Washindi wakabidhi kombe kwa wapinzani wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Washindi wakabidhi kombe kwa wapinzani wao

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by MAMMAMIA, Jun 21, 2011.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Katika hali isiyo ya kawaida, washindi wa ubingwa wa futbol kwa watoto wa miaka 11, wameamua kukabidhi kombe kwa washindani wao ambao kwa kauli moja wamekubali kuwa washindani wao walistahiki kombe hilo kuliko wao.

  Tukio hili la kipekee limetokea nchini Hispania ambako kulikuwa kunafanyika mashindano ya kugombania kombe la taifa la mpira wa miguu kwa watoto wa miaka 11. Katika mechi ya mwisho, timu za Seville na EspaƱol zilipambana vikali. Dakika za kawaida zilimaliza bila mshindi hivyo muda akaongezwa na bado matokeo yalikuwa 0-0. Ndipo ilipoamuliwa zipigwe penalti na Seville wakashinda 5 dhidi ya 4 za wapinzani wao.

  Jambo la kushangaza, washindi waliamua kombe hilo wapewe wapinzani wao kwa madai kuwa ingawa wao wameshinda mchezo lakini kombe lilipaswa kwenda kwa wapinzani wao ambao walicheza vizuri kuliko wao.

  Tutarajie siku moja kutokea kama hili baina ya Simba na Yanga, CCM na CDM, kwa mfano?
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Mhh waafrika ubinafsi umezidi!kila mtu anawaza tumbo lake tuu
   
Loading...