Washukiwa 500 waliokamatwa Tanzania kurejeshwa Mozambique kwa ugaidi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,034
23,826
23 November 2020
Maputo, Mozambique

Wapiganaji 516 wa Islamic State waliokamatwa Tanzania kurejeshwa Mozambique

Ni baada ya ziara ya mkuu wa jeshi la Polisi Mozambique kamanda Bernadino Rafael nchini Tanzania wiki iliyopita.

Jumla ya Washukiwa 516 wa kutoka mataifa mbalimbali Afrika wanaoshukiwa kujihusisha na ugaidi ktk jimbo lililopo kaskazini mwa Mozambique kurejeshwa nchini Mozambique toka Tanzania haya yamebainishwa na mkuu wa Jeshi la Polisi la Mozambique (Polícia da República de Moçambique - PRM) comandante Bernardino Rafael.

Mkuu wa Jeshi la Polisi la Mozambique amebainisha hayo kwa gazeti la Noticias la nchini Mozambique kuwa watuhumiwa hao wa Dola ya Kiislam Islamic State wanatoka nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia , Tanzania na DR Congo. Washukiwa hao wa ugaidi wanaojitambulisha kama wanamgambo wa Dola ya Kiislam Islamic State wakifikishwa Mozambique watapelekwa mbele ya vyombo vya sheria nchini humo.

Wana mgambo hao wa Islamic State 516 waliokamatwa Tanzania kutoka mataifa mbalimbali wanatuhumiwa kuendesha mapigano ktk jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique lenye maliasili ya gesi asilia nyingi .

Wanamgambo hao wamesababisha vifo zaidi ya 2,000 na wananchi 500,000 kukimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wa Islamic State hao katika jimbo la Cabo Delgado lenye mji mkuu wa jimbo hilo unaoitwa Pemba.
Source: https://sicnoticias.pt/mundo/2020-1...-500-detidos-na-Tanzania-vao-ser-extraditados

More info :
19 Novembro 2020
Maputo, Mozambique

Saudi Arabia kuisaidia Mozambique kupambana na ugaidi, waziri wa Saudi Arabia azungumza kuelekea mkutano baina ya Afrika na Saudia Arabia Saudi-Africa Summit source : https://www.jornalnoticias.co.mz/in...bia-saudita-disponivel-para-apoiar-mocambique

November 20, 2020
Muidumbe, Mozambique
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Mozambique akiwasili mji wa Muidumbe, baada ya majeshi ya usalama ya Mozambique kuukomboa toka kwa wanamgambo wa Dola ya Kiislamu

Source : Maningue Nice Channel
 
20 Nov 2020
Mtwara, Tanzania

MAKUBALIANO MAZITO YAFIKIWA, KUPAMBANA NA UHALIFU UNAOVUKA MIPAKA


Mkuu wa wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Bernadino Rafael wamekubaliana kufanya operesheni za pamoja kukabiliana na kikundi cha watu wanaofanya uhalifu katika maeneo ya vijiji vya mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo wakati Wakuu hao walipokutana mkoani Mtwara na kufanya kikao kazi cha ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili ambapo wote kwa pamoja wamesema wataendelea kuishirikisha jamii ili kuweza kupata taarifa zitakazosaidia kukomesha mtandao huo wa kihalifu.
Source : Muungwana TV
 
Magaidi 500+? Kisha unawarudiaha tu? Au ni sawa na ile oparesheni iloyofanyika enzi za kikwete na wale wanyarwanda?
 
hao wanamgambo wamekamatwa wakati wa mapigano, ? au wamekamatwa mtaani tu? kwa nini wapelekwe msumbiji wakati wamefanya uhalifu tanzania? mmh
 
watuhumiwa hao wa Dola ya Kiislam Islamic State wanatoka nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia , Tanzania na DR Congo. Washukiwa hao wa ugaidi wanaojitambulisha kama wanamgambo wa Kiislam wakifikishwa Mozambique watapelekwa mbele ya vyombo vya sheria nchini humo.
Hata hao watuhumiwa wenye uraia wa Tanzania wanapelekwa Msumbiji?
 
Hata hao watuhumiwa wenye uraia wa Tanzania wanapelekwa Msumbiji?

Pengine kwa vile wanamgambo hao ni wa Dola nyingine na hawajitambui kiuraia, kiimani na kiitikadi kama wanatoka ktk nchi hizo za kiAfrika ikiwemo Tanzania. Dola yao ipo Cabo Delgado wakakimbilia Tanzania .
 
Mozambique watafute sababu ya haya matukio na kuikomesha

Siasa na dini zisitumike kufanya uhalifu Afrika tutamalizana bure. Viongozi wa dini waambiwe ukweli ili wawahubiri wafuasi wao wasitumike

Tunaitaka afrika yenye amani
 
Kwa kauli ya Kamanda sirro, kunavijana wengi wamekamatiwa njiani mfano kigoma , mwanza wakitokea nchi majirani wakiwa wanaenda kujiunga na hilo kundi so wengi wao hawajui hata kitaya kunafananaje.

Wengine walioshikiliwa nibaadhi ya ambao nyumba zao hazikuteketezwa maana kamanda alieleza haiwezekani magaidi wachome nyumba zaidi ya 100 kwa kuruka ruka baadhi ya nyumba
 
Hongera sana vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Najua hapo ilipigwa recce kali msituni.
Hao majahili walikosea sana kuingia Kitaya, Tanzania.
Nafikiri somo la MKIRU hawakulielewa.
 
Waislam wenzangu tuweni wavumilivu kipindi hiki maana kwa kuwa tuna majina ya akina abdallah, juma, hassan basi tunaweza muda wowote kukumbana na hizi kesi, zitakufika zama mtume (rehma na amani iwe juu yake ) alisema uislamu utakuwa kama kaa la moyo, na leo wale wenye yakin bila shaka munaona hali wa Waislam wenzetu inavyoendelea duniani, burma miaka 3 iliyopita waislam walikuwa wakiuliwa na kufukiwa hai mamia kwa mamia ila halijawa ugaidi, serbia waislam waliuliwa kinyama na wanawake kubakwa halijawa ugaidi, mtume (rehma na amani iwe juu yake )asema tena watakaoishi zama mbele baada ya zama hizi watashuhudia mengi mnooo na kwa kwel tuna shuhudia, je ni nani aliyetayari kukumbatia kaa la MOTO !!View attachment 1633426View attachment 1633427View attachment 1633428View attachment 1633429
Kwamba hao wapiganaji wa Islamic State wanaoua watu wanaonewa kwasababu ya Uislam wao?
 
Hizi dini zinaleta matatizo sana, Kila watu wabaki za dini zao, Waafrika wabaki na dini zao, waarabu pia na wazungu vilevile, kwani zinabeba tabia asili za waanzilishi wa hizo dini. Hasa Africa ikatae kabisa hizi dini za kiarabu na magharibi zinawafanya kuwa watumwa wa akili na pesa.
 
Kwa kauli ya Kamanda sirro, kunavijana wengi wamekamatiwa njiani mfano kigoma , mwanza wakitokea nchi majirani wakiwa wanaenda kujiunga na hilo kundi so wengi wao hawajui hata kitaya kunafananaje.

Wengine walioshikiliwa nibaadhi ya ambao nyumba zao hazikuteketezwa maana kamanda alieleza haiwezekani magaidi wachome nyumba zaidi ya 100 kwa kuruka ruka baadhi ya nyumba
 
Kwa kauli ya Kamanda sirro, kunavijana wengi wamekamatiwa njiani mfano kigoma , mwanza wakitokea nchi majirani wakiwa wanaenda kujiunga na hilo kundi so wengi wao hawajui hata kitaya kunafananaje.

Wengine walioshikiliwa nibaadhi ya ambao nyumba zao hazikuteketezwa maana kamanda alieleza haiwezekani magaidi wachome nyumba zaidi ya 100 kwa kuruka ruka baadhi ya nyumba
Hapa kunatakiwa umakini wa hali ya juu ili watu wasije onewa, kwani nimeona video youtube kwenye vijiji vilivyochomwa huko msumbiji kuna nyumba hazikuguswa kabisa, kwa hio watumie ujuzi wa hali ya juu kutambua wahusika kutoka hapo kwenye hivyo vijiji.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom