Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

mkuu Omutwale kuna laana, laana ya manung'uniko ya wazalendo wa nchi hii inawatafuna CCM na washirika wake. kila mmoja amekuta akizamisha jahazi zaidi pale anapofikiri anapolirukia bila kujua kua analiongezea uzito. wameshikwa na upunguani hawajui kua inapaswa kujitosa na kupiga mbizi ili kujinusuru, vinginevyo watazama nalo.
 
Bado najiuliza kwa nini "washika mipini" (Spika, Majaji, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri, n.k) kwa maksudi wanachukua maamuzi ya kusiliba kaburi la ccm? Hakuna hata mmoja anajifunza kutokana na makosa yake ya awali au ya mtangulizi wake!


Hivi kuna upya gani katika neno "UDHAIFU" lililosemwa na Mnyika leo Bungeni? Mbona watu wengi sana ikiwemo viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa wamelisema na kulirudia neno hili na wakilihusisha na Taasisi ile ile (Rais Kikwete) bila kuchukuliwa hatua yoyote?

Juzi Prof. Lipumba kasema wazi Rais JK ni dhaifu na kaenda mbali zaidi kumsifia Mkapa na utawala wake. Mh. Sitta akiwa Spika aliwahi kusema "kiutu uzima" kuwa "wewe rais umekuwa mpole mno" Hapa kwa wenye kung'amua Sitta alitumia uungwana tu kukwepa kutumia neno DHAIFU. Angeweza kusema "wewe rais umekuwa DHAIFU mno". Pia mwandishi Kondo Tutindaga – katika MwanaHalisi ya tarehe 01 June 2011 iliyobeba kichwa cha mada "Ni ubaya wa Lowassa au udhaifu wa JK?" alitumia neno "UDHAIFU" kama kisifa cha Rais JK si chini ya mara 15. Upya uko wapi mpaka huyo Spika anampa Mnyika kupiga penalti kwenye goli lisilo na golikipa?!

Hapa chini ni baadhi ya waandishi wachache tu miongoni mwa Watanzania lukuki waliosema hadharani UDHAIFU wa Rais Kikwete
Mkuu Omutwale, haya yote usemayo ni ukweli mtupu!. Kwa sasa hali halisi ya CCM ni "sikio la kufa", au "la kuvunda"! na huku ni "kuvuja kwa pakacha!", nashauri tupunguze makelele, mwishowe mchuuzi atasikia kelele za kuvuja kwa pakacha akaamuru mchukuzi alitue pakacha lile kuliziba ndipo safari iendelee!. Tukinyamaza kimya, pakacha litaendelea kuvuja mpaka lifike tupu!.

Hili la udhaifu wa JK nililisema kule kwenye mada hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/230956-mapungufu-ya-jk-constructive-criticisim-4.html
na nilisema hivi
Wanabodi,
Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais weak"!,: asiyeweza kuchukua maamuzi magumu!.

Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

Nawatakia majadiliano mema.

Wasalaam

Pasco wa jf.

Baada ya kilichomkuta Mhe. JJ. Mnyika, nimepitia hii thread nikagundua kumbe kosa la Mnyika ni kuwa too bold to call a spade, a spade!.

Katika kumzungumzia JK, nilitoa angalizo lifuatalo "Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!." Inawezekana kabisa, Mhe. Ndungai amemtoa nje Mnyika kwa kuyaona matamshi yale siyo ya staha!, that being the case, Naibu Spika was Right!

Pasco.
 
Nilisema hapa kwenye huu uzi kuwa hawa akina Makinda pale wanapokaidi matakwa ya umma na kusiga utu na sheria wakidhani kuwa ndo wanaipa uhai serikali ya ccm, ndipo wanapozidi kusiliba kaburi lake. Ya jana Bungeni ni tukio la ushahidi mwingine wa hoja hii. Watu wanakufa Spika anang'ang'ania kuendesha vikao?!
 
Back
Top Bottom