Washairi- Tunaweza Kujitegemea, Wachumi - Hatuwezi

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Kati ya mijadala iliyochukua muda wa wengi hapa jukwaani ni Je, Tanzania inaweza kujitegemea ghafla leo baada ya kuwa tegemezi kwa miaka yote? Ukifuatilia utagundua kuwa watu wenye upeo mdogo na wasio na Elimu ya uchumi (kama akina Polepole) ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuelezea kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegema kwa 100% hata kuanzia leo. Lakini wataalam wa uchumi na viongozi wa serikali wameeleza kuwa Tanzania bado tunahitaji kusaidiwa ili kuweza kusimama kwa miguu yetu kwa 100%. Baadhi ya wachumi na watendaji wa serikali wamelisema hilo wazi na wengine wamenyamaza kimya kwa kukosa ujasiri wa kutamka kile wanachokijua kuwa Tanzania haina uwezo wa kujitegemea kwa 100% kuanzia leo, japo uwezo huo upo kwa siku za mbeleni kama tutakuwa na mipango thabiti.

Magufuli alipozungumzia kuhusu kujitegemea alitoa kauli tata, alisema Tanzania ina uwezo wa kujitegemea, na ilistahili kuwa donor country, hakusema tunaweza kujitegemea kuanzia sasa. Hakusema tutakuwa donor country kuanzia sasa. Na nina uhakika Magufuli kamwe hatathubutu kutamka kuwa Tanzania tayari tunaweza kujitegema kuanzia sasa, japo uwezekano upo.Tafsiri yangu ni kuwa alimaanisha kuwa uwezo huo tunao japo hatujitegemei, na je ni lini tutajitegemea, na kwa mipango ipi? Ndiyo jambo tulilostahili hasa kulijadili.

Miongoni mwa hatua za kuelekea kujitegemea ni hiyo ya kusimamia ukusanyaji wa kodi, na kuongeza uwekezaji, matumizi mazuri ya fedha za serikali na uwajibikaji.

Kujitegemea ni process, siyo kila siku unasaidiwa katika kila kitu: barabara unajengewa, maji unaletewa, wagonjwa wako wote wa HIV wanapewa ARV na wageni, uzazi wa mipango unasaidiwa, huduma ya Mama na Mtoto unalipiwa, umeme unajengewa, madaraja unajengewa, mafunzo ya watendaji wako unagharamiwa, mafunzo ya majeshi unasaidiwa, silaha za kivita unanunuliwa, n.k., halafu uamke tu na kusema kuwa kuanzia kesho najitegema. Utakuwa kichaa! Mwenye hekima lazima atatuambia kuwa katika process ya kujitegemea, mpaka sasa barabara zote tunazijenga wenyewe, mwaka mwingine atatuambia maendeleo ya sekta ya kilimo yanagharamiwa na sisi wenyewe, n.k.

Ni ukweli huu ndiyo unaofanya manguli wote wa uchumi au kukaa kimya au kuishia tu kusema, tunasikitishwa kukatiwa misaada, tunatarajia watoaji wa misaada watafikiria upya uamuzi wao, na wengine kuamua kukaa kimya. Ila wale wasiojua hata A ya uchumi kama akina Polepole wanabaki wanapiga kerere za kujifurahisha kuwa tunaweza kujitegema kuanzia sasa.

Zimbabwe ilikuwa na uchumi imara zaidi ya mara 10 ya uchumi wa Tanzania.

Zimbabwe inachimba madini mengi kuliko Tanzania. Zimbabwe ina migodi ya kisasa ya precious metals kama gold, na ilikuwa nayo hata kabla ya Tanzania. Inachimba base metals kama Nickel, Copper, Zinc na Lead. Tanzania hatuna migodi ya madini hayo, copper kidogo inatoka pale Bulyanhulu kama by-product.

Zimbabwe ni nchi inayoongoza katika uchimbaji na uuzaji wa madini ya Lithium.

Zimbabwe inachimba industrial minerals kama limestone, dolomites na phosphates.

Zimbabwe ni nchi ya pili Duniani katika uchimbaji na uuzaji wa madini ya platinum (white gold).

Zimbabwe ina viwanda vya aina mbalimbali vinavyozalisha bidhaa zaidi ya 6,000.

Ni kutokana na uchumi huo imara wa Zimbabwe, Mugabe alifanya jeuri, akiiamini uchumi wake imara ungeweza kusimama wenyewe bila ya kuyategemea mataifa ya Ulaya Magharibi na Amerika akijidai kuwa analinda uhuru wa Taifa lake wa kuwapokonya wazungu mashamba na kuwapa wazungu. Zimbabwe hata wananchi wa vijijini walikuwa hawajui kununua nyanya zilizowekwa barabarani kwenye mchanga, walikuwa wananunua kwenye super markets zilizokuwa zimeenea nchi nzima.

Leo Zimbabwe haina hata sarafu yake yenyewe, inatumia dola ya marekani na Randi ya Afrika Kusini. Je hapo sasa Zimbabwe imekuwa na uhuru zaidi. Nchi kutokuwa na sarafu yake na kuamua kutumia sarafu za wale wale uliosema wanakuingilia uhuru wako, ni uhuru zaidi?

Watanzania tuna ule msemo kuwa mwenzio akinyolewa wewe tia maji, tusijifanye ni Vinjekitile tunapigwa risasi tunakufa wanaotuona tunakufa wanasema risasi hizo zimegeuka maji na damu inayomwagika ni maji. Binadamu mwenye akili hujifunza kupitia makosa ya mwenzake. Tusiwe kama nyumbu ambao wanaona aliyetangulia anaingia kwenye mto, analiwa na mamba mmoja, na yeye anaamini hatakamatwa kwa sababu yule mamba ameshiba kwa mla yule nyumbu wa kwanza bila ya kujua mto una mamba wengi.

Tanzania nchi maskini kabisa, tena kwa mbali ukilinganisha na Zimbabwe haina uwezo wa kushindana na haya mataifa makubwa, yatubidi tuwe werevu, twende nao kwa urafiki na uelewano, huku tukiendelea kujenga uwezo wetu wa kujitegemea. twende kwenye uhalisia, tusipelekwe na sifa au mihemuko ya kisiasa.

Tunataka utawala wa Magufuli ufanikiwe, kufanikiwa kwa utawala wake ni unafuu kwa watanzania na kufanikiwa kwa Tanzania kaa taifa. Tunakuomba magufuli, fanya jitihada zako zote, ujenge uhusiano wa karibu na ulio imara na jamii ya kimataifa. Tofauti ya kuwa na mahusiano mazuri na mahusiano mabaya gharama yake ni kubwa mno. Zimbabwe kimaendeleo imerudi nyuma zaidi ya ilivyokuwa miaka 20 iliyopita, sahizi Mugabe amesalimu amri, wazungu wameanza kupewa ardhi, lakini muda umepotea na fursa zimetoweka.
 
haahaaa, washairi ni noma ila wanasema hivyo kwa sababu za kisiasa tu, ila ukweli ni kuwa Tanzania inaweza kujitegemea lakini sio kitu cha kutokea ghafla kisa umenyimwa misaada ni process ndefu, ambayo inaanzia kwenye ngazi ya chini kabisa...kuboresha elimu yetu na kufanya kazi

watu wana import zaidi ya 80% ya bidhaa zao na hawana chanzo cha kueleweka cha kujipatia fedha za kigeni wanazungumzia kujitegemea.......

ukiongea ukweli kama huu mtu ataanza kukuambia unaabudu wazungu, wakati muda huo huo unategemea wazungu waje kuchimba madini yenu, kunua korosho au kahawa,waje wawekeze ili ajira ziongezeke au wafanye utalii ili mpate fedha za kigeni
(ambazo ndio za hao hao wazungu) kwa ajili ya ku import bidhaa kutoka kwa hao hao wazungu
 
Huu ni uchambuzi murua. Kwanza sera za uchumi za serikali ya CCM zimejengwa kwenye misingi ya mfumo wa uliberali mamboleo (neo-liberal economic system) ambazo zenyewe ni kifungo cha kuendelea kutegemea "wafadhili" kutoka nchi za magharibi. Chini ya sera hizi ambazo zinajikita katika kunufaisha wawekezaji wa nje (na kuzidisha umaskini wa wananchi) chini ya uchumi wa soko huria (soko holela) na utandawazi (utandawizi), uchumi wa nchi umewekwa mikononi mwa wageni. Ndio maana sekta zote zinazochangia kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi (mawasiliano, fedha [mabenki], ujenzi, madini, utalii) zinamilikiwa na wageni. Tatizo ni kwamba mikataba ya uwekezaji katika maeneo haya ilikuwa na kipengele cha misamaha wa kodi (tax holidays) ya muda mrefu. Katika mazingira haya nchi itaachaje kuendelea kutegemea misaada ya wafadhili wakati haipati mapato ya kodi kutokana na sekta kuu za uchumi? Sera za uchumi za uliberali mamboleo ni majanga. Na hapo Magufuli hafurukuti!
 
Somo kama hili kwa wafuasi wa kusifia awatalielewa na kinachonichosha zaidi ni kuona hata polepole nae amekua mchumi serikali
 
haahaaa, washairi ni noma ila wanasema hivyo kwa sababu za kisiasa tu, ila ukweli ni kuwa Tanzania inaweza kujitegemea lakini sio kitu cha kutokea ghafla kisa umenyimwa misaada ni process ndefu, ambayo inaanzia kwenye ngazi ya chini kabisa...kuboresha elimu yetu na kufanya kazi

watu wana import zaidi ya 80% ya bidhaa zao na hawana chanzo cha kueleweka cha kujipatia fedha za kigeni wanazungumzia kujitegemea.......

ukiongea ukweli kama huu mtu ataanza kukuambia unaabudu wazungu, wakati muda huo huo unategemea wazungu waje kuchimba madini yenu, kunua korosho au kahawa,waje wawekeze ili ajira ziongezeke au wafanye utalii ili mpate fedha za kigeni
(ambazo ndio za hao hao wazungu) kwa ajili ya ku import bidhaa kutoka kwa hao hao wazungu
Na kwa kuongezea hapo katika nyekundu, na pia kuvaa mawigi ya nywele zao na mbwembwe ziendenazo na hizo nywele na kujichubua kwa mikorogo ili angaa tufanane nao kidogo - yaani tunachukia asili yetu wenyewe na kutamani kuwa kama wao:(
 
Y
Kati ya mijadala iliyochukua muda wa wengi hapa jukwaani ni Je, Tanzania inaweza kujitegemea ghafla leo baada ya kuwa tegemezi kwa miaka yote? Ukifuatilia utagundua kuwa watu wenye upeo mdogo na wasio na Elimu ya uchumi (kama akina Polepole) ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuelezea kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegema kwa 100% hata kuanzia leo. Lakini wataalam wa uchumi na viongozi wa serikali wameeleza kuwa Tanzania bado tunahitaji kusaidiwa ili kuweza kusimama kwa miguu yetu kwa 100%. Baadhi ya wachumi na watendaji wa serikali wamelisema hilo wazi na wengine wamenyamaza kimya kwa kukosa ujasiri wa kutamka kile wanachokijua kuwa Tanzania haina uwezo wa kujitegemea kwa 100% kuanzia leo, japo uwezo huo upo kwa siku za mbeleni kama tutakuwa na mipango thabiti.

Magufuli alipozungumzia kuhusu kujitegemea alitoa kauli tata, alisema Tanzania ina uwezo wa kujitegemea, na ilistahili kuwa donor country, hakusema tunaweza kujitegemea kuanzia sasa. Hakusema tutakuwa donor country kuanzia sasa. Na nina uhakika Magufuli kamwe hatathubutu kutamka kuwa Tanzania tayari tunaweza kujitegema kuanzia sasa, japo uwezekano upo.Tafsiri yangu ni kuwa alimaanisha kuwa uwezo huo tunao japo hatujitegemei, na je ni lini tutajitegemea, na kwa mipango ipi? Ndiyo jambo tulilostahili hasa kulijadili.

Miongoni mwa hatua za kuelekea kujitegemea ni hiyo ya kusimamia ukusanyaji wa kodi, na kuongeza uwekezaji, matumizi mazuri ya fedha za serikali na uwajibikaji.

Kujitegemea ni process, siyo kila siku unasaidiwa katika kila kitu: barabara unajengewa, maji unaletewa, wagonjwa wako wote wa HIV wanapewa ARV na wageni, uzazi wa mipango unasaidiwa, huduma ya Mama na Mtoto unalipiwa, umeme unajengewa, madaraja unajengewa, mafunzo ya watendaji wako unagharamiwa, mafunzo ya majeshi unasaidiwa, silaha za kivita unanunuliwa, n.k., halafu uamke tu na kusema kuwa kuanzia kesho najitegema. Utakuwa kichaa! Mwenye hekima lazima atatuambia kuwa katika process ya kujitegemea, mpaka sasa barabara zote tunazijenga wenyewe, mwaka mwingine atatuambia maendeleo ya sekta ya kilimo yanagharamiwa na sisi wenyewe, n.k.

Ni ukweli huu ndiyo unaofanya manguli wote wa uchumi au kukaa kimya au kuishia tu kusema, tunasikitishwa kukatiwa misaada, tunatarajia watoaji wa misaada watafikiria upya uamuzi wao, na wengine kuamua kukaa kimya. Ila wale wasiojua hata A ya uchumi kama akina Polepole wanabaki wanapiga kerere za kujifurahisha kuwa tunaweza kujitegema kuanzia sasa.

Zimbabwe ilikuwa na uchumi imara zaidi ya mara 10 ya uchumi wa Tanzania.

Zimbabwe inachimba madini mengi kuliko Tanzania. Zimbabwe ina migodi ya kisasa ya precious metals kama gold, na ilikuwa nayo hata kabla ya Tanzania. Inachimba base metals kama Nickel, Copper, Zinc na Lead. Tanzania hatuna migodi ya madini hayo, copper kidogo inatoka pale Bulyanhulu kama by-product.

Zimbabwe ni nchi inayoongoza katika uchimbaji na uuzaji wa madini ya Lithium.

Zimbabwe inachimba industrial minerals kama limestone, dolomites na phosphates.

Zimbabwe ni nchi ya pili Duniani katika uchimbaji na uuzaji wa madini ya platinum (white gold).

Zimbabwe ina viwanda vya aina mbalimbali vinavyozalisha bidhaa zaidi ya 6,000.

Ni kutokana na uchumi huo imara wa Zimbabwe, Mugabe alifanya jeuri, akiiamini uchumi wake imara ungeweza kusimama wenyewe bila ya kuyategemea mataifa ya Ulaya Magharibi na Amerika akijidai kuwa analinda uhuru wa Taifa lake wa kuwapokonya wazungu mashamba na kuwapa wazungu. Zimbabwe hata wananchi wa vijijini walikuwa hawajui kununua nyanya zilizowekwa barabarani kwenye mchanga, walikuwa wananunua kwenye super markets zilizokuwa zimeenea nchi nzima.

Leo Zimbabwe haina hata sarafu yake yenyewe, inatumia dola ya marekani na Randi ya Afrika Kusini. Je hapo sasa Zimbabwe imekuwa na uhuru zaidi. Nchi kutokuwa na sarafu yake na kuamua kutumia sarafu za wale wale uliosema wanakuingilia uhuru wako, ni uhuru zaidi?

Watanzania tuna ule msemo kuwa mwenzio akinyolewa wewe tia maji, tusijifanye ni Vinjekitile tunapigwa risasi tunakufa wanaotuona tunakufa wanasema risasi hizo zimegeuka maji na damu inayomwagika ni maji. Binadamu mwenye akili hujifunza kupitia makosa ya mwenzake. Tusiwe kama nyumbu ambao wanaona aliyetangulia anaingia kwenye mto, analiwa na mamba mmoja, na yeye anaamini hatakamatwa kwa sababu yule mamba ameshiba kwa mla yule nyumbu wa kwanza bila ya kujua mtamamba wengi.

Tanzania nchi maskini kabisa, tena kwa mbali ukilinganisha na Zimbabwe haina uwezo wa kushindana na haya mataifa makubwa, yatubidi tuwe werevu, twende nao kwa urafiki na uelewano, huku tukiendelea kujenga uwezo wetu wa kujitegemea. twende kwenye uhalisia, tusipelekwe na sifa au mihemuko ya kisiasa.

Tunataka utawala wa Magufuli ufanikiwe, kufanikiwa kwa utawala wake ni unafuu kwa watanzania na kufanikiwa kwa Tanzania kaa taifa. Tunakuomba magufuli, fanya jitihada zako zote, ujenge uhusiano wa karibu na ulio imara na jamii ya kimataifa. Tofauti ya kuwa na mahusiano mazuri na mahusiano mabaya gharama yake ni kubwa mno. Zimbabwe kimaendeleo imerudi nyuma zaidi ya ilivyokuwa miaka 20 iliyopita, sahizi Mugabe amesalimu amri, wazungu wameanza kupewa ardhi, lakini muda umepotea na fursa zimetoweka.
You have hit the nail on the head Msambichaka. Kwanza, ilikwa lazima tusubiri wahisani watukatie msaada ndipo tuanza kuzungumza lugha ya kujitegemea? Viongozi wetu wasitupeleke njia ya Zimbabwe. Waongee na washirika na kukubaliana namna ya kurekebisha mambo. Kamwe tusirubuniwe na blah blah za akina Polepole
 
Yaani wachumi ambao wanashindwa kudevelop theories za kuwezesha nchi kujitegemea wanasubiri kurejea theories za capitalistas na imperialists lazima wawaze hivyo.
 
Aisee umegonga kwenye mfupa!! Bwana Magu alipoingia ikulu akakusanya yale mafuriko ya arears akadhani amefika!! Kadiri muda unavyosonga mapato yanarudi nyuma!! Sasa ameanza kung'amua!! Leo hata watu wanaoonekana wameathiriwa vibaya na lishe mbovu kama akina Pole pole eti nao wanajifanya wataalamu wa uchumi!!! Ama kweli washairi wanatupeleka kubaya!!
 
fantastic
 
Tatizo tulilonalo kwa sasa ni Maono, tegemea uchumi kurudi nyuma ndani ya utawala huu

Ndoto ya Nchi ya viwanda ilikuwa ni hekaya za alfu lela ulela ki uhalisia bado tuna safari ndefu tuache kuota mchana ndoto za alinacha "kujitegemea" bado sana .

Kuleta siasa ndani ya maswala mazito ya kiuchumi ni ulevi wa hatari
 
Mshairi mkubwa hapa jukwaani ni@jingalao
subirini aje na pumba zake
 
Kati ya mijadala iliyochukua muda wa wengi hapa jukwaani ni Je, Tanzania inaweza kujitegemea ghafla leo baada ya kuwa tegemezi kwa miaka yote? Ukifuatilia utagundua kuwa watu wenye upeo mdogo na wasio na Elimu ya uchumi (kama akina Polepole) ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuelezea kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegema kwa 100% hata kuanzia leo. Lakini wataalam wa uchumi na viongozi wa serikali wameeleza kuwa Tanzania bado tunahitaji kusaidiwa ili kuweza kusimama kwa miguu yetu kwa 100%. Baadhi ya wachumi na watendaji wa serikali wamelisema hilo wazi na wengine wamenyamaza kimya kwa kukosa ujasiri wa kutamka kile wanachokijua kuwa Tanzania haina uwezo wa kujitegemea kwa 100% kuanzia leo, japo uwezo huo upo kwa siku za mbeleni kama tutakuwa na mipango thabiti.

Magufuli alipozungumzia kuhusu kujitegemea alitoa kauli tata, alisema Tanzania ina uwezo wa kujitegemea, na ilistahili kuwa donor country, hakusema tunaweza kujitegemea kuanzia sasa. Hakusema tutakuwa donor country kuanzia sasa. Na nina uhakika Magufuli kamwe hatathubutu kutamka kuwa Tanzania tayari tunaweza kujitegema kuanzia sasa, japo uwezekano upo.Tafsiri yangu ni kuwa alimaanisha kuwa uwezo huo tunao japo hatujitegemei, na je ni lini tutajitegemea, na kwa mipango ipi? Ndiyo jambo tulilostahili hasa kulijadili.

Miongoni mwa hatua za kuelekea kujitegemea ni hiyo ya kusimamia ukusanyaji wa kodi, na kuongeza uwekezaji, matumizi mazuri ya fedha za serikali na uwajibikaji.

Kujitegemea ni process, siyo kila siku unasaidiwa katika kila kitu: barabara unajengewa, maji unaletewa, wagonjwa wako wote wa HIV wanapewa ARV na wageni, uzazi wa mipango unasaidiwa, huduma ya Mama na Mtoto unalipiwa, umeme unajengewa, madaraja unajengewa, mafunzo ya watendaji wako unagharamiwa, mafunzo ya majeshi unasaidiwa, silaha za kivita unanunuliwa, n.k., halafu uamke tu na kusema kuwa kuanzia kesho najitegema. Utakuwa kichaa! Mwenye hekima lazima atatuambia kuwa katika process ya kujitegemea, mpaka sasa barabara zote tunazijenga wenyewe, mwaka mwingine atatuambia maendeleo ya sekta ya kilimo yanagharamiwa na sisi wenyewe, n.k.

Ni ukweli huu ndiyo unaofanya manguli wote wa uchumi au kukaa kimya au kuishia tu kusema, tunasikitishwa kukatiwa misaada, tunatarajia watoaji wa misaada watafikiria upya uamuzi wao, na wengine kuamua kukaa kimya. Ila wale wasiojua hata A ya uchumi kama akina Polepole wanabaki wanapiga kerere za kujifurahisha kuwa tunaweza kujitegema kuanzia sasa.

Zimbabwe ilikuwa na uchumi imara zaidi ya mara 10 ya uchumi wa Tanzania.

Zimbabwe inachimba madini mengi kuliko Tanzania. Zimbabwe ina migodi ya kisasa ya precious metals kama gold, na ilikuwa nayo hata kabla ya Tanzania. Inachimba base metals kama Nickel, Copper, Zinc na Lead. Tanzania hatuna migodi ya madini hayo, copper kidogo inatoka pale Bulyanhulu kama by-product.

Zimbabwe ni nchi inayoongoza katika uchimbaji na uuzaji wa madini ya Lithium.

Zimbabwe inachimba industrial minerals kama limestone, dolomites na phosphates.

Zimbabwe ni nchi ya pili Duniani katika uchimbaji na uuzaji wa madini ya platinum (white gold).

Zimbabwe ina viwanda vya aina mbalimbali vinavyozalisha bidhaa zaidi ya 6,000.

Ni kutokana na uchumi huo imara wa Zimbabwe, Mugabe alifanya jeuri, akiiamini uchumi wake imara ungeweza kusimama wenyewe bila ya kuyategemea mataifa ya Ulaya Magharibi na Amerika akijidai kuwa analinda uhuru wa Taifa lake wa kuwapokonya wazungu mashamba na kuwapa wazungu. Zimbabwe hata wananchi wa vijijini walikuwa hawajui kununua nyanya zilizowekwa barabarani kwenye mchanga, walikuwa wananunua kwenye super markets zilizokuwa zimeenea nchi nzima.

Leo Zimbabwe haina hata sarafu yake yenyewe, inatumia dola ya marekani na Randi ya Afrika Kusini. Je hapo sasa Zimbabwe imekuwa na uhuru zaidi. Nchi kutokuwa na sarafu yake na kuamua kutumia sarafu za wale wale uliosema wanakuingilia uhuru wako, ni uhuru zaidi?

Watanzania tuna ule msemo kuwa mwenzio akinyolewa wewe tia maji, tusijifanye ni Vinjekitile tunapigwa risasi tunakufa wanaotuona tunakufa wanasema risasi hizo zimegeuka maji na damu inayomwagika ni maji. Binadamu mwenye akili hujifunza kupitia makosa ya mwenzake. Tusiwe kama nyumbu ambao wanaona aliyetangulia anaingia kwenye mto, analiwa na mamba mmoja, na yeye anaamini hatakamatwa kwa sababu yule mamba ameshiba kwa mla yule nyumbu wa kwanza bila ya kujua mto una mamba wengi.

Tanzania nchi maskini kabisa, tena kwa mbali ukilinganisha na Zimbabwe haina uwezo wa kushindana na haya mataifa makubwa, yatubidi tuwe werevu, twende nao kwa urafiki na uelewano, huku tukiendelea kujenga uwezo wetu wa kujitegemea. twende kwenye uhalisia, tusipelekwe na sifa au mihemuko ya kisiasa.

Tunataka utawala wa Magufuli ufanikiwe, kufanikiwa kwa utawala wake ni unafuu kwa watanzania na kufanikiwa kwa Tanzania kaa taifa. Tunakuomba magufuli, fanya jitihada zako zote, ujenge uhusiano wa karibu na ulio imara na jamii ya kimataifa. Tofauti ya kuwa na mahusiano mazuri na mahusiano mabaya gharama yake ni kubwa mno. Zimbabwe kimaendeleo imerudi nyuma zaidi ya ilivyokuwa miaka 20 iliyopita, sahizi Mugabe amesalimu amri, wazungu wameanza kupewa ardhi, lakini muda umepotea na fursa zimetoweka.

Mkuu umeandika point hadi umenikumbusha yule prof. Msambichaka pale udsm. Jee mkuu una udugu naye nini prof. Vipi bado yupo hai ?
 
Yale majipu yote yaliyokuwa yampa kiburi anatembea na media yameisha muda si mrefu ataanza kutapatapa nakulia kama punda
 
Kweli JPM kuna wakati alianza kuropoka ropoka bila kuwa na facts za uchumi! Naona sasa atakuwa anaweka akiba ya maneno:
 
Umeongea vizuri Chief,wakati mwingine hata vyombo vyetu vya habari ni shida,kuna mijada mingine inayohitaji wataalam wa mambo ya uchumi wenyewe wanaalika wanasiasa.!
 
Hawa wanaoongea kujitegemea sijui wanachukuliaga vigezo vipi, mtu kama huyu PolePole ni wa kufunga kwa sababu anapotosha jamii na kutuchonganisha na nchi wahisani
 
Back
Top Bottom