Washington yaomba kuachiliwa huru mara moja raia wawili wa Canada nchini China

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,872
Marekani imetoa wito wa kuachiliwa 'huru mara moja' raia wawili wa Canada wanaozuiliwa nchini China baada ya kushutumiwa kufanya kazi za kijasusi nchini humo.

Marekani inasema shutma za China dhidi ya raia hao wa Canada ni za "kisiasa na hazina msingi wowote".

"Marekani ina wasiwasi mkubwa juu ya uamuzi wa Jamhuri ya Watu wa China wa kuwafungulia rasmi mashitaka raia wa Canada, Michael Kovrig na Michael Spavor," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema katika taarifa

China iliwafungulia mashtaka raia hao wa Canada kwa madai ya kufanya kazi za kijasusi nchini humo, miezi 18 baada ya kukamatwa na kuzua mvutano wa kidiplomasia kati ya Beijing na Ottawa

Mwanadiplomasia wa zamani Michael Kovrig na mfanyibiashara Michael Spavor, walikamatwa muda mfupi baada ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei Meng Wanzhou kutiwa mbaroni na kuonekana kama hatua ya China kulipiza kisasi.

Mahakama ya Juu nchini China imethibitisha kuanza kusikiliza kesi dhidi ya wawili hao kwa madai ya kufanya kazi za kijasusi na kuiba siri za serikali.

Hatua hii pia imekuja baada ya Mahakama nchini Canada kuamua kuwa Mkurugenzi huyo wa kampuni ya Huawei atasafirishwa nchini Marekani kufunguliwa mashataka kwa madai kuwa kampuni hiyo ilikiuka masharti ya vikwawo dhidi ya Iran.

Kesi hizi mbili zimeendelea kuhatarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili na hata kuyumbisha shughuli za kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.
 
Back
Top Bottom