Washindi Tuzo za Muziki Tanzania 2021, heshima kwa Rais Samia, Diamond, Ruge, Mabeyo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,264
5,355
Tuzo za Muziki za Tanzania (TMA) 2021 zinatolewa usiku huu wa Aprili 2, 2022 ikiwa ni miaka 7 imepita bila uwepo wa tuzo kama za muziki kama hizo Nchini Tanzania.

TUZO ZA HESHIMA
Shughuli inafanyika kwenye kwenye Ukumbi wa JNICC Dar es Salaam, watu watano wa kwanza kupewa tuzo ya heshima ni Rais Samia Suluhu, Mkuu wa Majeshi Mabeyo, Marehemu Ruge Mutahaba, Marehemu Bibi Kidude na Mwimbaji Diamond Platnumz.

SERIKALI IMEGHARAMIA TUZO 95%
Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohamed Mchengerwa ambaye ndiye mgeni rasmi katika shughuli za utoaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2021 amesema tuzo hizo zimegharamiwa na Serikali kwa takribani asilimia 95.

Akizungumza katika tuzo hizo, Waziri Mchengerwa amesema ni jambo jema kuwa na tuzo kwa mara nyingine baada ya kuwa imepita miaka saba bila kuwa na tuzo nchini na kueleza kwamba mtu wa kwanza anayestahili pongezi, ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mchengerwa amesema Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kutoa msukumo wa kufanyika kwa tuzo hizo na kuitaka wizara isimamie kikamilifu haki na stahiki za wasanii nchini.
WASHINDI WA TUZO ZA MUZIKI

Tuzo ya Muigizaji Bora wa Video za Muziki wa Kike

Fevushka

Tuzo ya Muigizaji Bora wa Video za Muziki wa Kiume
Seleman Masenga

Dansa Bora wa Kike wa Mwaka
Baby Drama

Tuzo ya Dansa Bora wa Kiume
Culture Centre

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Asili wa Kike
Sholinda Kilasi

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Asili wa Kiume
Msafiri Zawose

Tuzo ya Wimbo Bora wa Asili wa Mwaka
Asili Yetu - Sholo Mwamba Ft Wanne Star

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike wa Taarab
Khadija Yusuph

Tuzo ya Msanii wa Bora wa Kiume wa Taarab
Mzee Yusuph

Tuzo ya Wimbo Bora wa Taarab
Msinifokee – Jahazi Modern Taarab

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Raggae/DanceHall wa Kike
Dipper Rato

Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Raggae/DanceHall
Baddest 47

Tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Raggae/DanceHall
Unaota - Baddest 47

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Dansi wa Kike
Luiza Mbutu

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Dansi wa Kiume
Charles Baba

Tuzo ya Wimbo Bora wa Dansi/Rhumba/Zouk
Penzi - Twanga Pepeta

Tuzo ya Msanii Bora wa Singeli wa Kike
Snura

Tuzo ya Msanii Bora wa Singeli wa Kiume
Sholo Mwamba

Tuzo ya Wimbo Bora wa Singeli
Asili Yetu - Sholo Mwamba

Tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Kike
Saraphina

Tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Kiume
Harmonize

Tuzo ya Wimbo Bora Shirikisho wa Mwaka
Loyalty - Darassa Ft Marioo & Nandy

Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka
Alikiba

Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka
Profesa Jay

Tuzo ya Director Bora wa Mwaka
Hans Cana

Tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka
Only One King - Alikiba

Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Chaguo la Watu
Nandy

Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Chaguo la Watu
Alikiba

Tuzo ya Msanii Bora Afrika Mashariki
Alikiba

Tuzo ya Msanii Bora Kutoka Kusini mwa Afrika
Sho Madjozi

Tuzo ya Msanii Bora Kutoka Afrika Magharibi
Davido

Tuzo ya Wimbo Bora wa Kushirikiana Afrika
Attitude - Harmonize

Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Singeli
Kenny

Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Muziki wa Hip Hop
S2Kizzy

Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Zouk/Rhumba/Dansi
Erasto Mashine

Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Bongo Fleva
Mr T Touch

Tuzo ya Msanii Bora Chipukizi
Sarafina

Tuzo ya Msanii Bora Chipukizi wa Kiume
Rapcha

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Hip Hop wa Kike
Chemical

Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka
Young Lunya

Tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop
Mbuzi - Young Lunya

Tuzo ya Msanii Bora wa Bongo Fleva wa Kike
Nandy

Tuzo ya Msanii Bora wa Bongo Fleva wa Kiume
Marioo

Tuzo ya Wimbo Bora wa Bongo Fleva
Bia Tamu - Marioo

Tuzo ya Video Bora ya Mwaka
Salute - Alikiba

Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike wa Mwaka
Nandy

Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka
Harmonize


:::::::: Utoaji tuzo umekamilika saa 9:05 Usiku wa kuamkia Aprili 3, 2022.
 
Tuzo ni jambo zuri,linawapa motivation.........ila Kila dakika kumtaja Rais inachosha sana......sifa zinazidi kiasi yaleyale ya JPM......Yaani viongozi wa sasa hawawezi kujenga hoja bila kumtaja mkuu wa nchi....kumtaja si vibaya ila jengeni hoja basi hata kidogo........
 
Magufuli kawafufundisha hata mobutu seseko kuku ngwendu wa zabanga nae alipenda kuimbwa na wanamuziki wa Kongo bila kufanya hvyo huu mziki wenu na Sanaa yenu siyo kitu

Ccm wameona bila wasanii mikutano yao haitanoga kbsa so wameamua kwa kudhamiria kweli kweli kuekeza kwa wasaanii ili waendele kula kwa urefu wa kamba zao

Mpk wameundiwa federation kusudi waimbe ila wakumbuke kuwa lzm uwe ccm. Mziki wako utalipa vingivyo utakuwa kweny list ya wasani wasio na mafanikio kimziki ukiwa uko upande wa pili wa vidole viwili juu itakula kwako


Umeona kbsa mpk timu za mpira siasa zinaingizwa kumsifia rais wa nchi kwa mwak mmoja tu ya madudu yake aliyoyafanya toka achukue kiti toka kwa late CEO ikumbukwe kuwa siyo wachezaji wote Ni ccm Wal kumkubali rais hyu Ni uhuni huu

Sas kila msani akipnda nikumshukuru rais tu na kusema Kaz iendelee hawajui kuwa kufika Happ ni mungu tu Sasa kila saa mtu jinga kbsa linaanza kumshukuru rais badal kumpa mungu utukufu kwa kushinda tozo hzo za michongo

Stupid ach nilale mnk hata celewi elewi kinachoendelea HV Sasa dhid ya kampuni yetu hii pendwa
 
Sisikii Taarab sana siku hizi,kumbe bado watu wanapata tuzo kwenye huo muziki,Matamasha ya Taarab yapo wapi siku hizi? nimemiss mziki wa mwambao.
 
Watanzania wanapenda kuishi kwa kujipendekeza
Hao wasani ina maana maproducer wao hawana maana

Ova
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom