Washington Post: Ukoo wa Aal Saud ulimpa zawadi 'feki' Donald Trump

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Washington Post: Ukoo wa Aal Saud ulimpa zawadi 'feki' Donald Trump

Oct 12, 2021 02:30 UTC

Gazeti la Washington Post la nchini Marekani limefichua kuwa, familia ya kifalme ya Saudi Arabia ilimpa Donald Trump zawadi bandia wakati alipotembelea Saudia kwa mara ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Kwa ujibu wa gazeti hilo maarufu la Marekani, familia ya kifalme ya Saudi Arabia ilimpa Donald Trump na msafara wake makumi ya zawadi za thamani vikiwemo vijambakoti yaani vizibao vitatu vilivyofumwa kwa ngozi ya chui mweupe, jaketi la chui madoa na jambia lenye mkono wa pembe ya ndovu.

Baada ya kupewa zawadi hizo, wakili wa Ikulu ya Marekani, White House alikusudia kuingiza jaketi la chui madoa na jambia lenye mkono wa pembe ya tembo kwenye vitu visivyokubalika kutokana na kutengenezwa na viungo vya wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka. Hata hivyo Donald Trump aliamua kufanya siri na kuficha kabisa kupokea zawadi hizo.

Mfalme wa Saudi Arabia akimpa mkono mke wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump mjini Riyadh.

Katika siku za mwishoni mwa kuweko Trump huko White House, suala hilo lilifufuliwa upya na zawadi hizo zilikabidhiwa kwa Idara ya Huduma za Wanyama Pori nchini Marekani. Idara hiyo nayo iliamua kuzuia zawadi hizo kutokana na kutumiwa viungo vya wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka.

Cha ajabu ni kuwa, baada ya idara hiyo kufanya uchunguzi wa kina na wa kiutaalamu, imegundua kuwa zawadi hizo ni 'feki' na hazikutumiwa viungo halisi vya wanyama hao kama alivyodanganywa Donald Trump.

Haijajulikani iwapo Wafalme wenyewe wa Saudia walikuwa wanajua kuwa zawadi hizo ni bandia au na wao nao waliuziwa bidhaa feki?

Maafisa wa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington wamekataa kusema chochote kuhusu suala hilo.

4bve2c52d658691r16z_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom