Washtakiwa kwa kumdhalilisha Kikwete

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,876
Imeandikwa na Salome Kitomary
4th November 2010

Mwalimu na mwanafunzi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, mkoani Kilimanjaro wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi na kuchapisha matoleo ya aibu kwenye Mtandao wa Facebook dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

Kesi hiyo namba 677/2010 inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Simon Kobelo, ambapo washtakiwa hao walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu John Nkwabi kutokana na Hakimu Kobelo kutokuwepo mahakamani.

Washtakiwa hao ni Mwalimu Frednand Urio (25) ambaye ni mwalimu wa eneo la Marangu Komelo na mwanafunzi Daniel Mataji au RobinDaniel ni mkazi wa KDC Kiborlon.

Wakili Mwandamizi wa Serikali,Veritas Mlay, akiwasomea washtakiwa hao mashtaka hayo, alidai shtaka la kwanza la Urio ni kuchapisha matoleo ya aibu dhidi ya Rais Kikwete kinyume na kifungu namba 175(1) (a) ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai kuwa Urio kati ya Machi Mosi na Septemba mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete.

Mlay alidai kuwa mshtakiwa huyo pia anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu namba 32 (1) cha sheria ya Magazeti namba 229.

Alidai kuwa kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, mshtakiwa huyo alisambaza picha zakumdhalilisha Rais Kikwete.

Katika shtaka la tatu alidai kuwa mshtakiwa Daniel ambaye ni mwanafunzi anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu hichohicho cha Sheria ya Magazeti.

Alidai mshtakiwa huyo kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete kwenye mtandao wa Facebook.

Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo na ambapo Hakimu Nkwabi aliwaelezamasharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili na Sh.million mbili.

Washtakiwa hao walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na hivyo kwenda mahabusu hadi Novemba 17, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.

CHANZO: Nipashe
 
Yaanik hizo nchi zenye kukandamiza demokrasia ni taabuj mpaka basi, usikute hata hakimu mwenyewe hajui facebook ni kitu gani. Sasa huyo JK wao anatafuta nini fb kama hataki kudhalilishwa, nani alisema fb ni ridicule-proof?
 
KIKWETE.jpg
 
Ni kesi za kutaka kutisha wananchi kwani Kikwete ndiye aliyelalamika au ni kutokana na kiherehere cha hao Polisi? Hizi ndizo kesi wamekuwa wanamfungulia Mtikila kila siku na anawashinda.
 
Hivi kweli ninahitaji kuchapisha kitu ili kumdalilisha JK? Sidhani, maana ninachohitaji ni kumwambia tu mtu "angalia hali ya uongozi nchini na Tanzania".
 
Hivi kweli ninahitaji kuchapisha kitu ili kumdalilisha JK? Sidhani, maana ninachohitaji ni kumwambia tu mtu "angalia hali ya uongozi nchini na Tanzania".

siku hizi tenda zinaombwa kwa kufuata sheria ya Manunuzi sio enzi zile mkikutana Himo, kibororoni mngawana tenda za serikali kama makopo ya mbege!
 
Hivi sheria ya magazeti inadhibiti hadi facebook?

kesi itasomwa tena nov?au mwandishi kakosea?

Hivi kweli ninahitaji kuchapisha kitu ili kumdalilisha JK? Sidhani, maana ninachohitaji ni kumwambia tu mtu "angalia hali ya uongozi nchini na Tanzania".


Mimi nadhani sheria ingeenda mbali zaidi...Rais na viongozi wengine pia wakijidhalilisha wakamatwe, wahukumiwe na wafungwe....!!
 
Wacha wafundishwe adabu na serikali kama Wazazi wao wameshindwa
 
Tusirudi nyuma tupambane mpaka haki yetu ipatikane,hata south africa walipata shida sana,vitisho .Lakini walisimama mpaka leo hii wapo huru.Hakuna kurudi nyuma wakati unapotetea haki yako na ya taifa lako.Mungu ibariki harakati hizi.uwe nyuma yetu.amen
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom