Washtakiwa uhujumu uchumi waanza kuomba msamaha.

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,581
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha na kusamehewa wameanza kufanya hivyo kwa kasi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha na kusamehewa wameanza kufanya hivyo kwa kasi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Mahiga ametoa kauli hiyo katika mahojiano na televisheni ya Azam leo Jumanne Septemba 24, 2019.

Amesema DPP, Biswalo Mganga ameanza kupokea maombi hayo kwa kasi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa pendekezo la Rais wa Tanzania, John Magufuli alilolitoa juzi baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua.

Magufuli alitoa siku saba kwa washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha kufanya hivyo huku akiweka sharti kwamba wanaostahili msamaha ni wale watakaokuwa tayari kurudisha fedha walizotakatisha.

“Hapa tunavyozungumza nimetoka kuzungumza na DPP ananiambia maombi yanaingia kwa kasi sana na sasa lazima wafanye uchambuzi.”

“Si suala tu la kutazama kesi moja, lazima kutazama mafaili, kutazama chimbuko lake kwa kushirikiana na idara ya upelelezi,” amesema Balozi Mahiga.

Mganga ambaye pia alihojiwa na televisheni hiyo amesita kuitaja idadi ya watuhumiwa wanaohusika na kusisitiza kuwa idadi yao hatoitaja.

“Akiamua kukaa kule (mahabusu) tutaendelea naye akisema jamani mimi niko tayari kuomba msamaha tutaongea ila kwa hiyo minong’onong’o tuyaache tu.”

“Mshtakiwa mwenyewe au kwa kupitia mawakili wake akiwa mahabusu ataandika barua mwenyewe ili kesho na kesho kutwa asije kuiruka Serikali ndio maana watuhumiwa wenyewe wanaandika,” amesema Mganga.
Mahiga.jpeg
 
Hii kauli ya *kiushabiki* ya Mh Mahiga (Ukizingatia yeye kazi yake ni KUSIMAMIA SHERIA NA KATIBA tu) ina maana gani???

“Akiamua kukaa kule (mahabusu) tutaendelea naye akisema jamani mimi niko tayari kuomba msamaha tutaongea ila kwa hiyo minong’onong’o tuyaache tu.”

----xxx---

NB:

1) Kuna principle kisheria inaitwa "PRESUMPTION OF INNOCENCE" (Everyone is pressumed innocent until proved guilty by a court of law), kila mtu anasadikiwa kua hana HATIA mpaka atakapokutwa na mahakama ana hatia ya kosa ambalo anashtakiwa nalo.

Sasa hii issue ya mtuhumiwa kukubali na kulipa ili apate uhuru wake, inakwenda kinyume na principle za kisheria (Japo baadhi ya nchi sheria zao zinalitambua hili jambo), kwa sheria zetu inakua mtu anatiwa hatiani kabla hata ya mahakama kujiridhisha kwamba ana hatia, pia hii inaweza ikatumika kama silaha ya kukomoa/kufilisi/kuwaadhirisha raia ambao watakua wanapingana na serikali (Mfano Erick Kabendera), ukizingatia nchi yetu hali iliokua nayo kidemokrasia.

2) Watu kujazwa CRIMINAL RECORD (Kua na historia ya uhalifu), hii itawaathiri hata kuwekeza nje ya nchi au kuomba ajira nje ya nchi na ndani ya nchi.

3) Haki ya kikatiba ya UHURU (FREEDOM), itakua sio haki ya kila mtu KIKATIBA tena, haki hii itakua ya KUNUNULIWA.

*** Pia watu (hasa matajiri) wajiandae, kila atakae takiwa kutoa mchango katika hela zake, akigoma tu anaswekwa ndani kwa kesi ya uhujumu uchumi mpaka akubali kibano!!!
 
A
Hii kauli ya *kiushabiki* ya Mh Mahiga (Ukizingatia yeye kazi yake ni KUSIMAMIA SHERIA NA KATIBA tu) ina maana gani???

“Akiamua kukaa kule (mahabusu) tutaendelea naye akisema jamani mimi niko tayari kuomba msamaha tutaongea ila kwa hiyo minong’onong’o tuyaache tu.”

NB Pia watu (hasa matajiri) wajiandae, kila atakae takiwa kutoa mchango katika hela zake, akigoma tu anaswekwa ndani kwa kesi ya uhujumu uchumi mpaka akubali kibano!!!
Acha matajiri wachangie miradi ya maendeleo ili tufaidi sote, tatizo liko wapi?.
 
Ni mtihani mkubwa sana!
Kwamba tuhuma tu zitoshe?
Kama sijaelewa vile ?!
Kaka yangu serikali imeshindwa kuwapata na hatia. Sasa inataka wajikaange wenyewe. Wewe Akilinjema tulikua tunakutuhumu kutuinia elfu kumi lkn hatuna uhakika maana ulibambikiwa. Sasa utaamua. Uendelee kuozea jela au ukiri kwamba uliiba ili utulipe tujenge madaraja na wewe ukale pasipo na kunguni
 
Haya yote yanafanyka under duress, undue influence na huko Jiwe akisha "kufa" , watakwenda mahakamani kudai haki zao!

Coercion to effect an unwilling person's agreement to a transaction. It may take the form of a (1) compulsive act, (2) threat that causes fear, or (3) use of moral or social pressure to overpower the will of the individual. Agreements entered into, or testaments signed under, duress are judged illegal and invalid. See also coercion and undue influence
 
Acha walipe tufanye maendeleo, wakizidai mbeleni tutawalipa kidogo kidogo.
 
Ni mtihani mkubwa sana!
Kwamba tuhuma tu zitoshe?
Kama sijaelewa vile ?!
Fahamu kwamba mara nyingi mtuhumiwa anauelewa ukweli juu ya kesi yake, na mara nyingi anashauriwa na wakili wake jinsi anavyoiona kasi kisheria.

Iwapo mtuhumiwa atajiridhisha kwamba hapa sitoki na wakili akamshauri kuwa jiandae kisaikolojia kuvaa KAROTI why not, asilipe yakaisha.

Kuna mzee baba kiongozi serikalini tena waziri alituambiaga tutakula nyasi ilimradi ndege ya raisi inunuliwe akaingia choo kisicho chake, akakamatwa akakosa dhamana wakati wa kwenda mahakamani akaoneka na KANDAMBILI MBOVU ZA BLUE NA NYEKUNDU.

Mle MUNG'ANDA sio pouwa hata kidogo.
 
Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha na kusamehewa wameanza kufanya hivyo kwa kasi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha na kusamehewa wameanza kufanya hivyo kwa kasi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Mahiga ametoa kauli hiyo katika mahojiano na televisheni ya Azam leo Jumanne Septemba 24, 2019.

Amesema DPP, Biswalo Mganga ameanza kupokea maombi hayo kwa kasi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa pendekezo la Rais wa Tanzania, John Magufuli alilolitoa juzi baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua.

Magufuli alitoa siku saba kwa washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi walio tayari kuomba msamaha kufanya hivyo huku akiweka sharti kwamba wanaostahili msamaha ni wale watakaokuwa tayari kurudisha fedha walizotakatisha.

“Hapa tunavyozungumza nimetoka kuzungumza na DPP ananiambia maombi yanaingia kwa kasi sana na sasa lazima wafanye uchambuzi.”

“Si suala tu la kutazama kesi moja, lazima kutazama mafaili, kutazama chimbuko lake kwa kushirikiana na idara ya upelelezi,” amesema Balozi Mahiga.

Mganga ambaye pia alihojiwa na televisheni hiyo amesita kuitaja idadi ya watuhumiwa wanaohusika na kusisitiza kuwa idadi yao hatoitaja.

“Akiamua kukaa kule (mahabusu) tutaendelea naye akisema jamani mimi niko tayari kuomba msamaha tutaongea ila kwa hiyo minong’onong’o tuyaache tu.”

“Mshtakiwa mwenyewe au kwa kupitia mawakili wake akiwa mahabusu ataandika barua mwenyewe ili kesho na kesho kutwa asije kuiruka Serikali ndio maana watuhumiwa wenyewe wanaandika,” amesema Mganga.View attachment 1215468
Sasa ushahidi kwa miaka yote hii ya nenda rudi ya mahakamani uko wapi, na ukijipindua kuomba msamaha tu ujuwe umejiangushia jumba bovu mwenyewe
 
Kuna watu wamezaliwa na ROHO MBAYA kupitiliza, halafu hao hao wanasema eti "Kufa masikini, ni dhambi" wakati wanaombea watu wafilisike bila sababu.
Uliwasaidia kuzitafuta hizo pesa?
Acha kuandika kijinga,watu wengine wanajitesa ili wawe matajiri halafu wewe uje ufaidike kizembe?
 
Fahamu kwamba mara nyingi mtuhumiwa anauelewa ukweli juu ya kesi yake, na mara nyingi anashauriwa na wakili wake jinsi anavyoiona kasi kisheria.

Iwapo mtuhumiwa atajiridhisha kwamba hapa sitoki na wakili akamshauri kuwa jiandae kisaikolojia kuvaa KAROTI why not, asilipe yakaisha.

Kuna mzee baba kiongozi serikalini tena waziri alituambiaga tutakula nyasi ilimradi ndege ya raisi inunuliwe akaingia choo kisicho chake, akakamatwa akakosa dhamana wakati wa kwenda mahakamani akaoneka na KANDAMBILI MBOVU ZA BLUE NA NYEKUNDU.

Mle MUNG'ANDA sio pouwa hata kidogo.
Alikaa mahabusu miaka minne, na kesi iliishaje?
 
Back
Top Bottom