Washtakiwa kwa kumdhalilisha Kikwete facebook

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
By Salome Kitomary
4th November 2010

Mwalimu na mwanafunzi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, mkoani Kilimanjaro wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi na kuchapisha matoleo ya aibu kwenye Mtandao wa Facebook dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

Kesi hiyo namba 677/2010 inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Simon Kobelo, ambapo washtakiwa hao walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu John Nkwabi kutokana na Hakimu Kobelo kutokuwepo mahakamani.

Washtakiwa hao ni Mwalimu Frednand Urio (25) ambaye ni mwalimu wa eneo la Marangu Komelo na mwanafunzi Daniel Mataji au RobinDaniel ni mkazi wa KDC Kiborlon.

Wakili Mwandamizi wa Serikali,Veritas Mlay, akiwasomea washtakiwa hao mashtaka hayo, alidai shtaka la kwanza la Urio ni kuchapisha matoleo ya aibu dhidi ya Rais Kikwete kinyume na kifungu namba 175(1) (a) ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai kuwa Urio kati ya Machi Mosi na Septemba mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete.

Mlay alidai kuwa mshtakiwa huyo pia anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu namba 32 (1) cha sheria ya Magazeti namba 229.

Alidai kuwa kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, mshtakiwa huyo alisambaza picha zakumdhalilisha Rais Kikwete.

Katika shtaka la tatu alidai kuwa mshtakiwa Daniel ambaye ni mwanafunzi anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu hichohicho cha Sheria ya Magazeti.

Alidai mshtakiwa huyo kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete kwenye mtandao wa Facebook.

Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo na ambapo Hakimu Nkwabi aliwaelezamasharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili na Sh.million mbili.

Washtakiwa hao walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na hivyo kwenda mahabusu hadi Novemba 17, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.
SOURCE: NIPASHE
 
Bado hatuna cyber law Tanzania, wakipata wakili mzuri, hakuna kesi hapo!, wanawaonea bure, tena huyo wakili akiwapata waliosambaza hizo picha from fb na kuziprint ndio wakosaji!
 
Bado hatuna cyber law Tanzania, wakipata wakili mzuri, hakuna kesi hapo!, wanawaonea bure, tena huyo wakili akiwapata waliosambaza hizo picha from fb na kuziprint ndio wakosaji!
The Following User Says Thank You to Pasco For This Useful Post:

Mchukia Fisadi (Today)​
 
Back
Top Bottom