mwanae pia mtasema anaonewa na serikali
Siyo kupinga, ni tahadhari tu. Wewe unadhani kwa nini mahakama zipo? Haya mambo ya mtu kupigwa risasi kisha tukatangaziwa alikuwa jambazi, nani atakuwa na uhakika? kama mimi ni askari na siku moja nimekufumania na mke wangu kwa nini nisikutafutie siku mwafaka ya kukunyanganya bunduki yako harakaharaka? (hata kama haumiliki bunduki nitakutafutia)
 
Watu watatu wanaodaiwa kuwachinja watu 8 katika eneo la Kibatini lililopo kata ya Mzizima jijini Tanga wameuawa na Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi katika majibizano ya risasi wakati walipokuwa wakitaka kutoroka baada ya kukamatwa kisha kuwapeleka askari katika pori kuwaonesha silaha aina mbali mbali walizokuwa wamezifukia.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Kamishna Msadizi wa Jeshi hilo nchini Leonard Paul amesema silaha zilizokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na Jambia ambalo limetumika kuwachinja watu hao,SMG mbili, bastola moja yenye risasi 7 pamoja na risasi za SMG 35.

Baadhi ya wananchi wa Jiji la Tanga wakielezea hatua hiyo wamepongeza vyombo vya usalama kwa jitihada za kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu kutoka maeneo ya nje ya jiji la Tanga kwa kushirikiana na baadhi ya wakazi wa jiji.

View attachment 361391
Silaha walizokutwa nazo.
Soma kwa makiiini kisha TAFAKARI. Tunarudi kwa Afande Tibaigana.
 
Back
Top Bottom