Washitakiwa watatu wa TRA wanaohusika na utoroshaji makontena wapewa dhamana

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
attachment.php


Mahakama kuu ya Tanzania imeridhia dhamana kwa washitakiwa watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA wanaokabiliwa na mashitaka ya kutoa makontena 329 bandarini bila kulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.

Maamuzi hayo ya mahakama kuu ya Tanzania yametokana na ombi lililowakilishwa mahakamani hapo na washtakiwa watatu wakiongozwa aliyekuwa Kamishina wa Forodha wa TRA Bw Tiagi Masamaki.

Jaji wa mahakama hiyo Bi Wilfrida Koroso, alisema dhamana kwa washitakiwa hao watatu iko wazi kama watatimiza masharti sita yakiwemo ya kulipa hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja huku pia wakitakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiri na kutakiwa kuwa na wadhamini watakaokuwa na uwezo wa kusaini hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.


attachment.php

Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa Naibu Kamishna wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki (Kulia) akiwa na wenzake aliyekuwa Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Habibu Mponezya na Bulton Mponezya wakiwa katika Mahakama Kuu Tanzania jijini Dar es Salaam jana wakisomewa shtaka linalowakikabili la makosa ya jinai na uhujumu uchumi.

Chanzo:
mpekuzihuru.com
 

Attachments

  • c.jpg
    c.jpg
    94.3 KB · Views: 1,453
  • b.jpg
    b.jpg
    103.4 KB · Views: 1,974
Hii inathibitisha ile thred inayosema mh.rais adhibitiwa na kamati kuu ya ccm. Ambapo mzee wa msoga alisema isingekuwa watu hao basi chama kisingeweza gharama za kampeni. Wewe uliona wapi kesi ya uhujumu uchumi inapewa dhamana??


mahakama kuu ya tanzania imeridhia dhamana kwa washitakiwa watatu wa mamlaka ya mapato tanzania tra wanaokabiliwa na mashitaka ya kutoa makontena 329 bandarini bila kulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.


Maamuzi hayo ya mahakama kuu ya tanzania yametokana na ombi lililowakilishwa mahakamani hapo na washtakiwa watatu wakiongozwa aliyekuwa kamishina wa forodha wa tra bw tiagi masamaki.

Jaji wa mahakama hiyo bi wilfrida koroso, alisema dhamana kwa washitakiwa hao watatu iko wazi kama watatimiza masharti sita yakiwemo ya kulipa hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja huku pia wakitakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiri na kutakiwa kuwa na wadhamini watakaokuwa na uwezo wa kusaini hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.


Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa naibu kamishna wa mamlaka ya mapato tanzania (tra), tiagi masamaki (kulia) akiwa na wenzake aliyekuwa meneja wa kitengo cha huduma kwa wateja, habibu mponezya na bulton mponezya wakiwa katika mahakama kuu tanzania jijini dar es salaam jana wakisomewa shtaka linalowakikabili la makosa ya jinai na uhujumu uchumi.
 
Ishi na watu vizuri kwakuwa huijui kesho yako.
Ahsante
 
du ukisikia sura mbuzi ni hiyo hapo kulia...huyu sidhani kama anaguswa na matatizo ya watanzania!
 
Nashangaa mods kwa kuondoa thread yangu juu ya rsi kudhibitiwa na kamati kuu ya ccm.simunaona wahujumu uchumi wanarudi mtaani kirahisi kabisa
 
Kumbe kuna mazimba wana sura kama wanywa banana.
Kweli chapaa hainunui kila kitu.
 
Magufuli atafanya vizuri baada ya Jakaya kuachia uenyekiti wa CCM.... Naona jinsi Magufuli anavyozungukwa na kundi la Jakaya ndani ya chama. Na kwa bahati mbaya Magufuli hakijui chama vizuri
 
Back
Top Bottom