Washindwa kulimia matrekta kisa hayajazinduliwa na Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washindwa kulimia matrekta kisa hayajazinduliwa na Rais

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.  Wakulima 417 katika bonde la mpunga la Mtwango, Zanzibar, wamekwama kutumia materekta mapya katika msimu wa kilimo unaomalizika mwezi huu kwa sababu hayajazinduliwa na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
  Uchunguzi wa Nipashe umegundua kwamba matrekta hayo yaliwasili Zanzibar tangu Julai mwaka jana kutoka Italia.
  Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wakulima walisema wamekwama kutumia matrekta hayo baada ya watendaji wa Wizara ya Kilimo kudai hayawezekani kutumika kabla ya kuzinduliwa na Rais.
  Walisema kwamba msimu wa Kilimo umeanza tangu mwezi Machi mwaka huu na mwisho wa mwezi huu ndio mwisho wa kupanda jambo ambalo litaathiri kalenda ya kilimo ya mwaka huu
  Aidha walisema kutokana na kuchelewa kulima mashamba yao tayari wameanza kupata wasiwasi wa kushindwa kuvuka malengo waliyokuwa wamejipangia katika msimu wa kilimo mwaka huu
  “Tumeambiwa kwamba sasa matrekta haya yatazinduliwa na Mheshimiwa Rais Juni 6, wakati mwisho wa mwezi huu ndio mwisho wa kupanda,” alisema mkulima mmoja toka katika bonde hilo la Mtwango.
  “Toka kuanza kwa msimu wa kilimo mwaka huu, tumekuwa tukitumia matreka mawili ya mtu binafsi na gharama zake ni kubwa tofauti na matrekta ya serikali,” aliongeza.
  Rais wa Jumuiya ya wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda Zanzibar, (ZNCCIA), Abdalla Abass Omar, alisema hana taarifa kuhusu kutotumika kwa matrekiana na suala hilo na kuahidi kufuatilia kwa watendaji serikalini.
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira Zanzibar, Khatib Suleiman Bakar hakuwa tayari kuzungumizia swala hilo na kutaka atafutwe Kamishina wa Kilimo Zanzibar .  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...