Washtakiwa Dar wavua nguo na kujipaka kinyesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washtakiwa Dar wavua nguo na kujipaka kinyesi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Mar 26, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  WASHITAKIWA watatu jana walifanya kituko mahakamani kwa kuvua nguo na kubaki uchi huku wakiwa wamejipaka kinyesi kibichi cha binadamu na kisha kutoroka kabla ya kukamatwa tena baadaye.

  Tukio hilo lilitokea saa 6:45 mchana, baada ya hakimu Richard Kabate wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kuwaachia huru washtakiwa hao kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 225.

  Washtakiwa hao waliachiwa mbele ya Mwendesha Mashtaka, Mohamed Kilongo.

  Kifungu hiko kinaelekeza kuwa mshtakiwa anaweza kukamatwa na kufikishwa tena mahakamani baada ya kuachiwa huru ama kwa dhamana ama msamaha, kama upande wa mashtaka utaona ana kesi ya kujibu.

  Mwandishi wa habari hii alishuhudia washtakiwa hao, Rashid Salum, Hamza Abdallah na Juma Mathias waliokuwa mahabusu wakisubiri gari ya polisi, liwapeleke katika Kituo cha polisi Magomeni, kuandaliwa mashtaka upya, wakitoroka.

  Baada ya gari ya polisi kuwasili mahakamani washtakiwa hao wakiwa uchi huku wakiwa wamebeba kopo lenye kinyesi cha binadamu, walimwagia uchafu huo koplo Peter na kupata nafasi ya kukimbia.

  Mwingine ambaye alikuwa amebeba kinyesi cha binadamu kwenye mfuko, alijimwagia mwili kama njia ya kujihami asikamatwe na wananchi waliokuwepo mahakamani.

  Askari mmoja wa Magereza alipofyatua risasi juu kuashiria hali ya hatari na idadi ya magari aina ya defender ya kiwa na askari wenye silaha, waliminika mahakamani huku askari wakipewa maelekezo ya kiutendaji.

  Askari hao walitawanyika na baada ya takribani dakika 30, walirejea katika eneo la mahakama wakiwa na mshtakiwa mmoja ambaye kabla ya polisi kumtia tena nguvuni, wananchi wenye hasira walishaanza kumwadabisha.
  Wengine wawili waliletwa wakiwa katika gari ya polisi Defender huku mmoja akiwa amelowa damu sehemu ya kichwani na habari zilisema walikutwa katika eneo la Mwananyamala Bwawani.

  SOURCE: MWANANCHI
   
 2. gwambala

  gwambala Member

  #2
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  he he he hao walishaamua kama noma iwe noma ndo maana walianza kujipaka mavi kwanza
   
 3. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hahah haaaa... hii kali niliiona jana TBC nikabaki sina mbavu.
   
Loading...