Washtakiwa kwa kumdhalilisha Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washtakiwa kwa kumdhalilisha Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kilimasera, Nov 4, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwalimu na mwanafunzi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, mkoani Kilimanjaro wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi na kuchapisha matoleo ya aibu kwenye Mtandao wa Facebook dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

  Kesi hiyo namba 677/2010 inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Simon Kobelo, ambapo washtakiwa hao walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu John Nkwabi kutokana na Hakimu Kobelo kutokuwepo mahakamani.

  Washtakiwa hao ni Mwalimu Frednand Urio (25) ambaye ni mwalimu wa eneo la Marangu Komelo na mwanafunzi Daniel Mataji au RobinDaniel ni mkazi wa KDC Kiborlon.

  Wakili Mwandamizi wa Serikali,Veritas Mlay, akiwasomea washtakiwa hao mashtaka hayo, alidai shtaka la kwanza la Urio ni kuchapisha matoleo ya aibu dhidi ya Rais Kikwete kinyume na kifungu namba 175(1) (a) ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Alidai kuwa Urio kati ya Machi Mosi na Septemba mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete.

  Mlay alidai kuwa mshtakiwa huyo pia anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu namba 32 (1) cha sheria ya Magazeti namba 229.

  Alidai kuwa kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, mshtakiwa huyo alisambaza picha zakumdhalilisha Rais Kikwete.

  Katika shtaka la tatu alidai kuwa mshtakiwa Daniel ambaye ni mwanafunzi anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu hichohicho cha Sheria ya Magazeti.

  Alidai mshtakiwa huyo kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete kwenye mtandao wa Facebook.

  Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo na ambapo Hakimu Nkwabi aliwaelezamasharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili na Sh.million mbili.

  Washtakiwa hao walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na hivyo kwenda mahabusu hadi Novemba 17, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.

  source nipashe
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Isije ikaamia JF hii pale MOD atakapoambiwa ebu tuambie Njowepo ndo nani?

  But watu apa wako confident and determined on what they post
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
 4. KasomaJr

  KasomaJr JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wakalale mbele huko, na waje waanze na mimi...lazima ni mle mtu pua ndo kesi iendelee vizuri...pambavu kama si pumbavu
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Wamshraki Malaria sugu kwa kujipendekeza kwa jk kana kwamba ni mke wa 3 wa jk.
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hii kali...hivi tuneelekea wapi?? mbona hawamkamati SHAMTE na SMS zake alizowatukana viongozi wetu mbele ya watanzania zaidi ya milioni 15
   
Loading...