Washauri wa Rais Magufuli walimpotosha, kumbe nahodha wa MV Nyerere hakuwa ‘deiwaka’

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Mwanza. Mhandisi wa Kivuko cha MV Nyerere, Alphonse Agustine Charahani aliyekaa majini kwa zaidi ya saa 48, amesema nahodha aliyekuwa zamu kivuko hicho kilipopinduka Septemba 20 ni msomi na mtaalamu mzoefu na si deiwaka (kibarua) kama inavyodaiwa.
Katika mazungumzo kwa njia ya simu leo Oktoba 7, 2018, mhandisi Charahani amesema, nahodha huyo Abel Constatine Mahatine ambaye pia alifariki katika ajali hiyo, alikuwa mhitimu na alikuwa amefanya shughuli hiyo kwa zaidi ya miaka 10.

"Hayo madai kwamba marehemu alikuwa ‘deiwaka’, nimekuja kuyasikia hapa nje. Kwa nini watu wasijiulize kwamba ‘deiwaka’ angepataje fursa ya kupeleka chombo kama kile kwa muda mrefu kiasi hicho?," Alihoji mhandisi.

Aliongeza kwamba, nahodha (marehemu) alikuwa zamu siku hiyo, wapo wawili wanapokezana na wala si deiwaka kama inavyodaiwa.

Kuhusu kupakia abiria na mizigo kupita kiasi, amesema hilo hawezi kulijibu kwa kuwa wakati wote wa shughuli ya upakiaji kazi yake inakuwa kuangalia na kurekebisha mitambo na kuhakikisha kwamba chombo kipo imara kwa ajili ya kuanza safari.

"Yani baada ya kufika hapa nje sasa ndiyo nimekutana na mambo mengi, hivi kweli itakuaje mimi nianze kuangalia idadi ya watu na mizigo badala ya kufungua na kujaribu injini kama ziko sawa? Mimi jukumu langu ni kuhakikisha kivuko kinang’oa na kutia nanga salama," amesema mhandisi Alphonse.

Amesema licha ya kwamba kuna baadhi ya wenzake bado wapo chini ya ulinzi kwa ajili ya mahojiano ameishukuru Serikali kwa kumruhusu kwenda nyumbani kwake.

Mhandisi huyo mkazi wa Kigongo Ferry, wilayani Misungwi amesema hana sababu maalum ya kuikacha kazi ya uhandisi majini akitolea mfano mafundi wa magari kwamba wakati gari linapopata ajali, mafundi na madereva wanaendelea na kazi kama kawaida.

"Hii ni ajali kama nyingine na siwezi kusema kwamba nimeacha kuwa mhandisi, hii ni mipango ya Mungu ukizingatia maili chache zilizokuwa zimebaki kabla ya kivuko kutia nanga," amesema.

Kuhusu kukaa majini kwa zaidi ya saa 48, amesema ni miujiza ya Mungu na kushukuru kwamba wakati kivuko hicho kinapinduka, alikuwa kwenye ofisi yake akiendelea na shughuli kama kawaida.

"Siwezi kusema moja kwa moja kwamba ninajua sababu ya kuzama kwa MV Nyerere lakini tu nahisi ni bahati mbaya baada ya nahodha kupotea kidogo na kutoka kwenye mstari. Nadhani katika kushtuka kwake ndipo aligeuza kivuko ghafla na kusababisha uzito kuelekea upande mmoja. Sina uhakika lakini," amesema Alphonse.

Mhandisi huyo amekana kuzungumzia suala la kuwa chini ya ulinzi mkali akiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando na kuongeza kwamba wakati wa kuzungumza hilo utafika.
Pia amebainisha kwamba kati ya watu 41 waliookolewa majini, watatu walikuwa wafanyakazi kwenye kivuko hicho na wanafanyiwa mahojiano.

Mhandisi Charahani aliokolewa zaidi ya saa 48 baada ya kupinduka kwa kivuko cha MV Nyerere katika kijiji cha Bwisya eneo la Ukara wilayani Ukerewe. Ni ajali ambayo ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 225.

Chanzo: Mwananchi.

MY TAKE:

Watu wamekuwa wakilalamikia Washauri na wanaomfikishia taarifa rais kwamba wanampa taarifa zisizo sahihi, Natokeo yake anapohutubia taifa au kuonge kwenye vyombo vya habari anakuwa anakosea bila kujua.

Taarifa ya Ikulu ilisema Nahodha ailikuwa deiwaka. Rais Magufuli amedokeza mambo yaliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo kuwa ni pamoja na nahodha wa kivuko hicho kuwa si mwenyewe ila ‘deiwaka.

Ni wakati wa kujitafakari, Mnapofikisha habari kwa rais, kumbuka anawakilisha wananchi wote na neno lake ni sheria. Anaweza saini adhabu ya kifo mtu akanyongwa kimakosa. kuweni makini

Habari zaidi, soma=>Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa! - JamiiForums
 
Ajari ni ajari tu. Unaweza kuwa mdhoefu mzuri wa jambo fulani kama unalifanya kwa kujiandaa lakini jambo hilo hilo ukiambiwa ulifanye katikati ya kifo unaweza kuhidwa hata na mtoto mdogo
 
Watu wamekuwa wakilalamikia Washauri na wanaomfikishia taarifa rais kwamba wanampa taarifa zisizo sahihi, Natokeo yake anapohutubia taifa au kuonge kwenye vyombo vya habari anakuwa anakosea bila kujua.
Tusilaumu watu mkuu, Jiwe ana hulka ya Uongo na inaonekana ni tatizo la malezi wala haliwezi kuanza leo akiwa Rais, ni mtu anayependa kusema UONGO hata pasipo na sababu ya kudanganya!
 
Mie ninavyojua Day worker ninavyosikia hasa madreva wa daladala, anakuwa ni dreva mwenye sifa zote lakini anakuwa hana chombo au gari la kuendesha la kudumu, anakuwa pale stand kusubiria dreva mwenzie atakayekuomba amshikie siku hiyo au hata tripu moja. Ana ganga njaa.
Kwa maana nyingine "deiwaka" sio kwamba hajasomea hapana, ila anakuwa sio mwajiriwa wa hicho chombo.
 
Mie ninavyojua Day worker ninavyosikia hasa madreva wa daladala, anakuwa ni dreva mwenye sifa zote lakini anakuna hana chombo au gari la kuendesha la kudumu, anakuwa pale stand kusubiria dreva mwenzie atakayekuomba amshikie siku hiyo au hata tripu moja. Ana ganga njaa.
Kwa maana nyingine "deiwaka" sio kwamba hajasomea hapana, ila anakuwa sio mwajiriwa wa hicho chombo.
Uko sahihi kwa maana nyingine daiwaka ni dereva msaidizi. Huyu injinia inaonekana kapaliwa na grease
 
Hivi nahodha mzoefu atashibdwa kulenga daraja? Nahodha mzoefu atakata kona kama bodabida? Nahodha mzoefu atakufa maji mita mia kutoka ufukweni?
Wanasema tatizo lilikuwa ni simu. Alijisahau akiongea na simu ndiyo hayo yote yakatokea. Madereva wa vyombo vyote vya usafiri wasiruhusiwe kuwa na simu kwenye cabin zao. Nadhani Lugola analifanyia kazi jambo hili.
 
Charahani wenzio walikuwa wanataka hata wewe udanje ili wakutwishe jumba bovu vinginevyo bila maelezo hayo wangebakije katika nafasi zao na Mzee Baba ndio alionunua kivuko unafikiri wananzengo wangemuelewa.

Tena wengine walisema kapiga msele kabisa sie wapanda vivuko tukabakiwa midomo wazi na hawa wanasiasa kwa uwongo na kukosa haya ila wataumbuka kwa mauaji yao.
 
Hivi nahodha mzoefu atashibdwa kulenga daraja? Nahodha mzoefu atakata kona kama bodabida? Nahodha mzoefu atakufa maji mita mia kutoka ufukweni?
Sina uhakika kwa vyombo vya majini lakini kwa usafiri wa angani, zaidi ya 90% ya ajali zote za ndege husababishwa na marubani wazoefu. Tafakari.
 
Back
Top Bottom